Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

Live Updates: Mkutano wa CHADEMA - Arusha!

Mwigamba:
Tumedhamiria kuanzisha sera za majimbo ili kuweza ku-decentralize majukumu kwa maslahi ya watanzania, ni mfumo unaopunguza majukumu kutoka makao makuu
Vile vile Mkuu itapunguza gharama za uendeshaji serilkali, mara mkuu wa mkoa mara wilaya, yote hayo tunabana matumizi!!! CHADEMA wanatumia ubongo kufikiri juu ya maslahi ya nchi yetu!!!

mbowe anasema tumekutana arusha kutokana na azimio la chama chenu kuwa sasa tubadilishe mbinu, tumeongeza nguvu mbungeni, madiwani imebaki kuliongaza bunge na Ikulu, mbinu hii ni mbinu shirikishi, kwa miaka 20 mapambano yote hupangwa dar sasa tuna kula sahani moja..
 
Mwigamba:
Tumedhamiria kuanzisha sera za majimbo ili kuweza ku-decentralize majukumu kwa maslahi ya watanzania, ni mfumo unaopunguza majukumu kutoka makao makuu
Vile vile Mkuu itapunguza gharama za uendeshaji serilkali, mara mkuu wa mkoa mara wilaya, yote hayo tunabana matumizi!!! CHADEMA wanatumia ubongo kufikiri juu ya maslahi ya nchi yetu!!!

twanga kote kote makamanda. kazi yenu inaonekana!..jamaa wa lumumba hawalali...
..si walisema kila cdm wanapomaliza wao wanapita kusafisha ndo maana walienda temeke,ngoja nisikie tarehe watakayokuja arusha baada ya cdm..
 
Mbowe anapanda jukwaani.
Mbowe:
Namshukuru sana mwenyenzi Mungu, kwamba leo tumekutana tena kuzungumza mustakbali wa taifa letu.
tumekutana juzi na jana na viongozi takriban mia tatu, tumekutana arusha kufuatia azimio la chama chenu, kwamba mapambano dhidi ya ccm, kwamba tubadilishe mbinu.
tumwongeza nguvu bungeni, tumeongeza nguvu kwa madiwani, tumebakiwa na mbinu moja muhimu, ambao tunaita mbinu shirikishi.
Mbinu ambayo kila moja ataweka maslahi ya taifa mbele kuleta ukombozi.
kwa miaka 20 ambayo chadema ilikuwepo, mapambano yote yamekuwa yakipangwa daresalama, sasa tunapiga chini kwa chini, na kazi ya chama itaendelea kufanywa ki silencer.
Watanzania walio wengi hawajaelewa sera za majimbo.
Watanzania hawana kauli juu ya rasilimali zao.
watanzania hawana kauli juu ya hatima ya maisha yao.
maamuzi yanafanywa na watu ambao watanzania hawakuwachagua.
Tulipiga kura kuwachagua madiwani, wabunge, lakini hakuna aliyepiga kura kumchagua mkuu wa mkoa wala mkuu wa wilaya.
Mimi Mkuu wa mkoa simwogopi, kikwete simwogopi.
 
Dah, chadema kama kambale,mnawatesa sana ccm jamani,yaani wakishika huku mnapiga huku wakikaa kimya mnagonga mpaka wanachanganyikiwa,muwe na huruma kidogo,mtawaua kwa presha ! teheh,tehee
 
M/kiti anasema hakiamungu hii katiba akiwekwa mkuu wa mkoa na wilaya nawaambia Nchi hii haitatawalika na itakuwa mfano Duniani!

Kudadeki!
 
Mbowe:
Kama kuna watu hatari nchi hii ni wakuu wa mikoa na wilaya.
Kama wataendelea kuwatambua kwa katiba mpya hakyamungu mimi mbowe kitaeleweka.
ccm wanaleta masihara kwenye maisha ya watu.
tunakataa vyeo vya kishkaji.
 
Mbowe:
Katika sera zetu.za majimbo, tunasema viongozi wote watokane na kura za wananchi.
 
Gefu; Nakwambia CDM haitawaponyesha hawa mafisadi!
Hakuna kujuana!
Viongozi wote watokane na kura ya wananchi hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wa chama!
Hapatatosha kwa mafisadi kudadeki!

Dah, chadema kama kambale,mnawatesa sana ccm jamani,yaani wakishika huku mnapiga huku wakikaa kimya mnagonga mpaka wanachanganyikiwa,muwe na huruma kidogo,mtawaua kwa presha ! teheh,tehee
 
Last edited by a moderator:
ukubwa wa tanzania ni sawa sawa na nchi tano yaani kenya, uganda,malawi..kwenye sera za majimbo anasema mali zinazotokana na maliasili zimilikiwe na wananchi na siyo serikali maana matokeo yake wanamiliki wao na wake zao..
 
Mbowe:
Tunasema mali ambazo tumepewa na Mungu ni mali ya watanzania, siyo mali inayomilikiwa na serikali.
Kipaumbele cha kwanza ziwe ni watanzania.
siyo kila kitu Dar.
Hatukubali uwendawazimu wa serikali kurundika kila kitu kifanyiwe maamuzi Dar.
Serikali ya ccm inakusanya kodi nyingi ajabu.
 
anasema balaa lilianzia kwa mkapa pesa ikahamia serikalini wananchi wakawa wanashangaa ukapa unatokana na nini..
 
Wakati Mwinyi anaondoka madarakani alikuwa anakusanya kodi bil 27.
Mkapa bil 127 kwa mwezi wakati anondoka madarakani.
Kikwete mpaka sasa anakusanya kwa mwezi moja kuanzia mwezi wa 11 mwaka jana anakusanya Trilion 1. hizi kodi zinakusanywa kutoka kwa wananchi maskini, huku matajiri wakubwa wamepewa misamaha ya kodi.
Ndiyo maana safari za kikwete haziishi, kila mara uwanja wa ndege.
 
Asanteni live updaters, najihisi kama nipo hapo uwanjani ngarenaro.
 
Kila kiongozi wa chadema ni lazima ajue tawi lake liko wapi.
Hawa magamba lazima tuwakabe mpaka penalt
 
Wakati Mwinyi anaondoka madarakani alikuwa anakusanya kodi bil 27.
Mkapa bil 127 kwa mwezi wakati anondoka madarakani.
Kikwete mpaka sasa anakusanya kwa mwezi moja kuanzia mwezi wa 11 mwaka jana anakusanya Trilion 1. hizi kodi zinakusanywa kutoka kwa wananchi maskini, huku matajiri wakubwa wamepewa misamaha ya kodi.
Ndiyo maana safari za kikwete haziishi, kila mara uwanja wa ndege.

Hongera Mwenyekiti Mbowe kwa hotuba yenye utaifa na uzalendo. Jimbo la nyanda za juu kusini tunategemea ndo litafuatia kwa uzinduzi mkubwa,
 
Mbowe:
Ni marufuku kwa mwanachadema kwenda kwa balozi wa ccm.
Kila penye balozi wa ccm tuhakikishe kuna balozi wa chadema.
Kesho naenda kuzindua kanda ya ziwa, nitazindua kanda zote mpaka unguja na pemba.
haya mapambano tumeamua kuyahamishia ardhini.
uchaguzi ujao hawa jamaa hawana pakutokea.
 
Back
Top Bottom