Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Umetumia vigezo gani mpaka kusema usingependa alison apangwe kwa sababu ya kukaa nje miezi miwili?
 

Kwani Rashford na Lingard wana nini kikubwa Walichomzidi Lukaku? Mbona Kaondoshwa Lukakua wakati Rashford na Lingard wanapeta Man United?
Hoja nyengine bhana!
 

Kwasababu Tokea walipoondoka ALONSO, GERRARD na MASCERANO Liverpool haijawahi kusajili Midfield ya Maana yenye kieleweka ndiyomana Henderson na Ubovu wake bado anaendelea kupeta.

Na sioni Dalili ya Klopp kusajili Midfield kwahiyo Hendo ataendelea kutesa misimu mengine 5 mbeleni.

Mido zilizotegemewa ambazo zingempoteza Hendo ni KEITA na OX lakini ndiyo injuries zimewapoteza na wao.

Kama sio injuries basi Mido ingekuwa

KEITA - FABINHO - OX na huyo Henderson angelikwisha rudi Sunderland na Ucaptain wake.

Kwahiyo sio kwamba Makocha wanampenda kwasababu ana kitu cha ziada cha kuoffer! Bali anacheza kwasababu Liverpool hatuna mwengine tu wa kucheza na kikosi chetu cha wachezaji 12.

Tunhekuwa na watu kama MASCERANO-ALONSO-GERRARD huyo Hendo hata kuokota mipira asingeliokota.
 
Acha kuponda man, Jini ni moja ya mido bora wa Liverpool, we ni aina ya watu unaeongea passionately kuliko ujuzi, bora Mosfed anajua anachoongea

Acha unafiki mimi sijawahi Kuzungumzia Jini katika post zangu
 
Wakati Roy Kean anasema hayo ,man u wanajiandaa kupeleka £70m kumng'oa hapo westham

Manchester United could spend upwards of £70m to sign West Ham United's England midfielder Declan Rice.

bbcfootball

Man United ni Kijiwe cha Watu kujipigia hela tu kama wajanja walivyojipigia kwa Maguire
 
The Henderson guy is very poor. He is a disgrace to my Liverpool. A number 8 that is non productive. Bure kabisa. Whenever I see him in the line up I badly feel sick.

Stats za Henderson Ndani ya Msimu wa 2019/20 mpaka sasa:

8 EPL games
2 CL games
1 Ngao game
1 Super Cup game

Total 12 games

In 12 games mchezaji Attacking Midfielder ana 0 goal na 0 assist

Halafu anatokea Mtu from nowhere anakwambia ni Mchezaji Mzuri ana damu ya Kunguni tu.

Katika kikosi chetu cha FXI ukimtoa Kipa, Katika Wachezaji 10 waliobaki Mchezaji aliyekuwa hana hana Goli au Assist ni Hendo pekee.

Yani hata Mabeki wetu wote 4 (VVD, MATIP, ROBBO na TAA) basi kila mmoja aidha atakuwa na Goli au Assist kwa msimu huu lakini Kiungo Mshambuliaji wetu Henderson hana! Sasa uzuri wake Tumpime/Tumtathmini kwa kitu gani?
 

Si busara kulinganisha watu wawili wanaocheza aina tofaut za mpira
Pili wote naona ni walewale tu

Tatu, watanzania wengi wanaendeshwa na passionate na sio akili, hii humfanya mtu aamini mtu anaeona anaifurahisha moyo wake, ndo maana kuna makundi na kila kundi lina mtu aliesifiwa sana na wanakundi hilo, huwez mtoa muhuni sugu anaependwa na wahuni kutokana na kuwazidi uhuni wenzake katika kundi la wanadini na asifiwe vilevile kwa wanadini, na hivyohvyo viceversa

Ko haimaanishi mtu anachoongea yuko sahihi au lah, ila katika kundi hili ukigundua mtu kakushinda mapenzi na timu utamuamini sana maanda ndo jinsi binadam walivyokuwa programmed,
Najua anauchungu na timu ila hiyo haimaanishi anachokiongea ni sahihi
 
Kwa hiyo wewe Henderson unamuona bonge la mchezaji
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…