Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Ukisikia kupumuliwa ndio huku sasa, pointi moja alafu wote mko njema....
 
Me naona tucheze kama tunavo cheza kila siku, uzuri nikwamba wao wametusoma lakin na klopp pia kawasoma

Sawa mkubwa, ila unajua na unakumbuka mwaka juz rodgers alitaka kufanya nn na leicester city, we unahisi au unajua kwann alikaza vile wakat alikua hana chakupoteza.

Au kwann asernal alikuja amekaza meno kwenye gemu yetu ya marudio we unahisi hakukua na Pep connection

Ebu ngoja tuone iyo gemu
 
Mwendo ni ule ule tuchukue kila gemu moja moja na tushinde mengine tutayakuta mwisho wa Msimu hakuna namna.

YNWA
 
Kabisa mkuu, maana walijua kufungwa lazima wafungwe tu ila yule Dogo Gordon alitupeleka mkuu sijui aliikamia game?



πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Aisee El Cholo jana alikua kwa majirani lakini nina imani na vijana wapo vizuri.

Klopp kwa kweli hua sijui hawa wachezaji anawaambia maneno gani maana tazama Origi asie cheza lakini jana kaingia na moto utadhani ndio super sub wakati wote yaaani big up Klopp.

YNWA
 
Sisi kucheza vizuri inategemea katikati kacheza nani, hiyo mechi ya sare na Brighton kati alicheza ox, Jones na Milner na Henderson yaani viungo wengine hawakuwepo lakini hata leicester ilikuwa hivyo hivyo.
Duuh huyu Miller na ndio Klopp anakomaa eti apewe mkataba wakati naona sasa anachokiweza na kupiga viatu wachezaji. Hivi ile gemu ya Chelsea unakumbuka goli la kwanza alimla kiatu Pulisc wakapata faulo kupigwa ndio akafunga Mateo kwa huyu Milner hana msaada wowote aodoke.. Tena ile faulo alimpiga kiatu mara ya kwanza dogo akakwepa lakini mara ya mpili akampata na haikua move ya hatari ki vile. Hakika Klopp amuache asepe zake Leeds ama Aston Villa.

YNWA
 


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Allison bhana hakusubiri msimu ujao maana hawajulikana watacheza wapi kamlipa Pickford jana ile ile πŸ˜‚πŸ˜‚

YNWA
 

Ubora gani kwa Watford bana?
One against one Watford walipoteza nafasi tatu.
Akicheza vile kama Watford mechi zijazo nina uhakika 100% Liverpool ni bingwa
 
Brenford tulikua up 3-1 eti zikarudi ikawa 3-3
chelsea tukaongoza vizuri 2-0 eti zikarudi ghafla tuu, hata ile mechi na City Anfield ilikua yetu kabisa, Juzi tuu FA na City half time 3-0 ila hadi mechi inaisha tumebana mbupu, mi nahisi hatuna wachezaji wenye costistency ya juu kabisa ama saa zingine mbinu nk,

Mbinu rahisi ya kuishinda City ni kuwa na high lever ya consistency mwanzoni kabisa mwa ligi na katikati, wao wakiwa na point 50 wewe una 60 huko
 
Kama umefuatilia press conference nyingi za Klopp utaona kwenye gemu zote ambazo hua tunatokea kushinda kibishi amekua akisisitiza hilo unalosema wewe hapo kwamba slim na slight moments zinaweza kubadili upepo wa gemu muda wowote na utamsikia akisema.. 'wachezaji walisinzia dakika 30 za mwanzo ama kipindi cha pili walisinzia sana dakika 80 nk... Hivyo sio kwamba hatuna consistency mbali ni kasoro za ki mchezo ambazo wenzetu wamezitumia vyema kutuumiza kama ile gemu ya Brentford yaaani tuliomba sie mechi iishe maana walikua wanakuja.

Bila consistency hata nafasi ya pili hatupo wala pointi moja hii haipo.

Kuna gemu tumeshinda 1 bila sasa ndio utaona kuna gemu hawa jamaa hawajasinzia kabisa umakini unakuwepo.

YNWA
 
Ubora gani kwa Watford bana?
One against one Watford walipoteza nafasi tatu.
Akicheza vile kama Watford mechi zijazo nina uhakika 100% Liverpool ni bingwa
Aisee moja ya sifa ya bingwa mtarajiwa ni kushinda hata akiwa na siku mbaya kazini na kwa namna ubao wa magoli ulivyosoma pale Ethad haikua siku mbaya kwa Kipara maana pamoja na kusaka pointi 3 anasaka pia kupunguza goal difference ambazo kwa sasa nadhani tumewaacha goli 6 tukiwa na advantage.

Ngoja tuone mechi bado zipo.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…