Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Our Next Five Games (Exclude Tottenham) seemed to be our next 15 points for sure...

Screenshot_2016-10-24-09-22-19.png
 
Top four is our target.Let's not put pressure on our players for the title.We can't deny if it happens but let it just be 'by the way".This is very important if we want to maintain our current form.Lets do it in a Klopp way when we come to public
 
Top four is our target.Let's not put pressure on our players for the title.We can't deny if it happens but let it just be 'by the way".This is very important if we want to maintain our current form.Lets do it in a Klopp way when we come to public
Nini tofauti kati ya wachezaji weti na wa arsenal. Kwa mmoja mmoja na hakika tumewazidi arsenal man u hata Chelsea n Tottenham tuko sambamba na man city so sioni why not tusiwaze ubingwa. We have easy fixture between now to Dec 31 vs Man city let's just make it count am sure by the end of this year tutakuwa top pale hata kwa gepu la point 10
 
Liverpool like atletico de Madrid",..
hawana Superstars wa ulimwengu(mean wenye garama na majina yanayozunhumzwa na kila media) isipokua team work ndio zinazozipata hizi timu.

bora team work kuliko majina,.. sababu mmoja akikosekana ni ngumu kuona pengo mf.Alikua Torres A.Madrid akaondoka pengo halikuonekana the likes of Aguero,Falcao,Costa, Turan
tofauti na timu ya superstarz

Klop respect to you",.. kikosi kile kile cha BR kwa 50% ila Hata Haters wanakubali ule ni mziki sio muondoko...
Nasubiri wachezaji wazidi kuingia kwenye geggenpressing,.. Can ameanza Ku cope,..
nasubiri Grujic nae
YNWA
klopp stay with kop
 
Migs ataanza game ya kesho

Our capt ataikosa game ya kesho baada ya kupata technical yellow card

Ingawa game ni ngumu ila napenda kumuona Stewart na Grujic ndani
 
Nini tofauti kati ya wachezaji weti na wa arsenal. Kwa mmoja mmoja na hakika tumewazidi arsenal man u hata Chelsea n Tottenham tuko sambamba na man city so sioni why not tusiwaze ubingwa. We have easy fixture between now to Dec 31 vs Man city let's just make it count am sure by the end of this year tutakuwa top pale hata kwa gepu la point 10
Tofauti ya wachezaji wetu na wa arsenal inahusiana na nini sasa hapa?

Tuepuke pressure zinazoepukika ndo point yangu.Ranieri amefanikiwa mwaka jana kwa kuignore hizi media pressure.Sio kwambaalikuwa hataki ubingwa lakini aliamua kusema tu kuwa yeye lengo lake ni kuingia top four.Kwenye dressing room ni lazima alikuwa anaongea kitu tofauti na wachezaji wake.

Kinachoonekana sasa hivi ni kutaka kukubali hii media tension ituchukue kuwa sisi ni title contenders.Furaha ni kuwa Klopp knows that better ukimsikiliza anavyojibu maswali ya waandishi.Anaepuka sana kuweka pressure kwa mchezaji mmoja au timu nzima.That is why i suggested to keep it in a Klopp way
 
Ndugu wa Kop hivi yule assistant coach wa Klopp cjawahi kumwona anacheka aise. Anaitwa Brain buvac. Yeye hata timu ishinde 5 yy yuko serious tu. Yule jamaa mshawah kumwona?
TUMFAHAMU KIDOGO BRAIN BUVAC (KOCHA MSAIDIZI WA LIVERPOOL)


Jina lake la kwanza ni Zeljko likifuatiwa na Buvac. Ni m' Bosnia kwa utaifa na ndiye kocha wa kwanza msaidizi Liverpool ambako alijiunga mwaka 2015, mwezi wa kumi.

Buvac na bwana Klopp, ama Kloppo kama Buvac apendavyo kuita, wamekuwa marafiki wa karibu sana tangu wakicheza pamoja klabu ya FC Mainz kwenye mwanzo wa miaka ya 1990.

Huko (Mainz, na hata baadae Rudar Ljubija, Banja Luka, Rot Weiss Erfurt na Neukirchen) alikuwa kiungo mshambuliaji. Na alitundika daruga akiwa na miaka 36.

Kwenye timu yake ya mwisho kucheza, Neukirchen, ndipo alipoanza kuchukua hatua yake ya kwanza kwenye tasnia ya ukocha kabla hajaenda kuwa msaidizi wa Klopp kule Mainz mwaka 2001.

Lakini tuweke akilini kwamba, Buvac na Klopp waliweka nadhiri ya kwamba baada ya kutundika daruga basi watajihusisha na kazi ya ukocha. Na hivyo basi kwakuwa walikuwa wameshibana sana, wakaweka pia nadhiri ya kwamba kati yao, yeyote yule atakayekuwa wa kwanza kupata kazi ya ukocha, atamuita mwenzake awe msaidizi wake. Hiko kiapo kinaishi mpaka leo hii.

Pale Klopp alipotoka Mainz kwenda Borussia Dortmund, akaenda tena na mfuasi wake huyu, mwaka 2008.

Ilikuwa kwenye ground ya Westfalenstadion ndipo philosophy ya Klopp na Buvac ikachanua. Makombe ya Bundesliga mwaka 2011 na 2012 yakawafanya watu wawarushie macho makocha hao na kuwapa heshima inayostahiki.

Mwaka 2013, Borrusia Dortmund ikiwa kama timu inayocheza mpira mzuri na wa kuvutia Ulaya, walifika fainali na Buyern Munich ingawa bahati haikuwa kwao wakasogezwa kando.

Buvac aliungana na Klopp kwenye kuikacha Dortmund msimu wa mwaka 2014 - 15, lakini mapema akachepukia Liverpool na bwana Klopp wakitumai kuendeleza mafanikio yao.

Na July 8, Liverpool ilitangaza Buvac ameungana na Klopp pamoja na Krawietz kwenye kusaini mkataba mrefu na Liverpool.

KUHUSU U 'SERIOUS' WAKE.


Kwa namna moja ama nyingine, Buvac huonekana ni mtu mtulivu asiye na papara. Makini na asiyependa kupanua mdomo wake pasi na sababu shinikizi. Hulka yake hii imetengeneza ukuta fulani na wachezaji.

Inasemekana pale Buvac anapoongea jambo, huwa basi lina mkazo ndani yake. Ni mkali, kuliko Klopp. Na muda mwingine pale ambapo Klopp anakuwa 'frustrated' ama 'mad' basi hapo ndipo Buvac huchukua fursa kuwapa 'kavu' wachezaji. Au pale Klopp anapokuwa speechless, ama kuremba maneno, Buvac basi hupaka rangi halisi.

Hili limekuwa likiwasaidia kutimiza na kufanya kazi yao vizuri zaidi kutokana na kamgawanyo haka ka madaraka mbali tu na kupeana maoni, mawazo na maono.


BUVAC THE BRAIN, OR THE RIGHT HAND.


Kwa mujibu wa Klopp, Buvac kwake ni ubongo kwani humtegemea sana kwenye mawazo. Ila hili Buvac amekuwa halishabikii sana japo anali 'appreciate'.

Na kuthibitisha zaidi hili, amekuwa pia akimuita mkono wake wa kuume, kumbuka si wa kushoto. Hivyo basi waweza kuona ni kwa namna gani wanategemeana.

Kwa mujibu wa Nuri Sahin, mchezaji aliyewahi kupata huduma ya Klopp na Buvac, asema ya kwamba: hakuna tofauti yoyote kati ya Buvac na Klopp. Namna Klopp anavyouona mpira basi ndivyo Buvac hufanya vivyo hivyo. Hilo amelishuhudia walipokuwa timu moja kiasi kwamba hata pale Klopp alipokuwa anaadhibiwa kwa kuwekwa nje ya uwanja, uwepo wa Buvac unajaza nafasi barabara!
 
Mchezo Wetu Wa Mwisho Wa Kukamilisha Mzunguko Huu Wa Kwanza Ambao Utapigwa Ndani Ya Anfield Tarehe 31 December, Kati ya LIVERPOOL v/s MAN CITY ndiyo utakao tupa picha Kamili Ya kuweza Kuchukua Ubingwa..
Kweli katika watu 4 mmoja ni chizi...Yaani unaamini kabisa liver fools watachukua ubingwa? Hata top 4 hakanyagi
 
Our Next Five Games (Exclude Tottenham) seemed to be our next 15 points for sure...

View attachment 423324
Hizo away games sio guaranteed...at least we are sure Southampton at their home ground they will play an attacking game so it will be best situation for our attacking style of play so 50 - 50 on that one...but crystal palace will be tough...

My hope is our worst case scenario iwe 3 home wins and 2 away draws for a total of 11 points... 11 out of possible 15 points sio mbaya... then go on and take 3 points on new year's eve from Manchester City
 
Lile Walilokuwa Wakilisubiri Kopites Kwa Hamu Kutoka Kinywani Mwa JK nadhani ameshalitamka Katika Press Conference ya Pre-match ya Spurs!!

Baada Ya JK kuanza Kumchezeshaa Karius na Kumueka Benchi Simon bila Ya Kutoa Maelezo Yoyote, Wengi Tulidhani JK yupo katika Majaribio Ya Kuangalia Uwezo Wa Karius pale Golini! Lakini JK jana Alitamka Rasmi Kuwa GK wake Namba 1 ni Loris Karius, Na Simon Mignoleta ni Namba 2.

Nanukuu: "This is the ranking, if you want, in this moment, Loris is the No. 1 and Simon is in this moment the No. 2"

Hata Hivyo JK amekiri Kuwa LK Bado Anahitaji Mechi Zaidi ili aweze kukomaa Katika Udakaji Kwani Badi Hajawa Full experienced..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom