Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
attachment.php



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kinafanya mkutano mkubwa wa hadhara Arusha,ambao pia utatumika kuzindua utekelezaji wa sera yake ya utawala wa majimbo kwa kuzindua Jimbo la Kaskazini.

Katibu wa Muda wa Kamati ya Uratibu Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema mkutano huo utafanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro na utahudhuriwa na wabunge wote wa CHADEMA kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa Golugwa, Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

“Tunazindua Kanda ya Kaskazini kutekeleza uamuzi wa Baraza Kuu lililoagiza mfumo na shughuli za uendeshaji wa chama ushuke hadi ngazi ya majimbo ambayo ndiyo sera ya CHADEMA,” alisema Golugwa.

Kabla ya mkutano wa leo, viongozi zaidi ya 200 wa CHADEMA kutoka mikoa na majimbo 30 ya Kanda ya Kaskazini wakiwamo wabunge, wenyeviti, makatibu, wenyeviti na mameya wa Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA,walifanya vikao vya ndani kuweka mikakati na mfumo wa utendaji kikanda.

Kwa mujibu wa Golugwa, ambaye pia ni Katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha, kikao cha ndani pia kilihudhuriwa na mwasisi na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei.

Mbowe ambaye ni mmoja wa wajumbe waliohudhuria vikao vya ndani, ndiye atakuwa mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu kwenye mkutano wa hadhara ambao pia utatumika kuwatambulisha wajumbe wa timu ya uratibu ya Kanda ya Kaskazini.

Mkutano huo ni wa pili kwa CHADEMA ndani ya wiki mbili zilizopita baada ya kufanya mkutano mkubwa Dar es Salaam uliotumika kuueleza umma udhaifu wa mhimili wa Bunge na ukandamizaji unaodaiwa kufanywa dhidi ya wabunge wa chama hicho na uongozi wa mhimili huo wa dola.

Katika mkutano huo, viongozi wa CHADEMA waliutangazia umma namba za simu za Spika Anne Makinda na Naibu wake, Job Ndugai ili wananchi wawapigie au kuwatumia ujumbe mfupi kuwashinikiza kufuata Katiba, Sheria na Kanuni za bunge katika uendeshaji na maamuzi ya chombo hicho.

Update:
Niko kwenye uwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro ambapo kunafanyika mkutano wa uziduzi wa Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga, utahudhuriwa na wabunge wote wa CHADEMA kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini na kuhutubiwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe.

kwa sasa watu wanazidi kumiminika, tuungane kuwa habarisha wale wote ambao hawajafanikiwa kufika kwenye uwanja huu kwa njia moja ama nyingi...
picha zina kuja

attachment.php

Viongozi wakiwa tayari washawasili
attachment.php

Wananchi wakiwa mkutanoni
attachment.php

Mwenyekiti taifa (CHADEMA) akisalimia wananchi waliojitokeza kwenye mkutano

attachment.php

mwenyekiti Mkoa wa Tanga,Said Salehe Mbweto akizungumza
attachment.php

Kamanda akizungumza kwa hisia kukemea propaganda za udini za CCM

attachment.php

Kamanda wa mkoa wa Manyara akihutubia

attachment.php

Kamanda Basil Lema akihutubia

attachment.php

M/kiti Mbowe jukwaani tayari,tayari anazungumziwa sera ya CHADEMA,mfumo mpya wa utawala (majimbo)

attachment.php

Mwenyekiti Taifa akisisitiza jambo.
 

Attachments

  • chadema.jpg
    chadema.jpg
    9.7 KB · Views: 5,419
  • 1.jpg
    1.jpg
    36.1 KB · Views: 6,909
  • 2.jpg
    2.jpg
    48.2 KB · Views: 4,325
  • 3.jpg
    3.jpg
    35.2 KB · Views: 4,345
  • 4.jpg
    4.jpg
    31 KB · Views: 3,710
  • 5.jpg
    5.jpg
    33 KB · Views: 5,993
  • 6.jpg
    6.jpg
    35.2 KB · Views: 4,400
  • 7.jpg
    7.jpg
    47.9 KB · Views: 6,557
  • 8.jpg
    8.jpg
    46.8 KB · Views: 5,944
  • 9.jpg
    9.jpg
    35.2 KB · Views: 4,255
Ila kwa hili la majimbo yatupasa tuwe makini sana wakati wa kulipeleka kwa wananchi!!kwani yaonekana dhahiri kuwa watanzania wengi bado hawajawa na elimu(ufahamu) wa kutosha kuhusiana na issue hii ya majimbo,hivyo yaweza tumika kinyume na mahasimu wetu CCM kuonyesha kuwa CDHADEMA ni chama chenye lengo la kuigawa nchi,na kama member mmoja alivyowahi ku comment hapa ni vyema zaidi kama harakati hizi zingeanzia upande mwingine kabisa tofauti na kaskazini,ili kuondoa dhana iliyopandikizwa kuwa cdm ni chama cha kaskazini.
 
Jamani siku hizi sijui nimekuwaje nikisia au kusoma popote palipoandikwa Chadema au M4C nasikija furaha kupita kiasi naona ukombozi huo hapo.... Jamani cdm naipenda sana acheni utani. Nina bendera ya cdm huwa inanipa faraja sana nikiangalia
 
mkuu yani.naelekea sasa hivi uwanja wa shule ya ngarenaro.kusikiliza sera za chama makini.na kipenzi cha mioyo ya watanzania wote kwa sasa.
 
twanga kote kote makamanda. kazi yenu inaonekana!..jamaa wa lumumba hawalali...
 
PRINCE CROWN; Kama uko on line sema nikuseach hapo uwanjani! Je nikuPM?


QUOTE=PRINCE CROWN;5721579]mkuu yani.naelekea sasa hivi uwanja wa shule ya ngarenaro.kusikiliza sera za chama makini.na kipenzi cha mioyo ya watanzania wote kwa sasa.[/QUOTE]
 
Last edited by a moderator:
Makamanda leo ni uzinduzi rasmi wa Kanda ya Kaskazini ya CHADEMA. Juzi na jana tarehe 16-17 Feb kulifanyika vikao vya Kanda hiyo vya kupanga mpango mkakati na kuzindua kanda hiyo.

Leo tarehe 18 Feb kutafanyika Mkutano Mkubwa wa hadhara wa uzinduzi wa Kanda hiyo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro kuanzia saa 8:30 Mchana. Kanda ya Kaskazini inajumuisha mikoa yaArusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

Mkutano huo utawajia live katika radioarushamambo ambayo link yake ni Online Radio Stations in Tanzania bofya radioarushamambo. M/Kiti wa CHADEMA Taifa atakuwa ndie Mgeni Rasmi katika Mkutano huo.

Karibuni sana nyote.
 
Nimesikia gari la matangazo linatangaza juma tano mwenyekiti wa Chadema taifa Mh. MBOWE atakuwa Mwanza nafikiri ndo uzinduzi wenyewe pande za mwanza.
 
Back
Top Bottom