Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,949
- 6,874
Atangaze nia mara ngapi? Ameisha tangazo nia hadharani. Kama vile ilivyo kwa yeye kuwa na haki ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama vile vile wananchi wana haki ya kuonyesha wasiwasi wao kuhusu yeye kushika nafasi nyeti kama hiyo. Mwanasiasa makini yeyote anajitayarisha kupambana na tuhuma zozote zitakazoelekezwa dhidi yake.Mimi sijasema lazima apewe, nimesema mwacheni atangaze nia badala ya kuanza kumpaka mavi mapema namna hii mtakuwa hamna tofauti na siasa za majitaka za ccm.
Siasa za kupakana shombo hazina tija yoyote kwa taifa na wala hazitakiwi kufanywa na chama makini kama CHADEMA.
Au mmeshaondoka kwenye hii grade ya chama makini kinachoheshimu utu wa watu kwa mujibu wa ibara yenu ya 3 ya katiba ?
Sent using Jamii Forums mobile app
Na wewe mwenyewe hutendi haki kwa kujaribu kuyafanya matamko ya mashabiki ambao hawataki hata kujulikana kuwa ndio msimamo wa Chadema. Wasemaji wa Chadema wanajulikana. Kwa vile mpaka sasa hawajasema kitu, unapata wapi ujasiri wa kukinyooshea kidole chama chao kwa maneno ya shombo yanayosemwa humu?
Amandla...