Kwasasa ushindi wa Liverpool FC ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) umekuwa ni jambo la kawaida kama mke kulala na mumewe ama mume kulala na mkewe, sleeping with your spouse is not an option, ni lazima!
Kwasasa Liverpool FC imekuwa tamu kuliko hata 'Screaming Eagle Cabernet 1992' mvinyo ghali duniani (the most expensive wine in the world) unaouzwa kwa $ 500,000/- [ TZS 1.15 billion] kwa chupa moja tu! Liverpool FC ipo kileleni mwa mafanikio, imetwaa Ubingwa wa Dunia ngazi ya vilabu, imetwaa Ubingwa wa Ulaya ngazi ya Vilabu na imetwaa UEFA Super Cup, kwasasa Liverpool ndiyo timu bora Uingereza, Ulaya na duniani kwa ujumla katika ulimwengu wa soka.
Kwasasa Liverpool FC inacheza inavyotaka na inataka inavyocheza, inaamua ishinde kipindi cha kwanza ama cha pili, Mohammed Salah amerejesha makali yake, anafunga kila anapoamua, anavunja rekodi za akina Fernando Torres (El-Nino) na mtukutu Luis Suarez yule mjukuu wa Jose Mujica Pereira, Rais mnyenyekevu kuliko wote duniani!
Katika mechi 13 zilizobaki sasa Liverpool FC ni wazi ikishinda mechi 6 tu inakuwa Bingwa mpya wa EPL 2019/2020, hii inategemea kadri ya wapinzani wa Liverpool FC nao watakavyoshinda (zinaweza zikapungu zaidi au zikaongezaka) mambo yakienda sawia kama inavyotarajia. Kama Manchester City na Leicester City zitaenda na mwendo huu (wa kufungwa fungwa) ni wazi Liverpool itakuwa bingwa kwenye mechi dhidi ya Crystal Palace mechi itakayopigwa Anfield mnamo. Ikiwa inaenda kucheza na Manchester City tayari Liverpool FC itakuwa ishakuwa Bingwa!
Kinachonifurahisha na kuvutia zaidi ni pale Liverpool FC itakapokua inatoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (Dressing Rooms) pale uwanja wa Etihad, wachezaji wa Manchester City watakaa mistari miwili na wachezaji wa Liverpool FC watapita katikati yao huku wakipigiwa makofi na wachezaji wa Manchester City (Guard of Honor) kwa pongezi za kunyakua taji hilo ambao kwa miaka 30 Liverpool FC wamelikosa.
Kwasasa kutazama Liverpool wanavyocheza ni raha kama kuwatazama Shakira na J-Lo wakitumbuza kwenye jukwaa moja, utamu wa soka la Liverpool FC kwasasa ni sawa na kwenda kujivinjari katika kisiwa cha Mbudya na Miss World kutoka Latin Amerika! Kwasasa Liverpool ni Baba-Lao kwenye soka!
Kuna kijana anaitwa Roberto 'Bobby' Firmino Barbosa, anacheza kandanda safi kama mnenguaji katika sherehe ya kumtoa Mwalimu wa kimakonde, yeye huamua mechi ngumu matokeo yaweje, mechi ya S'ton aliifanya kuwa mechi rahisi bila uwepo wa Sadio Mane', anapora mipira katika eneo la hatari halafu anatoa pasi ya mwisho yanayozaa mabao matamu kama pilau lilopikwa na mama mkwe!
Jambo bays zaidi linalowaudhi akina Ferguson na wenzake ni kitendo cha Jurgen Klopp kuifanya EPL kuwa Ligi rahisi, hata Fergie katika zama zake hakuwahi kuongoza Ligi kwa tofauti ya alama 22, huyo ndiyo JK Mjerumani mbishi anayeamini kwenye soka akili siyo nguvu kama Jose Mourinho.
Kwasasa kila rekodi zimeshavunjwa na Liverpool FC na kuandika rekodi mpya, kinachosubiriwa ni kuivunja rekodi ya Arsenal FC ya kubeba Ubingwa bila kupoteza hata mechi moja, hili la Ubingwa wa EPL ni 100% unaenda Anfield kwa msimu huu! Naweza kuandika katarasi zenye urefu wa Dar-Songea kwenda na kurudi kuhusu Liverpool na nisimalize, kila siku zinavyokwenda Liverpool inazidi kuwa tamu kama nanasi!
Kwasasa kuiandika Liverpool FC ni sawa na kuwa mbele ya mwanamke mrembo kama Monalisa/Cleopatra ambaye ukiwa mbele yake huwezi kosa kumsifia kwa uzuri ulivyomwenea, ngoja niendelee kunywa Dodoma wine huku nikitafuta hela ya kununua Screaming Eagle Cabernet 1992 nikikosa nitakunywa Château hata nusu 'glass' kwa $ 20,000/-, Life is too short, let's enjoy when we're breathing!
Hivi ukiachana na ngono, mpira na kunywa wine kitu gani kitamu zaidi? Nawaona watu wanavyoguna kwenye ngono kana kwamba hawafanyi, nakuhakikishia hata kiongozi wako wa dini/kisiasa anafanya wala usione ajabu! Hey, Red's make as great, We Are Liverpool, This Means More!
#YNWA #EPL2020
Sent using
Jamii Forums mobile app