Ukitaka kufeli kwenye kila jambo basi jipime kwa aliyefeli.
Ukitaka kufanikiwa basi jipime kwa aliyefanikiwa.
Mfano:
Tumepoteza mechi ya UCL fainali dhidi ya Real Madrid mara mbili mfululizo, sasa dalili ya kufeli ni kusema mbona Arsenal hana UCL hata moja? Hatutakiwi kujipima kwa aliyefeli bali tunachopaswa kujipima naye ni kusema kwanini na sisi tunashindwa kufikia mafanikio ya Real Madrid ya kubeba UCL 14?
So, si busara kujipima kwa Ferguson kuchukua EPL 1 kwa miaka 7 bali ni busara kujipima kwa Pep kubeba EPL 4 ndani ya Miaka 5.
Nawasilisha.
Naunga mkono hoja. Ukitaka kufanikiwa tembea na aliefanikiwa.
Ingekua amri yangu ingekua tunakwenda jino kwa jino kwa Pep kwenye upana na uimara wa kikosi ili kuleta matokeo tunayohitaji lakini kila nikiwaza ni kama vile ma bosi wetu wana ridhika na ushiriki wa UCL kwa sababu hata kufika fainali mpunga wa maana upo...
Inakua hivi Liverpool kimahesabu pesa za TV msimu uliopita watakaua wamepata mapesa ya kutosha tena wakiwazidi hata Pep kwa kuweza kufika fainali UCL... Mapato haya naona kwa FSG wanaona sawa kwa kusajili kiduchu na kuingiza ela kama hizi inakua ahueni kwao sababu hata mishahara wanalipa kiasi...
Kimsingi FSG wananufaika zaidi na Liverpool kuliko Liverpool anavyonufaika na FSG... Pep aliwai kusema kama ela ipo Manchester City kwa nini asinunue wachezaji anaowataka? Kwa hio Pep kua na kikosi kipana na kushinda EPL zote hizi ni sababu sapoti anapewa...
Klopp kwa mara ya kwanza hili swali la usajili wa Midfielder lilimtoa kwenye comfort zone yake akapaniki balaa na kusema yeye sio mtu sahihi kuulizwa mambo ya usajili...
Mpira sasa umekua ni ishu ya pesa hakuna kingine zaidi ya smart buying, zile zama za kutengeza wachezaji kupitia academy zimeisha hivyo ni kununua kununua kununua,.. Kuna maswali mengi hua hayana majibu tazama ishu kama ya Ox huyu alitakiwa dirisha linafunguliwa awe wa kwanza kuondoka...
Pep alimwachia David Silva akiwa kwenye peak kwa kuona Foden anaweza kucheza vyema nafasi yake. Ingekua Liverpool naamini mpaka sasa Silva angekua Liverpool tungekua nae bado... Kazi ipo.
Kama ni ku aim lets topple Pep kwanza kwenye EPL aafu tujitzamaze kwenye UCL kukomaa na Real Madrid.
YNWA