Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Mzee Mwanakiji anataka kutuchanganya kwa kudai Kuhani aseme lini Mwalimu alitamka "ninang'atuka........" Hicho unachosema, ndicho anachokisema Kuhani!

Amandla.........

Mwanakijiji kumtaka, kumuomba, au kumdai Kuhani aseme lini Mwalimu alitamka maneno hayo si kutuchanganya bali ni katika juhudi za kutafuta ukweli tu. Sioni ubaya wowote hapo na mimi sijachanganywa na kitu hapo.

Labda wewe ndiye umechanganywa lakini kusema "kutuchanganya" ni kupotosha kwani hilo ni neno la uwingi unless na wewe uwataje watu wote walichanganywa na ombi la Mwanakijiji kama watu hao watakuwa wamekukubalia wewe uwe msemaje au mwakilishi wa mawazo au maoni yao.
 
Kwa hiyo tatizo ni mimi kutumia neno kutuchanganya? Mimi nilikuwa naamanisha anatuchanganya, mimi, mke wangu na wajukuu zangu, ambao wote ni membaz humu. Sasa kwa nini nisitumie wingi?

Au inakuuma kuwa upande mmoja na Kuhani?

Amandla........
 
Last edited:
- Kwa hiyo inaweza kusemekana hakuyasema pia, au?

FMES!

Kusema aliyasema lakini inawezekana sio kwenye siku hiyo niliyoitaja maana nimeenda kwengine nikakuta inadaiwa kuwa yalisemwa Agosti mwaka 1990, Diamond Jubilee. Lakini cha uhakika ni kuwa alisema kabla ya kung'atuka mwaka 1990. Naamini kuwa hoja msingi hapa ilikuwa ni kama Malecela alikuwa sahihi aliposema kuwa aling'atuka mwaka 1992 au la. Hili la alitamka lini si la msingi. Ni vizuri kupata uhakika lakini jibu la hoja msingi limeishapatikana. Malecela alikosea.

Amandla......
 
Tulichokiona ni kuwa haiwezekani kuwa Mwalimu aliyasema haya maneno mwaka 1992 kama anavyodai Malecela.

Yawezekana mmeona hivyo; kwani kuona hivyo hakuhusiani na ukweli halisi. Binafsi sioni sababu kwanini yasiwe yamesemwa kama alivyosema Malecela?

Kwa hiyo kama alidai hivyo alikosea. Inasemekana kuwa maneno haya yalitamkwa Agosti 1985 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amandla.........

Huwezi kusema kuwa alikuwa amekosea kama huna uhakika yalisemwa lini. Haijalisi kama 'Inasemekana au haisemekani'. Maneno hayo yalisemwa at a certain point in time... ni lini? Majibu ya "nadhania, sijui, nafikiri, inadaiwa" hayakubaliki.
 
Sijaona mahali ambapo Kuhani anasema maneno ya "mimi nang'atuka" yalitolewa lini?!

Unadhani, Mwanakijiji, Nyerere angeweza kung'atuka 1985 na 1990 halafu 1992 ndio akaja kusema "nang'atuka," miaka saba baadae? Miwili baadae? Jamani, hizi obfuscation za mada ndio haya ya kombe la mbuzi sasa!

i300_NANGATUKA.JPG

Mimi sijawahi hata kuingia kwenye ukumbi wa NEC kuona huo ukuta ambao Mzee Malecela anauona kiiiila mara. I mean, Mzee Malecela kaanza kuingia kwenye huo ukumbi toka enzi za gharika ya Nuhu. Nyerere aling'atuka na kusema nang'atuka Agosti, 1990. Period.Anakuwa loose with facts, anawaambia "vijana" wa vyombo vya habari "ngoja niwaambie, Baba wa Taifa alisema mwaka 1992 nang'atuka lakini CCM..." Mzee please!

Halafu Malecela akatoa hoja ya jinsi binadamu tunavyo tafsiri mambo tofauti akitumia mfano wa kisayansi kwamba "Malecela anaweza akavaa shati jeusi halafu mtu ambae ni color blind akaliona ni dark blue." Well, angekuwa sehemu zilizoendelea ki information angeandikiwa barua na viwanafunzi vya darasa la tatu vya physics kwamba mtu color blind maana yake ana matatizo ya kutofautisha na hata kuonga rangi. Shati jeusi katika physics maana yake halitoi miale ya rangi yeyote ile, kwa hiyo cones za retina ya jicho haziwezi ku respond kwa weusi, uwe mzima au uwe color blind, nyeusi ni nyeusi tu!

Lakini physics sio profession yake, japo kajiingiza. Profession yake ni siasa. Mbele ya national audience kwa nini anakuwa loose with facts kuhusu mlezi wake wa kisiasa? Malecela should know better.
i296_Malecela.jpg
 
Huwezi kusema kuwa alikuwa amekosea kama huna uhakika yalisemwa lini. Haijalisi kama 'Inasemekana au haisemekani'. Maneno hayo yalisemwa at a certain point in time... ni lini? Majibu ya "nadhania, sijui, nafikiri, inadaiwa" hayakubaliki.

Mbona unataka ku-split hairs. Tunachojiuliza hapa ni maneno haya yalisemwa lini, kati ya mwaka 1990 au 1985. Sasa kwa nini nisisema huyo aliyedai kuwa yalisemwa mwaka 1992 alikosea? Au unataka kusema hata mimi nikidai kuwa yalisemwa mwaka 2008 siwezi kukosolewa kwa sababu tu hatuna uhakika wa tarehe? Kinachojulikana ni kuwa haiwezekani kuwa aliyasema maneno haya baada ya 1990 maana aliishang'atuka. Mbona unang'ang'ania non-issue?

Amandla...........
 
Kwa hiyo, Mwanakijiji, Nyerere angeweza kung'atuka 1985 na 1990 halafu akaja kusema "mimi nang'atuka" miaka saba baadae, miaka miwili baadae? Jamani, hizi obfuscation za mada ndio haya ya kombe la mbuzi sasa!

i300_NANGATUKA.JPG

Mimi sijawahi hata kuingia kwenye ukumbi wa NEC kuona huo ukuta ambao Mzee Malecela anauona kiiiila mara. I mean, Mzee Malecela kaanza kuingia kwenye huo ukumbi toka enzi za gharika ya Nuhu. Anakuwa loose with facts, anawaambia "vijana" wa vyombo vya habari "ngoja niwaambie, Baba wa Taifa alisema mwaka 1992 nang'atuka lakini CCM..." Mzee please! Nyerere aling'atuka na kusema nang'atuka Agosti, 1990. Period.

Halafu akatoa hoja ya jinsi binadamu tunavyo tafsiri mambo tofauti akitumia mfano wa kisayansi kwamba "Malecela anaweza akavaa shati jeusi halafu mtu ambae ni color blind akaliona ni dark blue." Well, angekuwa sehemu zilizoendelea ki information angeandikiwa barua na viwanafunzi vya darasa la tatu vya physics kwamba mtu color blind maana yake ana matatizo ya kutofautisha na hata kuonga rangi. Shati jeusi katika physics maana yake halitoi miale ya rangi yeyote ile, kwa hiyo cones za retina ya jicho haziwezi ku respond kwa weusi, uwe mzima au uwe color blind, nyeusi ni nyeusi tu!

Lakini physics sio profession yake, japo kajiingiza. Profession yake ni siasa. Mbele ya national audience kwa nini anakuwa loose with facts kuhusu mlezi wake wa kisiasa? Malecela should know better.
i296_Malecela.jpg

sasa hili lilikuwa na ugumu gani!? Angalau mmeanza kufanya homework siyo mnabisha tu!
 
Kwa hiyo tatizo ni mimi kutumia neno kutuchanganya? Mimi nilikuwa naamanisha anatuchanganya, mimi, mke wangu na wajukuu zangu, ambao wote ni membaz humu. Sasa kwa nini nisitumie wingi?

Au inakuuma kuwa upande mmoja na Kuhani?

Amandla........

Kama ni wewe na familia yako basi nimekuelewa. Nilikuwa nataka clarity tu.

Na hainiumi mimi kuwa upande mmoja na Kuhani. Mimi sio anti-Kuhani wala anti Mchundo. Niko upande wa facts. Na wewe ukiwa upande wa facts nitakuwa upande wako.
 
Kama Mwalimu aliyasema maneno hayo 1990,basi atakuwa aliyasema mara mbili,nina uhakika alisema kuwa anang'atuka mwaka 1985.
 
- Alishawahi kuyatamka tena mwaka 1982, pale kwenye bunge la zamani Karimjee Hall.

FMES!

Nashukuru kwa info hiyo FEMS,siwezi kubisha kabisa kwasababu hata mimi nakumbuka aliposema neno hilo mwaka 1985,sasa ni wazi alishasema zaidi a mara moja kwani inaonyesha kuna udhibitisho aliyasema maneno hayo mwaka 1990 respectively....Kuhusu 1992 vile vile sina uhakika nalo.
 
Alishawahi kuyatamka tena mwaka 1982, pale kwenye bunge la zamani Karimjee Hall.

FMES!

FMES,

Hebu nisaidie hapo kama sijakuelewa vizuri.

Unasema Nyerere "alitamka tena mwaka 1982" Karimjee Hall kwamba anang'atuka?

Halafu akasubiri mpaka miaka nane baada ya kutoa ahadi? Miaka mitatu baadae? Ndio akaja kung'atuka?

See, this is one of those cases where sijui na sisemi umekosea, ila naona kama mantiki ya kilichosemwa haijakaa sawa. Au?
 
FMES,

Hebu nisaidie hapo kama sijakuelewa vizuri.

Unasema Nyerere "alitamka tena mwaka 1982" Karimjee Hall kwamba anang'atuka?

Halafu akasubiri mpaka miaka nane baada ya kutoa ahadi? Miaka mitatu baadae?

- Mwalimu alianza kuongelea kpumzika urais siku nyingi sana toka in mwishoni mwa 70s, sioni tatizo lolote na yeye kusubiri mpaka 1985 kutimiza nadhiri yake bila ya kufukuzwa na mtu, binfasi ninamuheshimu sana kwa hili, pamoja na kwamba I do not like the way he did it hasa alipoanza ku-determine who should replace him na kutuletea matatizo makubwa sana as a nation mpaka leo,

- Lakini bado naheshimu nia yake ya kupumzika na kuitimiza, kabla ya muda mrefu sana kupita.

Thanxs!
 
Kwa hiyo, Mwanakijiji, Nyerere angeweza kung'atuka 1985 na 1990 halafu akaja kusema "mimi nang'atuka" miaka saba baadae, miaka miwili baadae? Jamani, hizi obfuscation za mada ndio haya ya kombe la mbuzi sasa!

i300_NANGATUKA.JPG

Mimi sijawahi hata kuingia kwenye ukumbi wa NEC kuona huo ukuta ambao Mzee Malecela anauona kiiiila mara. I mean, Mzee Malecela kaanza kuingia kwenye huo ukumbi toka enzi za gharika ya Nuhu. Nyerere aling'atuka na kusema nang'atuka Agosti, 1990. Period.Anakuwa loose with facts, anawaambia "vijana" wa vyombo vya habari "ngoja niwaambie, Baba wa Taifa alisema mwaka 1992 nang'atuka lakini CCM..." Mzee please!

Halafu Malecela akatoa hoja ya jinsi binadamu tunavyo tafsiri mambo tofauti akitumia mfano wa kisayansi kwamba "Malecela anaweza akavaa shati jeusi halafu mtu ambae ni color blind akaliona ni dark blue." Well, angekuwa sehemu zilizoendelea ki information angeandikiwa barua na viwanafunzi vya darasa la tatu vya physics kwamba mtu color blind maana yake ana matatizo ya kutofautisha na hata kuonga rangi. Shati jeusi katika physics maana yake halitoi miale ya rangi yeyote ile, kwa hiyo cones za retina ya jicho haziwezi ku respond kwa weusi, uwe mzima au uwe color blind, nyeusi ni nyeusi tu!

Lakini physics sio profession yake, japo kajiingiza. Profession yake ni siasa. Mbele ya national audience kwa nini anakuwa loose with facts kuhusu mlezi wake wa kisiasa? Malecela should know better.

i296_Malecela.jpg

Mkuu tatizo la color blind ambalo ni genetic,asilimia kubwa ya waathirika majority ni wale wa Red/green color blindness ambayo ni common na inajulikana pia kama deuteranopia....Most of the time huwapata wanaume,hata hivyo back kwenye mfano wa Dk Malecela alipotumia mfano wa blue,tusisahahu pia kuna blue color blindness (protanopia) which is an inability to distinguish both blue and yellow, which are seen as white or gray,so nadhani labda angesema white or grey based on the protanomia condition,hata hivyo inaonyesha alizumgumzia tu kuhusu rangi bila kwenda kisayansi zaidi....Nakubaliana na wewe hapo kwenye kuhusu black kwani tatizo la color blindness hali affect blackness kwasababu haina maana kwamba unamiss cones kwani only ukiwa na rods peke yake then unaweza kuona only in black and white na ukiwa color blind haimaanishi kuwa una miss cones na hivyo nakubaliana kuwa black is always black whether you're color blind or not....Tuendelee kuelemishana.
 
Last edited:
Unapokuwa kwenye mahojiano, facts kama za miaka na mahali zinaweza kukutoka. Na hicho ni kitu kinachokubalika iwapo tu miaka na mahali sio agenda za mahojiano yenyewe bali ni kichapizo tu.

Mnategemea Mzee Malecela akiwa kwenye mahojiano, akumbuke mahali na mwaka kwa usahii kabisa kama vile anakwenda kwenye mtihani wa historia wa darasa la nne.

Nyie watu wazima mnashindwa kujadili theme ya kile alichosema na mnabaki kubishana kwenye miaka. Angesema mwaka 1990, mantiki ingebaki hilehile.
 
Mkuu tatizo la color blind ambalo ni genetic,asilimia kubwa ya waathirika majority ni wale wa Red/green color blindness ambayo ni common na inajulikana pia kama deuteranopia....Most of the time huwapata wanaume,hata hivyo back kwenye mfano wa Dk Malecela alipotumia mfano wa blue,tusisahahu pia kuna blue color blindness (protanopia) which is an inability to distinguish both blue and yellow, which are seen as white or gray,so nadhani labda angesema white or grey based on the protanomia condition,hata hivyo inaonyesha alizumgumzia tu kuhusu rangi bila kwenda kisayansi zaidi....Tuendelee kuelemishana.

JMushi,

Tusiwabughudhi wengine.

Twende kwenye jamvi la sayansi tukaeleweshane.
 
Back
Top Bottom