Live from EA Radio Super Breakfast: Mtangaza Nia Urais wa JMT Kupitia Chadema, Dr. Mayrose Majinge Yuko Live, Mubashara

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Wanabodi,
Wenye access fuatilieni hii
IMG-20200526-WA0002.jpg

Wanabodi, kiukweli huwa nasikiza Radio asubuhi mara chache sana, niwapo njiani kwenye gari, na station ninayosikilizaga sio EA Radio, lakini leo nimeamua kuisikiliza hii Redio Redio baada tuu ya kuona hili tangazo ili nimsikie huyu dada.

Watangazaji walisema, Dr. Mayrose Majinge atakuwa live kuanzia saa 1:00 asubuhi.
Two minutes kwa Redio is a long time, wasikilizaji tumeambiwa mgeni atazungumza kuanzia saa 1:00, saa hizi tunakwenda saa 1:25 and no mention ya mgeni!, no excuse ya kuchelewa!.

Kwavile mimi nilisomea utangazaji wa Redio na kuajiriwa RTD, tulifunzwa ukitangaza kitu fulani muda fulani, huo muda ukifika bila hicho kuwepo unaomba excuse, lakini hawa watangazaji wametutangazia saa 1:00 hadi saa hizi, 25 minutes later no excuse no nothing!, ndio utangazaji gani huu?!.

Saa hizi, saa 1:28, ndio Dr. Mayrose Majinge anapigiwa na sasa yuko live, amekaribishwa, amejitambulisha kuwa amejiunga Chadema toka July 13, 2013.

Msikilize mwenyewe
Na kwa faida ya wavivu wa kusikiliza,

Swali la kwanza, mtangazaji wa kiume akamuuliza yuko Chadema toka lini?.
Huyu mtangazaji wa kiume ni kilaza fulani!, mtu amejitambulisha yuko Chadema toka lini halafu hapo hapo unamuuliza amejiunga lini Chadema!. Kiukweli hawa watangazaji vilaza wa type hizi ni majanga kwa media zetu, kutafunya sisi watangazaji wengine wote tuonekane kama vilaza fulani!.

Swali la pili, mtangazaji wa kiume, akamuuliza, ulikuwa CCM na uligombea Uenyekiti wa UWT, imekuwa tena leo uko Chadema?.
Ndio swali gani hili?.
Akajibiwa ni kweli nilikuwa CCM na kweli niligombea uenyekiti wa UWT, sasa niko Chadema.

Swali la tatu la mtangazaji wa kiume akamuuliza Waziri kivuli wa fedha ni nani?.
Dr. Mayrose Majinge akashindwa kujibu swali hili,

Mtangazaji wa kiume was patronizing this lady!, ndipo mtangazaji wa kike akaingilia kati...

Swali la 4, Mtangazaji wa kike
nini kimsukuma kugombea urais?
Jibu: Nagombea ili kuleta maendeleo makubwa kupitia siasa safi.

Swali la 5, jee Tanzania tuna siasa safi?.
Jibu ni Tanzania hatuna siasa safi, hivyo nagombea kuleta siasa safi nchini.

Swali la 6 mtangazaji wa kike, nini sera zako?
Jibu: Huu sio wakati wa kutangaza sera, hapa nimetangaza nia tuu na sio sera, sera zitatangazwa na chama kupitia ilani ya uchaguzi ya Chadema.

Swali la 7 mtangazaji wa kiume.
Kwa sasa una wadhifa gani Chadema?.
Jibu: Sina wadhifa wowote ni mwanachama wa kawaida.

Swali la 8, sasa wewe huna cheo chochote Chadema, unataka kugombea urais wakati hujui hata Waziri kivuli wa fedha?, utawezaje kuwa rais?.
Again this is patronizing question!.
Jibu: sio simjui bali sitaki kumchanganya kutokana na kuwa busy na maandalizi haya!. Urais ni Taasisi, kazi ya urais sio ku crame majina ya viongozi bali ni utekelezaji wa pamoja.

Thats a lame excuse!.

Mtangazaji wa kiume aliendelea kukomaa nae, mtangazaji wa kike akamkatisha kuwa tutaendea baadaye.

Hiyo baadae ilipofika, Studio akaingia Mtulia, Mbunge wa Kinondoni.
Nami nikahama station.
Nimeisha hapa, asante kufuatilia.

Paskali
Rejea
Uenyekiti wa UWT: Ni Vita Kati ya Ukweli na Ubatili! - JamiiForums
Mwanamke ajitokeza kuwania Urais kupitia CHADEMA. Ni Msomi, Mwanamke wa Shoka, Ana uwezo na Jembe Kweli, ila... - JamiiForums

Akiwa live kupitia line ya simu katika East Africa Radio mtia nia wa kugombea urais kupitia CHADEMA, Mayrose Majinge amesema yeye amejiunga Chadema toka mwaka 2013 hivyo sio mgeni ndani ya CHADEMA.

Pia ameahidi kuleta siasa safi na maendeleo makubwa ndani ya nchini.

Akijibu swali la mtangazaji la kwanini anaonekana anataka kugombea urais kupitia CHADEMA na huku hawajui viongozi wa Chadema je atapangaje baraza la mawaziri? Mayrose Majinge amejibu kuwa yeye hana muda wa kuclaim viongozi wa Chadema na urais ni taasisi hivyo baraza la mawaziri hilo litapangwa na taasisi ya urais na sio yeye peke yake.

Mambo yamepamba moto.
Karibu pande hizi.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Wanabodi, kiukweli huwa nasikiza Radio asubuhi mara chache sana, niwapo njiani kwenye gari, na station ninayosikilizaga sio EA Radio, lakini leo nimeamua kuisikiliza hii Redio Redio baada tuu ya kuona hili tangazo ili nimsikie huyu dada.

Watangazaji walisema, Dr. Mayrose Majinge atakuwa live kuanzia saa 1:00 asubuhi.
Two minutes kwa Redio is a long time, wasikilizaji tumeambiwa mgeni atazungumza kuanzia saa 1:00, saa hizi tunakwenda saa 1:25 and no mention ya mgeni!, no excuse ya kuchelewa!.

Kwavile mimi nilisomea utangazaji wa Redio na kuajiriwa RTD, tulifunzwa ukitangaza kitu fulani muda fulani, huo muda ukifika bila hicho kuwepo unaomba excuse.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Dr. Mayrose Majinge sasa yuko live, amekaribishwa, amejitambulisha kuwa amejiunga Chadema toka July 13, 2013.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Swali la kwanza, mtangazaji wa kiume akamuuliza yuko Chadema toka lini?.
Huyu mtangazaji wa kiume ni kilaza fulani!, mtu amejitambulisha yuko Chadema toka lini halafu hapo hapo unamuuliza amejiunga lini Chadema!.

Kiukweli hawa watangazaji vilaza wa type hizi ni majanga kwa media zetu, kutafunya sisi watangazaji wengine wote tuonekane kama vilaza fulani!.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Swali la pili, mtangazaji wa kiume, akamuuliza, ulikuwa CCM na uligombea Uenyekiti wa UWT, imekuwa tena leo uko Chadema?.
Ndio swali gani hili?.

Akajibiwa ni kweli nilikuwa CCM na kweli niligombea uenyekiti wa UWT, sasa niko Chadema.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Swali la tatu la mtangazaji wa kiume akamuuliza Waziri kivuli wa fedha ni nani?.
Dr. Mayrose Majinge akashindwa kujibu swali hili,

Mtangazaji wa kiume was patronizing this lady!, ndipo mtangazaji wa kike akaingilia kati...
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Swali la 4, Mtangazaji wa kike
nini kimsukuma kugombea urais?
Jibu: Nagombea ili kuleta maendeleo makubwa kupitia siasa safi.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,286
2,000
Swali la 5, jee Tanzania tuna siasa safi?.
Jibu ni Tanzania hatuna siasa safi, hivyo nagombea kuleta siasa safi nchini.
P
 
Ngorunde

JF-Expert Member
Nov 17, 2006
1,916
2,000
Huku ni kukua kwa demokirasia ndani ya chama.
Ila avae ngozi ya chuma..vijembe vitakuwa vikali haswa.
Utasikia, pandikizi la sisiem, mara ametumwa na wapinzani wa mwanaume huru n.k n.k.

Hongera mama kwa kuonyesha njia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom