Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Tunacheza CL next season Kaka! Nafasi ya kwanza mpaka ya Tatu hizo zimeshapata wenyewe, Nafasi ya 4 ni Vita kati yetu na Leicester City! Hivyo ni kuhakikisha hatupotezi mchezo hata mmoja kati ya Minne iliyobakia basi tutacheza UCL next season.
Aisee una roho ya paka [emoji23][emoji23][emoji23]


itakuwa maajabu makubwa sana Liverpool kucheza CL msimu huu ..

Kiufupi haiwezekani ,mmeshachelewa tayari ...

Yaan mmtoe westham ,lecister city kirahisi tu
 
Usajili, Usajili, Usajili ndiyo mafanikio ya Timu.

Imagine Tuchel angelikuwa na Chelsea ile ya kina Tomori, Barkley, Abrahamu na Willian je kuna maajabu yoyote angeweza kufanya?

Lakini angalia sasa Chelsea ilivyoimarika unadhani ni kwa Ufundi tu wa Tuchel? Pongezi nyingi ziende kwa Lampard kwa Wachezaji aliowasijili ambao alishindwa kuwamanage hatimae Tuchel anafaidika nao.

Usajili ni Nguzo muhimu ya mafanikio kwa Watu wenye akili ya Mpira kwani akili zipo nyingi Mfano Albert Einstein alikuwa na akili ya Darasani but hakuwa na akili ya Mpira, lakini Messi hana akili hata ya Darasa la 7 but ni Genius kwenye Mpira.

Same to Liverpool Michael Edwards ni Genius kwenye Negotiations za Kibiashara lakini kwenye Mpira ni Sifuri hamna kitu kabisa that's why anatuletea Vitoto vya £2M na kuanza kumsifia ni Genius huku Top Red wakiwabrainwash Washabiki Maandazi kuwa Timu iliyotupa CL isiguswe kwani Duniani hakuna Mchezaji anayeweza pata namba mbele ya Wachezaji hao.

Sasa ona kinachotufika.
 
Aisee una roho ya paka [emoji23][emoji23][emoji23]


itakuwa maajabu makubwa sana Liverpool kucheza CL msimu huu ..

Kiufupi haiwezekani ,mmeshachelewa tayari ...

Yaan mmtoe westham ,lecister city kirahisi tu

Hakuna CL ya Westham dunia hii.
Hapo tunayepambana naye ni Leicester tu.

West anapambana Europa Qualification rounds na Spurs kwani kuingia Europa moja kwa moja tumeshaingia sisi lakini hatutaki hiyo nafasi ya Europa tunataka CL.

Inaonesha hujaangalia Msimamo hebu nenda kwenye Table ukaangalie Msimamo.
 
Tuende pole pole

Next match upo na man utd ,matokeo yake nadhan unajua ...

Lecister kakuzid point 6 ,unatakiwa kushinda match 3 ,yeye apoteze match 3 ...


Liverpool ya sasa kushinda match 3 na team ambazo zinapigania kushuka daraja ,majibu unajua ..

Table
 
Mkuu dong yi kwanza hili la kuodoka Klopp sahau yaani hawa FSG hawana mpango wa kumwodoa labda atake mwenyewe.

Ipo hivi chini ya uongozi wa Klopp Liverpool imeongezeka valua yake kwa asilimia 165.


Tazama mwenyewe hapo juu. Liverpool kwa sasa ina value ya usd 4.1 billions. Sasa ndugu hawa mabeberu unadhani kwa kupanda kwa value ya Klopp watamwodoa Klopp hivi hivi.


Mark you Manchester United ina value ya dollar 4.2 billions pamoja na kutawala soka la Uingereza ndani ya miaka 30.

Tazama Klopp effect inainyanyua timu kibiashara. Yaaani huyu tunae. Wewe unadhani angekua kocha Rodgers haya yangewezekana wapi.

Cha msingi ni wenye timu waelewe tu kwamba kushindana na timu bora kunihitaji Klopp awezeshwe sokoni. Kushiriki UCL na kushinda ndio kunaleta haya yote. Kushiriki EPL na kushinda ndio kunaleta haya yote. Kwa kifupi mafanikio uwanjani yanaleta mafanikio kibiashara yanavuta Makampuni makubwa kuwekeza nk.

YNWA
 
Unataka Klopp akiondoka aje kocha gani???
 
Kumbe kuna muda akili huwa zinakurudi.
 

Na ndiyomana nikamwambia huangalii Msimamo na inawezekana hata Ratiba pia huangalii.

Liverpool kacheza michezo 34 kabakisha 4
Leicester kacheza michezo 35 kabakisha 3

Leicester game ijayo anacheza na Manchester United una uhakika kuwa Leicester atashinda?
 
Wewe Hesabu ulijifunzia wapi?? Maana mmmm..
 
Wewe Hesabu ulijifunzia wapi?? Maana mmmm..
Achen kukaza ubongo Hamaa uwezo wa kuingia top four ,...


Mnadhan hicho kipolo mmeshachukua point 3???

Hesabu gan wewe wasema ??


Weka hiyo hesabu ya Liverpool kuingia top four
 
Point si hizo hapo 6 ,au mnaangalia nini..

Hicho kipolo mnahesabu ni point 3 ????


Kudadeeeek nyie mmeshavurugwa
 
ushawahama 'halisi' mkuu?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


sisi liverpool artificial tupo pembeni tunawatazama!
 
sipingani kabisa na usemacho mkuu, ila hoja yangu ni kwamba Klop nae ni sehemu ya matatizo yetu....!


huyu hata akiwezeshwa sokoni ile tabia yake ya kukariri wachezaji na formation itaendelea kutugharimu sana....... anao wachezaji wengi hata sasa pale anfield lkn kukariri kwake na ule ukaidi wake na kutaka kuwa-prove watu wrong kutaendelea kutu-cost
 
Mkuu hilo lipo wazi Klopp ni tatizo na Klopp ni jibu hivyo ebu tuwe na subira apate kikosi chake kamili.

Kama unakumbuka vyema Klopp na wachezaji wake wa kuungaunga akina Robertson nk amechukua vikombe heavy duty hivyo tumpe benefit of doubt kwamba haya ya msimu huu yamempa fundisho tosha kuhusu EPL haina mwenyewe aisee.

Hili la mfumo 4 3 3 ishu sana lakini kwa vile sijawai mazoezini ni ngumu kuelewa kwanini ana trust issues especially na hawa new comers. Sielewi kwa nini mfumo haupangwi kwa kufuata wachezaji walio wazima.

Mambo ni mengi ya kutazama. Tusubiri kikosi chake msimu ujao tuone mambo niaje. Kwa msimu huu binafsi nishasema null and void regardless tutamaliza nafasi ya ngapi.

YNWA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…