Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Chatakiwa Ukamilishaji wa Dirisha la Kieletroniki la Uwekezaji (TeIW)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA (TIC) CHAAGIZWA KUKAMILISHA DIRISHA LA KIELETRONIKI LA UWEKEZAJI (TeIW)

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameagiza Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuharakisha ukamilishaji wa dirisha moja la kieletroniki la uwekezaji (TeIW), kutembelea miradi yote iliyotekelezwa na kuona maendeleo yake na kupanua wigo wa kuvutia uwekezaji kupitia Balozi zetu.

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema hayo tarehe 27 Mei, 2023 alipokuwa akizindua bodi ya TIC na kusema kuwa jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuvutia wawekezaji kupitia filamu ya royal tour na ziara mbalimbali zimepelekea kuongezeka maradufu kwa watalii na wawekezaji nchini.

"Naiagiza TIC kuharakisha ukamilishaji wa dirisha moja la kieletroniki la uwekezaji (TeIW), kutembelea miradi yote iliyotekelezwa na kuona maendeleo yake na kupanua wigo wa kuvutia uwekezaji kupitia Balozi zetu. Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji - (WUVB). Uzinduzi bodi ya TIC, 27 Mei, 23

Aidha, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) aitaka SIDO kutengeneza mkakati wa muda mrefu na mfupi wa kuendeleza viwanda vidogo, kupanua wigo wa kuwahudumia wafanyabiashara kwa kutumia rasilimali zilizopo na kufuatilia changamoto za wafanyabiashara wadogo.

Mhe. Dkt. Kijaji ameyasema hayo tarehe 27 Mei, 2023 katika uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) makao makuu ya Shirika jijini Dar es salaam.

"Naitaka SIDO kutengeneza mkakati wa muda mrefu na mfupi wa kuendeleza viwanda vidogo, kupanua wigo wa kuwahudumia wafanyabiashara kwa kutumia rasilimali zilizopo, kufuatilia changamoto za wafanyabiashara wadogo". Dkt. Ashatu Kijaji, (WUVB) - uzinduzi wa bodi ya SIDO. 27 Mei, 23
 

Attachments

  • FxMcZsfWYAEKaOT.jpg
    FxMcZsfWYAEKaOT.jpg
    98.4 KB · Views: 3
  • FxJcA9RXgAUfvw2.jpg
    FxJcA9RXgAUfvw2.jpg
    49 KB · Views: 3
  • FxJb_26XwAEWB3J.jpg
    FxJb_26XwAEWB3J.jpg
    55.7 KB · Views: 3
  • FxK9icyWIAQ5vvw.jpg
    FxK9icyWIAQ5vvw.jpg
    190.2 KB · Views: 3
  • FxK9jqpXwAgcyuB.jpg
    FxK9jqpXwAgcyuB.jpg
    304.9 KB · Views: 3
  • FxK9jBvXwAE8-lj.jpg
    FxK9jBvXwAE8-lj.jpg
    219.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom