Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Duuh kweli tulikotoka panatisha mno wachezaji enzi kuja team ya nafasi ya 7 mpaka 10 ilikua ishu sana kuwavuta wengi walitugomea kwa vile hatukua na UCL lakini leo hii mpaka wachezaji kama Mbappe tunatajwa kuwataka kweli maisha yanakwenda kasi 5G...

Enzi hizo wachezaji wetu ni Downing, Charie Adams, Jerry Spearing, Insua, Peter Crouch nk bado tulitulia tulii tukijua kuna siku tutakaa sawa na kweli baada ya kutua Klopp tupo sawa na huu wa sasa ni upepo utapita tu...

Hakika kumfananisha Steve Gerrard na Hendo ni kama kufananisha usiku na mchana...

Hendo ana bahati amezungukwa na wachezaji wenye talanta bora kabisa zaidi yake na anacheza chini ya kocha bora kabisaaaa... Hii bahati Steve hakuipata.

YNWA
 
Mim binafsi naamin title contenders mpaka sasa ni

Liverpool na man city

Full stop

Swala la utd kubeba EPL ,akili inakataa kabisa ,

Unazungumzia Liverpool hiihii inayofunga goli moja la kuvizia kwenye mechi 5 au kuna nyengine?

Title race ni Man City v/s Man United ndugu.

Liverpool kwasasa anachoweza ni kugombea Top Four tu manake muda wowote anaweza kutupwa nje.
 
mirror na daily mail ni wazee wa kuchochea moto.
Ile sinema ya CEO michael zorc vs klopp ilimalizika kwa talaka
sijui hii ya FSG itakuwaje.
============

Some frank home truths from Klopp who says:
He strongly recommended signing centreback. Was told no money by Liverpool owners. They will not change stance on signings despite poor form. He won't 'cry like a baby' because he doesn’t get what he wants.
 
Washabiki wenzangu hivi munajua kuwa Mathematically sisi tupo nafasi ya 6?

Sasa subiri Everton ashinde kiporo kimoja tu kati ya Viporo vyake Viwili.
Na Spurs ashinde kiporo chake kimoja.

Sasa katika hizo Timu 6, mbili kati yao Man City na United lazima zimalize wa kwanza na wapili, nafasi za kugombea Top Four zimebakia mbili tu Yani 3 na 4.

Sasa kwenye nafasi hizi za 3 na 4 wafuatao ndiyo wanazitaka:-

Leicester
Everton
Spurs
Liverpool
Chelsea
Arsenal

Timu 6 hizo wanazitolea macho nafasi ya 3 na 4 unadhani hapo tutamshusha nani?

Kazi tunayo.
 

Huyu Klopp atashindwana nao hawa FSG, jamaa wana very strong Financial Policy ambayo hawako tayari kuivunja kwa reason yoyote ile.

Sera yao Sell tu Buy kamwe hawapo tayari kuivunja.

Kwasasa watalazimika kumuuza Star mmoja ili wapate pesa nyingi wasajili, na kila nikiangalia mchezaji ambaye ni Superstar kwa Timu yetu tunayeweza kupata pesa za usajili ni Salah, Hivyo njia pekee kwasasa auzwe Salah ili tupate pesa za usajili.
Pia kina Origi, Xhaqiri, Grujic, Wilson, OX, Keita, Matip nao wauzwe kuongezea hela za usajili.

Vinginevyo basi imekula kwetu kwani Klopp hata atoe mapendekezo gani ya usajili hatosikilizwa.
 
Aseno, chelsea na everton watoe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani Wataalamu sijui mutapata maana gani kwenye haya maneno ya Klopp lakini mimi mwenzenu maana ya moja kwa moja niliyoipata hapa ni kwamba Klopp kakataliwa na FSG kumsajili CB.

Hawa jamaa wanasimamia sera zao fedha bila ya kuyumba hata kama Timu ipo kwenye hali mbaya kiasi gani.
 
umeongea ushabiki tu apo
 
Mashabiki wa Man u tuna balaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mim binafsi naamin title contenders mpaka sasa ni

Liverpool na man city

Full stop

Swala la utd kubeba EPL ,akili inakataa kabisa ,
Liverpool hii hii inayo struggle kuwafunga Fulham, West Bromwich, Newcastle, Southampton, Burnley, Brighton bado unaiweka kwenye Title Race Mkuu ,Timu inayochezesha Midfield CB Liverpool hata Top 4 kuipata itakuwa mbinde.

AU NASEMA UONGO NDUGU ZANGU.
 
Pamoja na yote ,ukiangalia vizur kwa jicho la tatu ,Liverpool bado wanacheza kibingwa ,ukilinganisha na mbinu za kocha mzoefu klop

Harafu ile table ilivo sio ya kujivunia et uko top ,never

Liverpool wanakosa kitu kidogo tu finishing ,kuhusu kutengeneza nafasi bado wapo vizur .

Timu bado ina sprit ya ubingwa ,team yeyote kuna muda mpira unawakataa kabisa ,then wanarudi kwenye form
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…