Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Henderson sijui anafanya nini liva

Hivi kwa nini hatusajili kama hawana pesa wanambie niwakope

Mad !
 
Mimi kinachofanya nikuquote ni kuwa inaonekana wazi kuwa tokea Dalah ahamie Liverpool nlanaibeba Liverpool kwa kila halo hasa inapokuwa katika Mazingira Magumu lakini still unamponda kama kwamba hana msaada wowote.
Sijawahi kuwa na ushabiki wa hivyo ni mara nyingi tu akifanya vizur Nampa pongez zake mm ni shabiki na mpenzi wa mpira mzuri...siwezi kuwa na kinyongo na mchezaji wa timu ninayoshangilia tokea nilipopata akili.nashangaa ewew unaetaka kusema No salah No Liverpool.kisa goli la Napoli halafu unasahau mtu unasahau uwezo wa hao wengine kwenye msimu uliopita.CHIEF ACHA MAPENZI BINAFSI. mchezaji anasifiwa na kukosolewa ndio mpira.
 
Keita ni misuse of resource pale liverpool, yaani unanunua viatu vya ngozi kwa bei gharama halafu badala ya kuwa cha mitoko we unakigeuza ndala (za kuogea) ilhali huna kiatu kingine. Kwa majukumu na position anayolazimishwa acheze pale sitegemei makubwa kutoka kwa naby keita(wa rb leipzig) Huyu tutaanza kumwita JORDAN KEITA
kabisa sasa kazi kwake ajilinde na majeraha ya mara kwa mara...
 
Aguero hayupo level moja na Mo Salah kwenye umaliziaji kadhalika Harry Kane au Hazard

Salah anajua kufinish pale EPL

Hazard angekuwa finisher mzuri kuliko Mo Salah angefunga goli zaidi ya 20 kila msimu sababu yupo exposed sana na Chances kuliko Salah cha ajabu kacheza misimu yote hiyo hajawahi fikisha goli 20, hata 17 tu nina wasiwasi na tena ndio penalty taker wa Chelsea

Kane strength yake anapiga mashuti mazito sana, ila sio finisher kumfikia Mo Salah , Spurs finisher wao bora ni Eriksen

Aguero ni mpiga mashuti mzuri sio finisher mzuri, kwa city finishers ni DeBruyne na Bernado Silva halafu huyu Aguero anapooza sana move za kufunga kama mwenzie Kane

Salah anakufanyia finishing ya kuugongesha mpira kwenye post kuwa goli(ana shabaha sana kama anataka kufunga kwa kutambaza mpira)
 
Labda finisher kwenye soka sijajua maana yake, bernardo silva huyu awe finisher mzuri pale city???
Hivi kufinish si kutumbukiza kitu kambani?
Sasa bernardo awe finisher mzuri city? Labda ungesema ni hatari kwa ku create chance pale city ningekuelewa mkuu. Anyway nahitaji elimu yako mkuu @ MASAMILA
 
Ni mawazo yako na sio sheria na ulichokiandika ni unachokitaka ewew.huyo unaemuona anajua kufinish epl nzima sijui Kama alifikia hata uwezo wa Torres au Suarez lkn unaamua kuandika tu sababu hutaki kubaki nyuma.mm lfc damu lkn salah na aguero kwenye finishing ni vitu viwili tofauti....acha bla bla sijui za mashuti au kulenga goli
 
Keita is coming very good, his box to box qualities utaziona Tu
He came.on Jana and it was lively

I don't see Henderson and lallana giving us any joy very time soon

Naby, faby, ox, Gini ndio way to go
 
hahaha Mtu Fulani umesema vyema kabisa...hata hivyo ndogo lazima ajikinge na majeraha ya mara kwa mara...
 

Na ni kweli it's just opinion na bla bla

Aguero na midfield ile kashindwa fikisha goli 27 na tena yeye ndie mchukua penati
 
Keita is coming very good, his box to box qualities utaziona Tu
He came.on Jana and it was lively

I don't see Henderson and lallana giving us any joy very time soon

Naby, faby, ox, Gini ndio way to go
as long as hakuna majeraha Ox, Naby ni kazi kazi...

lets hope pia the gaffer atawapanga in thier respective positions wang'ae vipoa...
 
hahaha Mtu Fulani umesema vyema kabisa...hata hivyo ndogo lazima ajikinge na majeraha ya mara kwa mara...
Majeraha kwa left mid anakocheza atapata sana labda tuombe apazoee. Speaking from experience zile turn, dribble & tackles ndo zinamsababishia majeraha ya mara kwa mara kwani anakua limited space-wise kwani kule anapokuwa uwanja unakuwa finyu kwake kufanya turn ikizingatiwa kakua amezoea kuwa central kabisa sehemu yenye greater space kufanya udambwi
 

Finisher ni uwezo wa kufunga katika chances kubwa (timing & accuracy na skill/ufundi wa kumalizia ili kufunga)

Messi ndio top kwenye sekta hii (opinion)
 
KIUKWELI SIJAWAHI KUMFATILIA HUYU KIPA MPYA TULIYESAJILI LAKINI KWELI SI NI BORA MIGNOLET ANA AFADHALI? AU NAMFANANISHA TU?

IVI NDIYO ANA MIAKA 32?

NAHISI HATA KARIUS NI DE GEA MBELE YA HUYU KIPA MPYA
 
cant say otherwise...zile turn ndio kabisaaa hata kule Misri ndio zilimcost yale majeraha...

the boy likes to dribble he just have to know hii ni EPL muda wowote anakwatuliwa..am positive after the 1st season he will be better...his instinct will be superb as he has 1st hand experience how to connect, turn,dribble etc..
 
Unavyosema harry na aguero ndio wachezaji PEKEE wanaokupa uhakika wa magoli kuanzia 20 Salah unamtoa kwa kigezo gani haswa wakati yeye amethibitisha kua bora katika kufunga.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…