Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mkuu kweli nimeamini kuna watu mnajua kuchambua mpira,unaweza ukamuona mchezaji kwenye mechi fulani hayupo fit kumbe kuna hesabu tu unakuta hakufanyika vizuri na kocha.
 
Imagine Being Us
Mkuu wacha na Sisi tufurahi, tumepitia magumu mno, tulisemwa sana. Mara Liverpool ina miaka 30 bila ubingwa wa epl, mara hakuna kombe la maana kwa karibuni tofauti na UEFA ya 2005.

Ile 2008 kuna wanoko walichukua makombe yote waliyoshiriki wakawa na midomo kama tarumbeta, mbaya zaidi ile 2009 Madrid (tunawadai pakubwa sana) wakatupokonya Alonso, timu ikawa kama imekatika. Literally first eleven ilikuwa ni Reina, Gerald, na Torres. Kuna kipindi hadi UEFA tunaiangalia kwenye TV tu, siye zetu ilikuwa Alihamisi tukabondwe na kina Atiletico, Sevila, Valencia na Vila real(hawa ndio walikuwa wamiliki wa europa cup).
Sasa hivi tunachukulia for granted kuangalia Liverpool akicheza fainali tatu kubwa Ulaya ndani ya msimu mmoja zingatia nafasi aliyonayo ya kuchukua EPL, lakini tusisahau miaka kumi nyuma ndoto zetu kwenye msimu ilikuwa kumaliza top four EPL(It was not easy being us). Maswala ya ubingwa wa FA, EPL, UEFA, yalikuwa ya kina Man UTD, Chelsea, Real Madrid, Baryurn, Barcelona n.k ambao kwa sasa wana wish wakutane na Shetani kuliko Liverpool. Wakikutana na Shetani watafanya maombi na Dua kumkabili lakini hakuna mbinu au silaha itokayo Peponi ama Jehanamu inayoweza kuikabili Liver.

Jurgen Klopp anastahili credit kwenye hii revolution iliyotokea ndani ya Liverpool. Mambo aliyofanikisha ndani ya miaka 7 inawafanya watu wamuone kama vile ana miaka 3 tu, yaani bado tunamuona ni mpya.
Iwapo Liver atafanikiwa kuchukua quadruple itakuwa ni mapinduzi mengine ndani ya LFC. Itaifanya Liver iwe the brightest football brand in Europe. Makampuni makubwa, mashabiki wapya, wachezaji mastaa wakubwa watataka kujihusisha na Liverpool, then automatically LFC itajiseti kwenye momentum ya kutawala soka la Ulaya kwa miaka kadhaa ijayo.
The future is bright, YNWA.
 
Na akibeba UCL, linafuata
Europa super cup,
World club cup
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…