Pep anauwezo wa kumuweka bechi yeyote pale Kloop anawezaa?
Usiwafananishe hawa.
Kwa nini Eliot kageuzwa kiungo na ni sahihi kumuweka benchi Keita acheze Eliot?
Sasa kwa anavyo ng'ara huyo Bowel atapangwa wapi au benchi?
Manga ML kwa hio ishu ni atawekwa wapi ama ishu ni akiwekwa basi analeta ushindi kwenye timu... Ina maana ni bora kuongeza mkataba kwa Origi kuliko kusajili Bowen.
Wachezaji wote aliowasajili Klopp walikuta kuna wachezaji waliokua wanamiliki zile namba lakini walipambana na hatimae nao kuzimiliki na sasa nao wajipange maana kuna revolution tayari ishaanza ya kununua hawa makinda kwa ajili ya ku replace akina Mane, Salah, Henderson nk....
* Robertson alimkuta Moreno dogo akapambana na hatimae kua chaguo la kwanza,
* Jota alimkuta Bobby sasa amepambana kiasi anastahili kua kikosi cha kwanza muda wote.
* Allison aliwakuta Karius na Mignolet na akapambama akamiliki namba.
Ni kweli Klopp sio brutal kama alivyo Pep lakini hata yeye mazingira yanamlazimu kubadilika sasa hatuwezi kua wasidikizaji wa kipara kwa kuwang'ang'ania akina Salah wacheze dakika 90+ lazima tulete benchi la kuleta ushindani...
Maswali yamekua mengi sana ki vipi hizi sare zimekua kila msimu zinatu cost ubingwa huku Pep akichekelea. Jawabu na benchi kua dhaifu.
Tsimikas amemfanya Robertson kua bora.
Gomez amemfanya Matip kua bora.
Bowen, Fabio Carvalho na Bissouma waje kuongeza nguvu Juni 2022.
Top performers wetu ukimtoa TAA na Fabinho wapo over 29yrs hivyo kama hutaki yatukute ya Manchester United au Arsenal ni mapema kua na continuation plan.
YNWA