Live update: Yanayojiri kwenye uchaguzi kata za Ipole na Kiloleli - Sikonge!

JACADUOGO2.

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
930
217
Kwa sasa nipo Ipole, wana wa nchi wanazidi kumiminika kwenye vituo vya kupiga kura na kadri muda unavyozidi kusogea ndivyo na matumaini ya CCM yanavyopotea na ishara za CHADEMA kushinda zinaongezeka!
Baada ya saa moja nitakuwa Kiloleli kuwajuza yanayojiri, lakini kwa ujumla CCM wako chali. Tuvute subira kwa matokeo za zaidi ya kituo baada ya kituo na matokeo kwa ujumla.
NB: Natumia Nokia 2323c ambayo haina kamera, kwa hiyo msiniulize habari ya picha! Ahsanteni.
 
Pamoko sana, wazodoeni kina ndugai na makinda kuwa ulinzi wanaowapa mafisadi bungeni unatukera sana na adhabu yake waione kwenye hizi chaguzi.
 
Hivi CUF sio chama cha uypinzani............mbona sioni mtu yeyote humu jamvini akisema kuhusu cuf? au cuf haina wanachama humu.....Au cuf wao ni vitendo zaidi sio maneno km cdm?......au ile ndoa imekuwa tamu mno kiasi cha mtu akisema ccm anakuwa amesha include na cuf?
 
Kila mpiga kura leo ni bosi, maana anamiliki uamuzi wenye impact kubwa ajabu.
Wapiga kura msichezee nafasi hiyo. Fanyeni maajabu.
 
Safi sana Kamanda. Bahati mbaya mie nipo huku Tutuo kwa leo kwa shughuli muhimu.

Jioni ntakuwa SIKONGE tena kufuatilia matokeo.

Shusha vitu huko na tutasubiri kujua nini kinaendelea.
 
Safi sana Kamanda. Bahati mbaya mie nipo huku Tutuo kwa leo kwa shughuli muhimu.

Jioni ntakuwa SIKONGE tena kufuatilia matokeo.

Shusha vitu huko na tutasubiri kujua nini kinaendelea.
ingawa maeneo yote haya siyajui, hata sikuwahi kuyasikia zaidi ya humu JF, lakini nafarijika sana na updates. JF ni mtandao mzuri sana kwa mawasiliano.
 
Wakati nipo kwenye pikipiki natoka Kiloleli nimeliona gari moja (Landcruiser) likiwa na bendera ya CCM karibu kabisa na kituo cha kupigia kura eneo la getini (Ipole). Bahati mbaya sikuwa na simu yenye kamera halafu limenipita kwa kasi kubwa sana. Ila nalifuatilia, nikiliona nitalipiga picha kwa ushahidi zaidi kwani nimeshapa simu ya moja hapa ya mchina yenye kamera! Ahsanteni sani.
 
aiseeeeeeeee babaangu ngoja 2agize mbege 2sherekeee ushindi wa cdm wakati serekali ya jk inapambana na shee mponda wa uwamwisho dr slaa anatembea nchi nzima kutowa elimu
 
Wakati nipo kwenye pikipiki natoka Kiloleli nimeliona gari moja (Landcruiser) likiwa na bendera ya CCM karibu kabisa na kituo cha kupigia kura eneo la getini (Ipole). Bahati mbaya sikuwa na simu yenye kamera halafu limenipita kwa kasi kubwa sana. Ila nalifuatilia, nikiliona nitalipiga picha kwa ushahidi zaidi kwani nimeshapa simu ya moja hapa ya mchina yenye kamera! Ahsanteni sani.

Lifuatilie sana maana huenda wanataka kuchakachu hao, wanajua maji yapo shingoni!!!
 
Watz wangekuwa wanaelewa umuhimu wa kura zao hii inchi ingekuwa mbali sana think ya kwanza Africa kwa economic growth na mazaga zaga mengine
 
Kila mpiga kura leo ni bosi, maana anamiliki uamuzi wenye impact kubwa ajabu.
Wapiga kura msichezee nafasi hiyo. Fanyeni maajabu.
Kikwete alisema yeye ndiyo mwajiri mkuu lakini kiukweli wananchi ndiyo waajiri wakuu maana bila wako kikwete asingekuwa hapo hivyo na leo wananchi wakata 29 wanatafuta wa kuwa tumikia wasije waka wakawaajiri watu ambao mwisho wa siku watajifanya wao ndiyo maboss...
 
Hivi mwisho wa kupiga kura ni saa ngapi
Hakuna mwisho lakini uwepo kwenye msitari kabla ya saa kumi hivyo hata kama mtakuwa 500000 ikawakuta kwenye mstari basi itabidi msubiriwe mpaka mtakapo maliza kupiga kura tofauti na hapo mwisho saa kumi vinageuka vituo vya uhesabuji kura ...
 
Matokeo kamili ya kata ya Ipole Sikonge ni kama yafuatayo:
CHADEMA - 577.
CCM - 373.
CUF - 48.
Tofauti ni 204.
Mshindi ni kijana mdogo wa CHADEMA Kamanda Mohammed Hija.

Ama kweli ni chama cha wakristo na ukanda wa kaskazini!
 
Back
Top Bottom