Liverpool kumsajili Carvalho

Liverpool wapo mbioni kumsajili Fabio Carvalho kutoka Fulham.
Makubaliano yamefikiwa na Liverpool wamekubali kutoa Euro Milioni 5 kama ada ya uhamisho na Euro Milioni 2.7 kama ada ya nyongeza kuwapa Fulham. Dili hili lilikubaliwa mwezi Januari lakini likayeyuka muda mfupi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Fulham pia wameweka kipengele ikiwa Carvalho atauzwa kwenda timu nyingine na Liverpool wapewe 20% ya mauzo hayo.
Mkataba utakua hadi mwaka 2027 (miaka mitano) na mshahara tayari makubaliano yameshafanyika kati ya pande mbili.
Hakuna mipango ya kumrudisha Fabio Carvalho kwa mkopo kuchezea Fulham, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool msimu ujao.
Vipimo vya kitabibu tayari vimeshafanyika huko Liverpool kwa ruhusa ya Fulham na Jurgen Klopp tayari ameshafanya mazungumzo na mchezaji.
Taarifa kamili ya usajili huu haitatolewa sasa au wiki chache zijazo lakini itatolewa haraka mwishoni mwa msimu huu kuwaheshimu Fulham na mashabiki wao.
[Fabrizio Romano]
NB: Fabio Carvalho msimu huu amecheza michezo 30, amefunga magoli 8 na pasi za magoli 7. Ana umri wa miaka 19. Ni kiungo mshambuliaji wa katikati.
Mnauonaje usajili huu, Wekundu?