Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Dogo anajituma kuliko huyo ulomfananisha
 
Mtu pekee atakayeondoka Liverpool hii na itetereke ni Jurgen Nobert Klop basi siyo mane Wala Salah Wala mtu yeyote yule

Hivi Kati ya fabinho na Mane Nani alikuwa akimiss game timu inaflop??
Mane
 
Bosi kasema hapo kati an Eliot na Chambali tusiwe na shaka
 
Unakubali Harvey Elliot ni kiungo ategemewe?
 
Nunez tumepgwa wazee, bora tukampgie Mane magoti arudi kuokoa jahazi. Msimu ujao liva naiona nafas 10

Hizo kelele tumeshazoea,ingekuwa beki kaondoka sawa utasema sasa tutakuwa uchocholo.

Hazitutishi hizo kelele.
 
Mimi hofu yangu kwenye Midfield ni upande wa DM tu kama fabinho akipata majeraha au akichoka hatuna like for like replacement yake lakini kwingine sina hofu sana.
Yupo Henderson duuh..

Yupo Morton....

Yupo Milner...

Sasa pata picha hao hapo tukutane na Brighton au Spurs...

Klopp hakukosea kwenda mazima kwa Tchouameni alijua fika waliopo sio tegemezi mia kwa mia lakini baada ya kumkosa Tchouameni mwenyewe akaona isiwe tabu abadili mfumo kutoka 4 3 3 na sasa kwenda na 4 2 3 1...

Ina maaana

4 Trent Konate VVD Robo
2 Fabinho Thiago
3 Diaz Jota Salah
1 Nunez

Bado mapema kutoa hukumu kuhusu huo mfumo kwani hata mechi ya Bangkok alianza na 4 3 3.

YNWA
 
Msimu ujao mutamkataa Klopp..huyu jamaa Ni Mwinyi Zahera mweupe...
😂 😂 😂 😂 😂 Wewe mwenyewe ulitonywa humu Lukaku(@£97m+) umepigwa hukuamini zaidi ya ulikomaa ni Chelsea bingwa teh teh teh labda ubingwa wa play station.....

Vipi Ronaldo aka CR7 anatua lini Chelsea aje kulinda rekodi magoli yake ya Uefa eti Messi asiyapunguze 😂😂😂...

YNWA
 
Tuchel hamtaki.
 
Naona Jota tayari kapata majeruhi, naombea tu huo mfumo wa 4231 u click mapema. Ile 433 kuna baadhi ya timu zimeshajua namna ya kutukabili.
 
Naona Jota tayari kapata majeruhi, naombea tu huo mfumo wa 4231 u click mapema. Ile 433 kuna baadhi ya timu zimeshajua namna ya kutukabili.
Hilo lipo wazi na hata makocha wanasema sasa kuna umuhimu wa kubadili mfumo kutokana na kikosi kilichopo...

4 3 2 1 ya Klopp akiwa Dortmund ilivyokua inafanya kazi.




Huu mfumo aliwai kuutumia Dortmund wakashinda Ligi 2011 na 2012 hivyo sio mgeni kwa Klopp kama endapo wachezaji watauelewa mapema itakua jambo njema kwetu na pia sio mara ya kwanza kwa Klopp kutumia huu mfumo hapa Liverpool actually baada ya Coutinho kuodoka naona ndio alizidi kukomaa na attacking 4 3 3.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…