"WANA OLE GUNNER, TUNA HASHIM RUNGWE SPUNDA"
Kuna zama za kimaisha lazima binadamu akubali ukweli kuwa uwezo umefika kikomo..
Haijalishi bado unaipenda kazi unayoifanya au matamanio ya kufikia malengo flani...Ukomo wa uwezo ukifika mwisho ni lazima kutupa taulo na kukaa mbali.
Ishawahi kutokea kwa Mike Iron Tyson, Muhammad Ally, Kobe Bryant, Ronaldinho Gaucho, John Cena na mastaa wengine kibao.
Hali ni tofauto kwa mwanasiasa wa Tanzania mtaalamu Hashim Rungwe na Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer kwani wote wawili bado wanaamini wana uwezo wa kutimiza malengo yao na mafanikio ya taasisi zao ilihali uwezo wao ukiwataka kutupa taulo.
Hashimu Rungwe kuna nyakati aliamini sera ya kutoa ubwabwa inaweza kumpeleka Ikulu ila Ole Gunner anaamini kuwa kupewa muda kunaweza kumfanya kuwa kocha wa mafanikio wa Manchester United na kuondoa ubabe wa Manchester City, Liverpool na Chelsea.
Hawa ni binadamu wanaovuta hewa moja ya oxygen kwenye majiji tofauti lakini akili zao zikiwa zimefanana..
Ole Gunner akiwa Jiji la Manchester United anawaza kama mtoto mdogo kwa kitu ambacho hakiwezekani kwani uwezo wake umefika mwisho na pia uwezo wake ni mdogo sana kulinganisha na makocha wakubwa waliopo ligi ya Epl.
Ukiondoa makocha wakubwa wa Epl swali la kujiuliza Je Ole Gunner anasogelea hata nusu ya uwezo wa Claudio Ranieri?Brandan Rogers? Antonio Conte? na wengineo wachache waliopo Epl ambao ni makocha wa timu za kiwango cha kati?.
Naamini na nitaendelea kuamini kuwa Manchester United ina matatizo mengi sana lakini tatizo kubwa la kuanza nalo ni kumuondoa Ole kwenye kiti cha Old Trafford.
Chauma haiwezi kuchukua nchi ndivyo ilivyo kwa Ole hawezi kufanya lolote ndani ya Manchester United.
Anyway Tanzania tuna Hashim Rungwe wetu na Manchester United wana Ole Gunner Solskjaer wao.
KEY THE DON