Live from EA Radio Super Breakfast: Mtangaza Nia Urais wa JMT Kupitia Chadema, Dr. Mayrose Majinge Yuko Live, Mubashara

Akiwa live kupitia line ya simu katika East Africa Radio mtia nia wa kugombea urais kupitia CHADEMA, Mayrose Majinge amesema yeye amejiunga Chadema toka mwaka 2013 hivyo sio mgeni ndani ya CHADEMA.

Pia ameahidi kuleta siasa safi na maendeleo makubwa ndani ya nchini.

Akijibu swali la mtangazaji la kwanini anaonekana anataka kugombea urais kupitia CHADEMA na huku hawajui viongozi wa Chadema je atapangaje baraza la mawaziri? Mayrose Majinge amejibu kuwa yeye hana muda wa kuclaim viongozi wa Chadema na urais ni taasisi hivyo baraza la mawaziri hilo litapangwa na taasisi ya urais na sio yeye peke yake.

Mambo yamepamba moto.
Gamba huyooo,katumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nje ya mada kidogo.
Hilo bango, kwan hiyo ndio picha nzur pekee alionayo huyu mama?Katokea ki hip hop sana yan

Ahsante
 
Mkuu una hoja ya msingi sana ila tuambiane jambo moja kwamba kabla hatujataka uhuru wa Tume kitaifa, Tengenezeni uhuru wa uchaguzi ndani ya vyama vyenu ya Kisiasi, mpaka leo kile chama kikuu cha upinzani huko Tanzania kinalalamikiwa kutokuwa huru kwenye chaguzi zake za ndani, wanachama wanalalama, wabunge wenu pia wanalalamika kwamba kiongozi ni yule yule tu. Jambo la muhimu ni wananchi kujitambua. Hata Mbowe na Chadema wangekuwa Ikulu wangesema NEC ni tume huru na CCM wangepinga! 👏👏👏👏
 
Sawa kama mwenye CCM anavyowaendesha kama vifaranga wake. Ngoja nione kama kuna mtu atatia nia ya urais!
Mbona ukilinganisha chapati kwa andazi??
Huyo Mwenyekiti wa Maisha anajijua hawezi kugombea, lakini ana fursa ya kurudisha fedha alizowekeza, ndio maana alimuomba Dr Slaa, baadae akachukua kutoka kwa EL, wakati wa CCM ni Raisi wa sasa ambaye ananafasi ya kugombea au kutogombea
 
Safari ya CHADEMA ndefu sana. Lakini najua nia yao sio kuchukua kiti cha raisi nafikiri coz huwezi kuja na mtu asiyejulikana kisiasa ikawa rahisi kuchukua nchi, chadema ilipaswa kumuandaa mtu wa hyo nafasi kwa muda mrefu na apewe airtime ili ajulikane mapema na Mambo mengine lakini Sasa hv wanachomoka na mtu hata asiyejulikana .
 
Back
Top Bottom