Live from EA Radio Super Breakfast: Mtangaza Nia Urais wa JMT Kupitia Chadema, Dr. Mayrose Majinge Yuko Live, Mubashara

Mimi sijasema lazima apewe, nimesema mwacheni atangaze nia badala ya kuanza kumpaka mavi mapema namna hii mtakuwa hamna tofauti na siasa za majitaka za ccm.

Siasa za kupakana shombo hazina tija yoyote kwa taifa na wala hazitakiwi kufanywa na chama makini kama CHADEMA.

Au mmeshaondoka kwenye hii grade ya chama makini kinachoheshimu utu wa watu kwa mujibu wa ibara yenu ya 3 ya katiba ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Atangaze nia mara ngapi? Ameisha tangazo nia hadharani. Kama vile ilivyo kwa yeye kuwa na haki ya kugombea nafasi yeyote ndani ya chama vile vile wananchi wana haki ya kuonyesha wasiwasi wao kuhusu yeye kushika nafasi nyeti kama hiyo. Mwanasiasa makini yeyote anajitayarisha kupambana na tuhuma zozote zitakazoelekezwa dhidi yake.
Na wewe mwenyewe hutendi haki kwa kujaribu kuyafanya matamko ya mashabiki ambao hawataki hata kujulikana kuwa ndio msimamo wa Chadema. Wasemaji wa Chadema wanajulikana. Kwa vile mpaka sasa hawajasema kitu, unapata wapi ujasiri wa kukinyooshea kidole chama chao kwa maneno ya shombo yanayosemwa humu?

Amandla...
 
Ndio shida ya kutanguliza ushabiki. Ni nani aliyesema asigombee? Ni kiongozi gani wa Chadema amesema asigombee. Ni wapi nimemzungumzia mtu anayeitwa kigogo? Mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi yeyote ya uongozi ( hata za ukaka mkuu) ni lazima wategemee kuulizwa maswali. Hiyo ndio demokrasia. Kwa kuulizwa maswali na kutupiwa tuhuma mapema kunampa nafasi ya kutosha ya kuyatolea maelezo kabla ya uteuzi kufanyika na kuwathibitishia wanachama wenzake kuwa hazina msingi wowote. Ni watu kama nyinyi ndio hamumtakii mema kwa kumtaka alelewe kama yai. Madongo hasa yatakuja pale atakapokuwa mgombea wa urais na kuonyesha kuwa kweli amepania kuchukua urais. Ndiyo siasa ilivyo.

Amandla...
Mkuu nisamehe kwa kuweka neno kigogo kwenye majibu yangu niliintend kumjibu retired, na wewe kwa pamoja.

Lakini hebu tujielekeze kwenye sera zake badala ya uanachama wake tu.

Haya kujadili uanachama wake na utiss wake hayana tija cause TISS siyo common enemy wa CHADEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kila mwanachama wa CHADEMA lazima apitie mateso wanayoyapitia viongozi wa juu wa chama.

Lowassa alipewa nafasi ya kugombea urais uliwahi kuona au kumsikia akipitia mateso waliyoyapitia wanachadema ?

Na wala kupitia Mateso kama mwanachama hakijawahi kuwa kigezo cha mtu kupewa nafasi ya kugombea katika CHADEMA.

Tumieni muda huu kuchambua sera zake na kuzikosoa badala ya kujikita kujadili utiss na uanachama wake wa nyuma which has nothing to do with your prosperity as a political party .

Sent using Jamii Forums mobile app
Amesema hana sera, anangoja ilani ya chama. Sasa watu wachambue nini?
Huwezi kuwazuia watu kusema ovyo. Si Chadema wala CCM wanaoweza kufanya hivyo. Na duniani kote ndivyo ilivyo. Mtu ukiwa public figure basi uwe tayari kutupiwa shombo na mashabiki ambao kwa sababu zao hawakupendi. Hali hii itaendelea hata wakati wa kampeni za kugombea urais. Akae akijua kuwa sio yeye tu atakayechafuliwa bali watu watajaribu kuiingiza hata familia yake. Yeye ajitayarishe kupambana na uozo wote huo. Ndio watu tutajua ukomavu wake.

Amandla...
 
Mkuu nisamehe kwa kuweka neno kigogo kwenye majibu yangu niliintend kumjibu retired, na wewe kwa pamoja.

Lakini hebu tujielekeze kwenye sera zake badala ya uanachama wake tu.

Haya kujadili uanachama wake na utiss wake hayana tija cause TISS siyo common enemy wa CHADEMA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna taabu Mkuu. Huyu dada hakujitendea haki. Inaelekea hakujitayarisha kabisa ukiondoa kusema tu kuwa anataka kugombea urais. Alikataa hata kuzungumzia sera zake akisema anangoja kwanza ilani ya chama chake itoke. Alitakiwa atumie nafasi aliyopewa kuufahamisha umma kwa nini anaona Rais aliyekuwepo hafai kuendelea na nafasi hiyo. Yeye kama mgombea urais anatakiwa kuendesha mjadala utakaozaa Ilani ya chama chake. Anaposema anataka kuleta siasa safi anatakiwa aeleze hiyo siasa chafu iko wapi. Kwa vile anataka kugombea urais, anatakiwa aseme kama anahusisha chama kinachotawala sasa hivi na siasa chafu. Kama hiyo siasa chafu iko ndani ya chama chake basi alitakiwa kugombea uongozi kwenye chama hicho ili akisafishe. Huyu ni Dokta, alitakiwa ajue kuwa anatakiwa kuwa convince sio tu viongozi wa chama chake bali pia wanachama, mashabiki na hata wasio wafuasi wa chama chake kuhusu uhalali wake na mabadiliko anayotaka kuwaletea katika maisha yao. Kwa vile bado ana muda, tunangoja kwa hamu maelezo yake na jinsi atakavyojinadi. Ila akae akijua kuwa kama mwanamke ana kazi ya ziada ya kufanya mpaka watu wamkubali. Na ajue tu kuwa kuna wapuuzi wengi watatumia jinsia yake kumchafua.

Hata mimi nimemsikiliza lakini niliona wazi kuwa hajajiandaa na yawezekana hata sera za chama hazielewi vizuri sana.

Nafasi aliyopewa na hiyo radio ilikuwa adhimu sana ya kumfanya ajipambanue kuwa ni mtu wa aina gani na kwanini anafaa kuchaguliwa kuwa rais.

Ngoja tuendelee kumpa muda labda atajifanyia assessment atatambua wapi kateleza na wapi arekebishe.

Ila mpaka sasa anapaswa kutengeneza team ya kumsaidia kufanya analysis ya mambo ya msingi na namna gani atajiuza kwenye media vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za tanzania tangu 2015 todate zimekuwa zinatawaliwa na shetani. Lazima kuwa macho sana na lolote CDM mlifanyalo. Huyu mama hajui lolote la machungu CDM wanayopita, leo anasema nataka kugombea urais! Nakubali aheshimiwe on the gender basis, lkn si huyu! Kuna watu wana vilema kwa kuipigania CDM, leo eti huyu mwanachama wa CCM anatakka kuwa rais kupitia CDM. Si aende CCM? CDM ndiyo ameona uchochoro? Mwanahabari Huru
 
Back
Top Bottom