Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Game imeshaisha mbona..!
Screenshot_20220402-134309.jpg
 
Baada ya kupoteza Consistency kwenye michezo kama 5 iliyopita naona Jota amerudi mchezoni.
Hope katika mechi zilizobakia msimu huu hatapoteza Consistency
 
Huyu Roy Hodgson umri huu bado tu anang'anga'nia Ukocha? Ningemshauri astaafu tu tena akacheze na Wajukuu
 
Sio game time tu, na hilo kwake sio shida! Ni hali ya hewa ndani ya familia pale PSG ndio inamkumbusha mapenzi mtu anayopewa akiwa liverpool. Juzi tu hapa hali ikuwa mbaya baada ya kutolewa na Madrid wakati huku kwetu we stand together no matter what!

Wrong timing sio kuhusu contact terminal na extension period, ni nyakati hizi ambapo sisi ni macontender wa makombe 3 huku tukiwa tumeshaweka kibindoni limoko. Inahitajika loyalty zaidi.

Ushauri na maoni yangu mimi kwa Mo; akubali hio offer ambayo FSG wamempa kwa mwaka mmoja, alafu akili yote na club nzima ifocus kwenye kuyanyakua haya makombe. Then arudi mezani mwaka ujao kudai vitita vyake vipya wakikataa ang'oe. Hapo hata mimi nitaona kweli hawa FSG ni wa*#@$*&#@!

Huyu agent wake hana akili kabisa, anashindana na Klopp ambae amechangia kwa asilimia kubwa kiwango cha Salah kufika hapa!

Mfano Haller alisajiliwa West Ham kwa 45m Sterling akafunga goli 10 tu in 48 games, wakoana ni hasara wamuuza kwa Ajax kwa 18m Sterling na in 43 games ana goli 31, na maajabu aliyofanya huko UCl achilia mbali kutwaa mataji makubwa huko uholanzi.

Mchezaji anaweza kuwa na potential nzuri lakini asiwike kutokana na mfumo na namna anavyotumika na kocha wake, msisahau hichi kitu! Alikuwa Chelsea akaonekana garasha leo kwetu ni lulu.

Kitendo cha kumuonyesha dharau Klopp ni kitu mbaya sana, huyu agent atafurahia shoo ....
We jamaa story nyingi afu za uongo uongo klabu gani ulaya inatoa mkataba wa mwaka mmoja. Salah ajazaliwa Liverpool yupo kazini na kimsingi thamani anayo hivyo ni haki yake kudai. Mpira ni ajira ya kipindi kifupi sana asipo dai sasa hivi unataka adai lini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom