Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,606
- 81,641
wanawake pia wanaweza wakiwezeshwa hivyo tumwezeshe aje kuwa mchambuzi wa soka la kimataifa
Naona watu wanakariri sana mpira
Kosa sio kumtoa Salah ila hayo ni matokeo ya mpira na lazima tuujue na sio kuukurupukia.
Roma wangeweza kupata magoli ata Salah alipokuwepo uwanjani. Tayari watu wamesahau kuwa dakika 20 za mwanzo za mchezo Roma ndio walionekana kuwa hatari zaidi, je Salah hakuwepo uwanjani??
Wewe mpenzi wa mpira unayesema mechi bado mbichi huku moyoni mwako unasema Liverpool bila Salah ni nyeupe je huko kwao Roma Salah hatocheza?? Jibu ni kwamba atacheza.
Mnasahau kuwa Liverpool ni mabingwa mara 5 ulaya huku wakiwa na historia nyingi za comebacks ambazo huyo Roma hana. Kuwafunga Chelsea na Barca kwao sio kipimo cha ubora.
Wewe shabiki wa mpira unayekaa ukiwa na mtazamo wa mwelekeo mmoja nataka nikukumbushe tu kuwa, Liverpool ndiyo timu pekee ambao ina wastani wa kufunga angalau magoli matatu katika mechi za ugenini msimu huu wa UCL.
Hii post naiandika kishabiki ila na facts tupu. Unaposema kuwa Liverpool ina beki mbovu je unataka kusema kuwa beki nzuri huwa haifungwi magoli?? Je unataka kusema kuwa wao Roma waliweka wale washambuliaji wao wafanye jukumu la ulinzi au la kushambulia??
Unaposema Liverpool inabeki mbovu huku kuna timu mnazoamini kuwa zina beki bora kabisa na zimeshatolewa tunakuwa hatuwaelewi na tunakuwa na mashaka na uwezo wenu wa kuujua mpira.
Ndio mpira una maajabu yake na Roma wameweza kufanya msimu huu kwa kumtoa Barca ila niwaambie tu maajabu ya mpira sio Comebacks bali kuna maajabu mengine ya kufungwa nyumbani na ugenini kwa goli nyingi na hayo pia yatafanywa kwa Roma pia.
Ili Liverpool isikufunge basi cheza mipira ya kihuni huni ambayo haina utaratibu kama ya yule mwimbisha kwaya ya taarabu kikundi cha Old Trafford. Ukija wote tucheze mpira kwa faida ya mashabiki my friend hii Liverpool haitokuacha Salama.
Narudi kwa nini Salah anatoka: Salah kwa sasa ndo Star player wa timu ni lazima kocha amlinde.
Umeshaongoza goli tano unachotaka ni kipi tena?? Je unataka aendelee kuwepo uwanjani ili aumizwe na mabeki waloijikatia tamaa??
Je unapokuwa na timu yenye kikosi finyu huku wachezaji wako tegemezi wengi ni majeruhi unatakiwa kufanya nini zaidi ya kuwalinda waliopo ili usiongeze majeruhi??
Risk ya kurudisha goli tano bila Salah ni ndogo sana kuliko risk ya kumpoteza salah kwa majeruhi. Ni kichaa tu ndo asingemlinda mchezaji wake bora hasa pale anakuwa Tayari katimiza wajibu wake.
Niwaambie tu kitu: Tatizo la magoli kufungwa anapotoka Salah uwanjani sio Salah kutoka bali tatizo ni wanaoingia kama mbadala wake.
Mchezaji anayembadili Salah haingii kufanya majukumu ya Salah zaidi anaenda kuikaba timu yake.
Niwakumbushe tu: Mechi bado mbichi sana kama mnavyosema na maajabu yatatokea ila hayo maajabu yatakuwa ni ya Roma kufungwa goli nyingi sana kwake. Ila msije mkageuka na kusema kuwa Roma hakustahili kucheza nusu fainali na wengine mtasema hii ni nusu fainali mbovu kabisa ya muda wote...!
Ila kweli Liverpool inabeki mbovu sana ila nashangaa imefikaje nusu fainali na ubovu huo inamaana timu zingine nazo hazijui kufunga. Bora kuwa na silaha unayoweza kuitumia kifasaha kuliko kuwa na ngao ambayo haiwezi ata kukuokoa vitani.
Jana tumetia mpapaso mechi ya pili tunakula kiboga sebuleni kwenye nyumba ya mshua wao (sisi watoto wahuni)
TUKUTANE KIEV.
Jamani vp kuhusu chamberlain anarudi lini?
Hivi Liverpool aliwahi lini kupoteza fainali nipe jibu
Mara moja tu, 2007!
Asante kwa ufafanuzi mkuuTumewahi Kupoteza Fainali Mara 2 Wakuu!
1) Mwaka 1985 tulipoteza dhidi ya Juventus! Walitufunga goli 1 - 0 na goli lilifungwa na Platin Kwa Njia Ya Mkwaju Wa Penalty.
2) Mwaka 2007 tulipoteza dhidi ya AC Milan Kwa Magoli 2 - 1.
Mohamed Salah has been named the Champions League Player of the Week
Na Goli bora la week wanamtangaza lini?
i think formation ya leo ni 3-5-2!!
best of luck!!!..to us Kops!
ynwa
Sadio Mane Atakosa Mchezo Wa Kesho dhidi Ya Stoke City Kutokana Majeruhi! Tuombe Arudi Kikosini Kabla Ya Jumatano.