Liverpool Legends 5-5 Bayern Munich Legends.
Mechi ilikua kali na yakusisimua. Magoli ya Liverpool yamefungwa na Dirk Kuyt, Robbie Fowler (2), Michael Owen na Bjon Tore Kvorme.
Magoli ya Munich yamefungwa na Alexander Zickler (2), Luca Toni, Sergio na Xabi Alonso.
Nyota wa mchezo na alievutia wengi ikiwamo mimi ni Alexander Zickler alieonekana huenda ndie mzee kuliko wote lakini alionyesha uwezo mkubwa kiufundi na kwangu ndie alikua nyota wa mchezo.
Kikubwa nilichofurahia katika hii mechi ni kuwashuhudia ma legend ambao wengi wao ndio walini inspire kuipenda klabu ya Liverpool, Owen, Fowler, McManaman, Gerrard, Berger, McAllister, David James na wengine walionifanya nizidi kuipenda kama Carragher, Riise, Alonso, Kuyt, Smicer, Agger..
Nime enjoy sana weekend hii isiyokuwa na ligi kwa kutizama mtanange huo