Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Adjustments.jpg
 
Ni raia wa Ubelgiji kwa kuzaliwa na ni Mkenya kwa uraia wa wazazi wake.

Anaongea lugha 3 safi kabisa Kiswahili, Kingereza na Flemish.

Ndio Mbelgiji wa pili kufunga katika fainali ya Champions League, wa kwanza akiwa Yannick Carrasco na timu ya El Choro.

Ndio mchezaji wa Kwanza with Kenyan origin kufunga kombe la Dunia.

YNWA
Kumbe anajua hadi kiswahili!
Amazing



Tuendelee na nondo mkuu
 
Kilichonifanya niipende Cameroon nakumbuka ni kuangalia Movie tu kibanda umiza enzi hizo Nipo Zanzibar Kuna Mtaa unaitwa Chumbuni Mtaa mzima ilikuwa hakuna mwenye Video Tape player (Deki) hivyo tunaenda kwa Mzee mmoja maarufu anaitwa NDEVU kuangalia Movie za Kivita enzi za Komando Vipensi na War Bus 😂😂😂

Basi kabla ya Movie huwa tunawekewa Trailer za Mziki wa Rumba basi around mwaka 1996 au 1997 mzee NDEVU wiki nzima alikuwa akituwekea Trailer ya Pepe Kale ya Roger Miller 🎶🎶
Makanaki Makanaki 🎶🎶
Mpaka nikajikuta naipenda Cameroon.

Mshua alisoma Newscastle Upon Tyne University hivyo alikuwa Mshabiki wa NewCastle kindakindaki nikamfuata kuipenda NewCastle ya Kaven Keegan kama miaka miwili hivi si nikaja kumuona Rigobert Song yupo LIVERPOOL wakati mimi naipenda Cameroon! Nikamwambia Mshua baki na Nucasto yako mimi simo nahamia Merseyside 😂😂😂
Newcastle ile ilikua fire sana miake ile 1992 mpaka 1997 na baadae 2008.

Turudi kwa jamaa zetu Cameron haha yaani ule wimbo ki ufupi ulichangia sana Cameron kujizolea mashabiki wengi sana maana kwanza ni moja ya tunzi bora kabisa kutoka kwa Pepe Kale na pia video yake akiwahushisha wale mastaa ilikua fire sanaaa.. Pale anapotaja Rodger Miller basi huku tunaitikia utadhani tunajua kikongo haha...

Indomitable Lions walikua neutral favourites kwa hapa Africa. Ilikua aidha upo Nigeria ama Cameron maana ndio walikua miamba miaka hiyo. Baadae wakaja Ivory Coast na Senegal.

Vibada Umiza mbona vimetutoa mbali kwani ndio mahala pekee angalau enzi hizo burudani zilipatikana tena kupitia VHF hahaha. Angalau sasa zipo njia nyingi baada ya internet popote ulipo burudani ipo kigajani..

Duuh kwa hio ndugu yangu urojo umeutadika haswa na alkasusi 🤠🤠🤠..

Upande wa Movi hahaha War Bus, POW the escape, Rambo, Terminator, Enter The Dragon, James Bond 007, Indian Jones.

Kweli kitambo was damn cool. No Dstv, No smart phone haha no problem. Ubea wa majuu chap kwa magazeti yaaani.

Fast forward baadae sana ITV wakaja rusha UCl ilikua lazima tusogee kwa TV kumskiliza Dr Leakey akitema madini mazito enzi hizo.

YNWA
 
Kumbe anajua hadi kiswahili!
Amazing



Tuendelee na nondo mkuu
Leo Tupo Na Samba nambari 1 the bearded GK of Liverpool.

Allison Becker.

Born Allison Ramses Becker in 2/10/1992 in State of Rio Grande Do Sul Jiji la Novo Hamburgo Brazil.

Wazazi wake ni Baba Jose Agostinho Becker na Mamake ni Magali Lini De Souza Becker na asili yao ni Ujeremani.

Ana kakake aitwae Muriel Gustavo Becker.

Alilelewa maisha ya kati na babake alikua dalali wa nyumba.

Baba yao aliona mahala sahihi pa vijana wake kupata elimu safi kabisa ya kadada ni Academy ya Internacional. Allison akiwa na miaka 10 alijiunga nao mwaka 2002. Mwaka 2013 alipandishwa rasmi timu ya kwanza Internacional. Alicheza mechi yake ya kwanza 17/2/13.Alicheza mechi 115 pale Internacional.

Mwaka 2015 kipa mkongwe kutoka Brazil alishindwa kuinyakua nafasi ya Allison pale Internacional mpaka kumpelekea Dida kustaafu. Kitendo hiki kilivuta ma Scout wa Ulaya sana kuanza kumfuatilia na hatimae Roma wakafanikiwa kumshawishi ajiunge nao July 2016 kwa dau la Euro 7.5m. Hakua chaguo la kwanza Roma kwani alimkuta kipa Szczesny akiwa chaguo la kwanza lakini dogo alipambana mpaka msimu uliofuata akawa chaguo la kwanza huku Szczesny akitimkia Juventus.

Baada ya kua na msimu safii kabisa pale Roma akipata clean sheet 17 Serie A na UCl clean sheet 5 na baada ya Karius kutuvuruga sana fainali ya Uefa vs Real Madrid ilikua ni dhahiri Liverpool kupata kipa mwingine. Hivyo mnano tarehe 19/7/21 Liverpool walimsajili Allison Becker kwa dau la £66.8m ikiwa ni rekodi mpya wa kipa ghali sana duniani kwa wakati ule. Rekodi ile ilidumu kwa wiki nne tu na Chelsea wakamnunua Kepa Arrizabalaga kwa £71.6m ikiwa ni rekodi mpya ya dunia mpaka sasa kwa kipa.

Alitua Liverpool akiwa na miaka 25 na kupewa jezi namba 13 kwa msimu wa kwanza.

Msimu wa pili alipewa jezi nambari 1.

KEY POINTS FOR ALLISON.
* NI devoted Christian.

* knock out stage za UCl vs Napoli alituokoa wengi mnakumbuka hii gemu jamaa walitushbulia sana dakika za mwishoni lakini Allison alikomaa mpaka mwisho tukatoka salama.

* Mechi ya pili dhidi ya Barcelona pale Anfield alituokoa tena na Liverpool kushinda 4 0 kwa kumtoa Barcelona nje ya mashindano ya UCl.

* Fainali Champions League pale Wanda Metropolitano dhidi ya Tottenham alisimama vyema sana kutusaidia kushinda taji la 6 la UCL kwa kuwapiga Tottenham goli 2 kwa bila.

* Msimu wake wa kwanza alipata clean sheets 21 na kumpelekea kushinda tuzo ya kipa bora EPL.

* Tangu ametua Liverpool ameshinda
--Champions League 2018 2019 season
--Club World Cup 2018 2019 season
--EPL trophy 2019 2020.

* Alishinda pia Copa America 2019.

* Alishinda kipa bora wa Dunia mwaka 2019.

* alishinda kipa bora wa Uefa msimu wa 2017/2018.

* alishinda tuzo ya Yasin trophy mwaka 2019.

* goli yake dhidi ya West Bromwich ndio ilikua goli bora ya msimu wa 2020 2021.

*Alisson ndio kipa pekee katika historia ya Liverpool ya miaka 130 kufunga goli kwenye competitive game akifanya hivyo dhidi ya West Bromwich Albion na kusaidia Liverpool kushinda mechi ile kwa goli 2 kwa 1 na kutuweka nafasi salama kumaliza top 4 last season 2020 2021.

*Alisevu penati yake ya kwanza dhidi ya Chelsea (Jorginho) 20/9/20. Alisaidia Liverpool kushinda mechi hio kwa goli 2 bila.

* Allison key areas alipo bora ni kwenye speed with both his hands and legs, crucial saves, timely tackles, blocks akitumia mwili wake wote kwa vile sio muoga. Ana distribute mpira kwa miguu ama mikono kwa kiwanga cha juu sana. Anajua ku ji position. Works really hard na ni team player.

* his idols ni Victor Valdes of Barcelona na Maneul Neuer wa Bayern Munich.

* ameshacheza gemu 149 hapa Liverpool.

* mkataba wake Liverpool unaisha 30/6/2027 huku akilipwa around £150,000 kwa wiki.

* Mwaka 2015 alimuoa mpenzi wake wa siku nyingi Natalia Loewe daktari kutoka Brazil. Wamejaaliwa watoto watatu. Mtoto wa kwanza wa kike jina Helena akizaliwa April 2017 na wa pili mtoto wa kiume Matteo akizaliwa 4/6/2019. Na mwaka huu 11/5/21 wakapata mtoto wao watatu wa kiume.

* Kakake Muriel Becker ni kipa akichezea timu ya Fluminesse Brazil.

* Nick name for Alisson
..... Ally
.... The German(wazazi wake wana asili ya Ujeremani.
..... Messi of goal keepers.

* anapenda pia kuedesha baiskeli na ni mpiga guitar safi kabisaaaa.

* anapendelea kuedesha magari ya kifahari aina ya Audi Q7, Range Rover na Mercedes Benz.

YNWA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom