Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

How about this season?

Salah ile ilikuwa suprise package, ndio maana harry kane alimwambia KAMA MWANAUME AFANYE VILE TENA MSIMU HUU

Tuthibitishe kuwa ni world class player
Kwani msimu umeisha???? Huyo Harry Kane mwenyewe hua inafikia October kafunga sana goli sita ikija may ana 20+
Huko
BTW umemtaja degea kama world class hivi huyu degea wa msimu huu ndio degea wa last season?????
 
Kwani msimu umeisha???? Huyo Harry Kane mwenyewe hua inafikia October kafunga sana goli sita ikija may ana 20+
Huko
BTW umemtaja degea kama world class hivi huyu degea wa msimu huu ndio degea wa last season?????
Tatizo uelewa wako mdogo

Kane kila msimu ana 25+ goals, degea ana misimu karibu minne yupo bora

Salah ukitoa msimu uliopita, ni upi alishaini?

Ndio maana mpaka sasa amedrain,
 
Sina hakika Kama atakuelewa Leo!!!!
 
Leo humu mtapaona pachungu. Mjitahidi mshinde lkn km hamtashinda yaaani tutakuja kuwafyekelea mbali.

nguvu fyeka kabisa, MosDef fyekelea kule, Gwamahala fyeka fyeka na Mheshimiwa diwani Malafyale kaka yake everlenk fyekelea mbali kabisa


[emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiv unaamin salah ni world class player?

Mimi kwenye issue ya Salah siwezi Kukubishia Coz ninajua Kuwa Salah Ni inconsistency.

Lakini Wewe Kuamini Mawazo ya Bascombe Kuwa Ni De Gea pekee Kwa Makipa Wa EPL Kuwa Ni World Class basi ndiyo hatuelewani.

Kwani Alisson Becker naye Ni World Class amedumu Na Consistency akiwa na Timu ya Taifa, Akiwa na Roma, na Sasa Akiwa Liverpool still ameinesha Ubora Zaidi Kwa Kutuokoa Karibia Kila Mechi ambazo Tunaelekea Kupoteza.

So, Alisson Ni World Class na Ndiyomana Hata Real na Chelsea walimtaka lakini Akaichagua Liverpool.
 
Tatizo uelewa wako mdogo

Kane kila msimu ana 25+ goals, degea ana misimu karibu minne yupo bora

Salah ukitoa msimu uliopita, ni upi alishaini?

Ndio maana mpaka sasa amedrain,
Kwani Salah huu ni msimu wake wa ngapi akiwa na liverpool?? [emoji12]
 
Jamaa una kichwa kigumu kuelewa aisee. Hata mfano wa Arthur hujauelewa?

Angalia Hazard anaingia katika kikosi ambacho kimetoka kutwaa UEFA na makombe kadhaa ya EPL. Msimu wa 2012/2013 Hazard kawakuta
Cahill,
Ashel Cole,
Ivanovic,
John Terry,
Ferreira,
Frank Lampard,
Frolent Malouda,
Oscar,
Ramires,
Torres,
Peter Cech.
Wote hao ni aina ya wachezaji ambao wanajua jinsi ya kushinda makombe(jamaa amewaita winners). Hivyo Hazard hakuwa mpweke kwenye timu.
Na unaweza kumuona Hazard wa leo is a mature player. Anajua kusadia timu kupata vikombe
 
Yaani utadhani wewe hutakutana na huyo cty, kumbuka msimu uliopita alikupiga nje ndani,
 
Angewasaidia na Belgium basi kupata kikombe
 
Ukweli unabaki pale pale.
Ushindi wa Leicester ya 2015 ulichangiwa na vitu vikubwa viwili.

1. Inconsistency katika big teams hasa Man U na Man City ukiachilia mbali Chelsea ambayo ilikuwa imeparaganyika kabisa. Kwa hiyo hata timu zilizotegemewa kutoa ushindani zilikuwa na matatizo mengine ya ndani. Hivyo hii ilichangia Leicester na Arsenal kubaki kama timu 2 zilizokuwa zikipigania ubingwa na kumbuka Arsenal haina winners, so factor ya pili nitakayoitaja hapa chini ikawapa Leicester odds za kubeba EPL

2. Team spirit.
Hiki ndicho kiliwatofautisha Arsenal, Liverpool na hawa mbweha. Vardy, Mahrez na Ngolo Kante walikuwa na winning spirit ya hali ya juu sana.

Hizo ndizo sababu kuu mbili za kwanini Leicester ilibeba ubingwa 2015 pamoja na kuwa haikuwa na wachezaji wenye uzoefu wa vikombe.

Sasa tukija kwa Liverpool msimu huu utaona inapata upinzani kutoka timu zenye wachezaji wenye uzoefu wa kubeba EPL i.e Man City na Chelsea (na hata Man U usii-underate maana hujui kitakachotokea mzunguko wa pili) tofauti na ilivyokuwa 2015 kwa Leicester ambapo Chelsea inamaliza ikiwa nafasi ya 10 na Man na Man City wakiwa na inconsistency.

Pia swala la winning spirit kwa sasa Liverpool ni tofauti na ilivyokuwa kwa Leicester 2015. Salah, Mane, Firminho sijawaona wakiwa na mentality ya akina Vardy, Ngolo na Mahrez. Kumbuka Mahrez, Ngolo na Vardy wote walikuwa included katika PFA team of the year 2015
 
Na mm Kyatile nitakuwepo kufyekelea mbali
 
Angewasaidia na Belgium basi kupata kikombe
Kombe la dunia ni kitu tofauti kabisa. Lakini hata nafasi ya Tatu ni mchango wake mkubwa. Argentina, Brazil na Ureno zilifika wapi? Wewe usitake kubadili mjadara bwana. Tuzungumzie makombe haya yanayowaonyesha wachezaji kila mwaka
 
Bora gari moja linalofanya kazi muda huu kuliko kuwa na magari matano ambayo yamechakaa na hayafanyi kazi tena ila yamebaki tu kuwa maonyesho kwa wajukuu.
Hili ni jibu mujarabu kabisa. Huu mjadala wa kujivunia historia umeishia hapa.
 
Kama hujamuelewa ngoja nikueleweshe. Alichozungumzia hapo ni kwamba timu ni vizuri ikarecruit wachezaji ambao wameshazoea kuchukua makombe au hata kama hawajazoea basi kuwe na wachezaji ambao wameshachukua toka zamani. Hazard alikuna Chelsea kawakuta kina Didier wameshazoea mataji na yeye akaingia kwenye mfumo huo.

Unamsajili Shaqiri unategemea akupe nini huyu? Ni heri usajili anayetoka nje ya EPL Atleast anakuwa na motisha kucheza ligi inayotazamwa na sana ulimwenguni. Hawa wanakua na passion.
 
Acha kukalilishwa ..........
Shaqiri ana
DFL super cup 1
Uefa super cup 1
FIFA club world cup
DFB cup 2
Bundesliga 3
Uefa Champions league 1
Narudia Tena Acha kukalilishwa
 
Huyo shakir unaemtaja anayo champion's league medal 🥉
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…