Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ujio wa calvin ramsay liverpool naona kama vile TAA anapata nafasi mpya ya kucheza ndani ya uwanja
 
Uwe na heshima kidogo na suarez.. Unapomtaja suarez ni striker class moja na kina benzema na lewandowski, humo ndani, darwin bado hajaonesha jambo, mpeni muda kwanza.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hakukuwa na kingine zaidi ya kuumia mara kwa mara, ilifikia wakati Agger kila baada ya mechi moja au mbili anaumia, na akipona hawezi kuwa kwenye form lazima apate match fitness, na timu kubwa nyingi zilikuwa zinamtaka ukiachilia mbali za Uingereza pia za Spain, Italy na German zilikuwa zinamtaka, ila mwenyewe alitamka kwa kauli yake kuwa, kama angeweza kucheza ligi ya ushindani angebakia Liverpool baadae ndio Liverpool wakambia atafute maisha mapya ya soka na yeye baada ya kufunguliwa mlango alisema anataka akacheze ligi yenye ushindani mdogo ili kuendana na hali yake ya afya. Ndio akahamia timu yake ya toka utotoni ya Brondby
 
Yeah dogo majeruhi yalimkomalia sana lakini mapenzi yake kwa Liverpool hayakua na kificho.

YNWA
 
DNS kwa drip hii lazima Mgonjwa apige chafya tu
Ni mwendo wa 4 3 2 1 kumekucha.....
Wapinzani watulie maana tunakuja kivingine kabisaa msimu ujao.

DNS ina ridhi rasmi SMF na kwa mahesabu haya ya Klopp sasa ni kwamba hata RB na LB wanaeda kupunguziwa majukumu kwa mfumo mpya..

Klopp ni revolutionary kule Dortmund alikua na anatumia sana 4 3 2 1 lakini tangu atue Liverpool amekua 4 3 3 ambayo hubadilika 4 1 4 1 au 2 1 4 3 na sasa tetesi ni kwamba anahamia rasmi 4 2 3 1 kwa vile sasa ana wachezaji sahihi wa kuleta huo mfumo klabuni.. Usajili wa Fabio na Nunez ni kimkakati.


YNWA
 
Kujiamini ndiyo vizuri kabisa aisee... halafu wangempa six years huyu kabisa!
Kabisa alikua na ofa tangu January 2022 kwenda Italia lakini akasema ngoja msimu uishe atazame haswa wapi panamfaa na kwa Uingereza Leeds, Brighton na Southampton walikua mstari wa mbele kumsaka, kilichomvutia zaidi ni kuona kwa Liverpool vijana chipukizi wanapewa nafasi team A baada ya Trent, Jones, Elliott kupata dakika za kutosha huku pia kucheza na wachezaji hodari kama VVD, Robertson nk wakimvutia bila shaka na lile hug la Klopp nalo akilitamani na amechagua vyema mahala sahihi...

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…