Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

Samahni picha zingine zina kuwa nyeusi kwa ajili ya jua kali
 
Kamanda fundi kira akirudi kuketi
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1361196781246.jpg
    uploadfromtaptalk1361196781246.jpg
    99.8 KB · Views: 78
Kamanda Rose Kamili
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1361196902645.jpg
    uploadfromtaptalk1361196902645.jpg
    86.3 KB · Views: 77
Kamnda
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1361197123762.jpg
    uploadfromtaptalk1361197123762.jpg
    71.5 KB · Views: 72
Ila kwa hili la majimbo yatupasa tuwe makini sana wakati wa kulipeleka kwa wananchi!!kwani yaonekana dhahiri kuwa watanzania wengi bado hawajawa na elimu(ufahamu) wa kutosha kuhusiana na issue hii ya majimbo,hivyo yaweza tumika kinyume na mahasimu wetu CCM kuonyesha kuwa CDHADEMA ni chama chenye lengo la kuigawa nchi,na kama member mmoja alivyowahi ku comment hapa ni vyema zaidi kama harakati hizi zingeanzia upande mwingine kabisa tofauti na kaskazini,ili kuondoa dhana iliyopandikizwa kuwa cdm ni chama cha kaskazini.
Mkuu haikutolewa amri kwamba waanzie kanda ya kaskazini,hii inatokana na usharp wa mratibu wa muda wa kanada ya kaskazini mabe pia ni katibu wa mkoa wa Arusha,Time frame ni moja isipokuwa kila watu wajipangie waanze lini lakini miezi ni hii hii utasikia kimelia kila kanda.ila nakuunga mkono juu ya elimu kuhusu sera ya majimbo kwamba kuna haja ya kuungana wote kama wanachama,viongozi,na individuals kutoa elimu kwa mapana yake juu ya sera ya majimbo.
Kanda ya Kaskazini nawapa Big up sana alunta continua,na kanda zingine tuchangamke fasta to launch hii kitu mapema na kisha tuanze operation
 
Kamanda Nassary
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1361197182293.jpg
    uploadfromtaptalk1361197182293.jpg
    70.2 KB · Views: 90
nasari anasema haiwezekani watoto wana maliza la saba hawajui ---- na kuandika huku watoto wao wakisoma shule za nje..
 
Joseph Selasini:
Leo tunazindua kanda ya kaskazini, hivyo atakayezungumza atakuwa mw/kiti.

Nassari:
Ndg zangu, ile noma yangu na Makinda na Ndugai inaendelea.
Haiwezekani watoto wetu wanamaliza shule hawajui kusoma wala kuandika.
Kama hawatarudisha hoja yangu noma itakuwa noma.
 
Grace Kiwelu:
Tumeamua kuyaweka makao makuu kuwa Arusha, ila kwa heshima ambayo tumeiweka.
 
Dogo janja Mh. Nassari kwa kweli nimetamani apewe nafasi lakini ndiyo hivyo muda haitoshoshi!
 
Lema ndani ya jukwaa na hakika umati umezidi uwezo wa jukwaa!
Ama kweli tumefanya makosa kwani ingependeza umati huu uwepo hapo Shehk Abed Stadium kidogo ingetosheleza umati huu!
Anadai ana mengi ya kusema ila muda haitoshi!
Anamalizia kwa kusema A town hatuna Meya!
 
Lema:
Ndugu zangu, leo tuna viongozi wengi, ambapo mzungumzaji wetu atakuwa mwenyekiti wetu, ambaye ayatueleza nini maana ya kanda. wenzetu magamba wamejaribu kupotosha kuwa maana ya kanda ni kutaka kuwagawa watu kwa ukanda.
Ndg zangu, natambua shida za watu wa Arusha, mna shida ya maji.
Kuanzia alhamisi ijayo tutazunguka jimbo zima.
Mpaka sasa watu wa Arusha tunasema mpaka sasa hatuna meya.
 
Lema anasema lengo kuu ni kuzindua kanda ya kazikazini, anasema watawaelewesha wananchi kwani mafisadi walitaka kupotosha dhana ya kanda leo mwenyekiti atafafanua..anajua arusha bado kuna kero..wananchi wanamwambia Lema kuwa wanasumbuliwa na mgambo lema ana waambia mgambo ni size yao.
 
Mbunge wa Karatu Mh. Israel Natse ndiyo mwenyekiti wa Kanda.
Natse:
ccm bye bye.
Ndg wananchi tunayo kazi moja tu. kazi tuliyonayo ni ya kumkomboa mtanzania.
watu wanahitaji mabadiliko na wanataka yatimie mara moja.
serikali ya ccm imefika pabaya, hatua ambayo wameamua watu wachinjane.
kule zanzibar wameuana serikali imekaa kimya.
Geita watu mchungaji ameuawa kikwete amekaa kimya.
zanzibar padre ameuawa kikwete amekaa kimya.
Kikwete hatufai ikulu, aondoke siyo kiongozi anayetufaa.
Watanzania sasa muda wa kulalamika umeisha, ni wakati wa kufanya maamuzi.
wanasema kuna usalama wa taifa. ni usalama gani wa taifa hawaoni mauaji na ufisadi, lakini unaona harakati za chadema.
 
M/kiti F. Mbowe anaendelea na anasema wamekutana viongozi zaidi ya 500 juzi na tukaamua ya kwamba tumeamua kubadilisha mbinu ya kuing'oa ccm madarakani!
 
Back
Top Bottom