Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

BREAKING NEWS.

Nasikia leo David Silva kaamka na tumbo la kuhara kwa hiyo hatacheza. Halafu Aguero kaamka na chongo kwa hiyo mnaweza kuanza kupumua. Hizi ndio habari njema kwenu. [emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
Droo ya Southampton imekuvuruga na muda sio mrefu Mtaa wa 6 utakuhusu
 
Uzuri wa Liverpool! Yani huwez kujua nan ataibuka man of the match. Team ipo decentralized mpaka raha, yani kila mtu star na kila mtu anaweza fanya maajabu wakat wowote.

Sio Salah, mane, sturrg, firmino, shaqir yan hata Lallana 😂😂anaweza ingia na kufanya maajabu . Tofauti na viteam vingine vinavyojiita big six yan ukishika tu harzard au Torori la Arsenal basi team imekufa tayari.

Am proudly to be Red
We are Liverpool
You Will Never Walk Alone.
 
Hapo umenena vyema sana Mkuu, ukweli hatuna RB mwingine zaidi ya TAA maana hata Clyne kwa ndogo anasubiri.....

Milly is mr many position ila si kwa RB vs City yaani penati kama zote....Klopp is smart to know better vs City we need fresh legs..

Hope Klopp atakwenda na TAA, Lovren, VVD na Robby kwenye back four...
 
Mkuu kuna kitu utakuwa ujaki-note. Robbo mara nyingi ndio amekuwa mzuri kwenye kuanzisha mashambulizi kuliko mchezaji yoyote kikosini kwa sasa. Kwa kasi yake na cross zake ni mzuri zaidi katika kufanya caunter attack,kuliko kuanzia kwa Fabby.

Kwa game ya leo ningependa kama Milner atakuwa fit aanze flank ya kulia TAA aanzie banch. Aingie kuanzia dk ya 70...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Milly kucheza RB leo vs City ni kujitafutia kipigo maana kwa pace ya Sterling or Sane atakimbiza upepo...

Aidha apangwe TAA or Clyne, Milly apangwe midfild tu.

Hapandi juu yaani acheze kama anavyocheza Azpilicueta
 

Hivi unaangalia game za Man City Mkuu?
Au kumbuka game za last season tulizokutana na Man City!

Mkuu si kwamba Milner hawezi kucheza vizuri RB! lakini tuangalie na aina ya opponent wetu
Ungelikuwa unajua jinsi Sane anapokuwa na mpira mguuni anavyokimbia basi ukimuekea Milner umemrahisishia kazi tu manake akishamtoka hatua moja basi kumkamata ni ndani ya nyavu.

Mkuu hahitaji Milner bali anahgitaji FB anayeweza kukimbia, lakini Milner kukimbia hawezi tena.

Kwa game ya leo RB ni TAA au Clyne ndiyo wanaoweza kublock pace ya Sane.
 

Na kuhusu Robbo kuanzisha Mashambulizi ninajua kuwa maranyingi huwa ni yeye ndiye anayeanzisha! Lakini leo Mkuu nimezungumzia special case ya game plan ya kutafuta draw! That is why nimemtaja Fabi kuanzisha Kaunta kwasababu yeye ndiye mtaalamu pekee wa kupiga mipira mirefu kwenye timu yetu.

Robo anapoanzisha Kaunta hajui kupiga mipira mirefu bali anakokota na kukimbia na mpira mwenyewe jambo ambalo huenda Man City wasiliruhusu.
 
Mkuu watu wengi wanataka Milner acheze RB hii itakuwa ni kucheza Gambling Watu wanaamini sana katika kujituma kwa Milner na Nguvu kazi yake wanasahau kujiuliza hiyo nafasi ya RB akicheza ataicheza kwa Uwezo na Ubora hili swala la kulazimisha mtu acheze Out of position lina madhara makubwa
 
L’Equipe’s team of the year for 2018 ni hii hapa haina Front 3 hata mmoja wa Liverpool FC lakini hili ni sawa kwa 100%

Palipo na Hazrad, Messi, Mbappe na Ronald basi hapana nafasi ya kumueka Salah, Mane na Firmino.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…