Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Mar 25, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Mar 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kuna mjadala unaendelea na nimeonelea ni vema kuanzisha mwingine ambao itaenda sambamba (baadae kuunganishwa) nikiambatanisha Audio version ya alichokiongea Mzee Malecela tarehe 25 Machi 2009. Hapa ni JamiiForums Listening Audio Booth (J-LAB)

  Sikiliza kwa kubonyeza alama ya kucheza moja kwa moja:

  [mp3]http://www.jambovideos.com/mahojiano/JM_PC_March.mp3[/mp3]
   
  Last edited by a moderator: Mar 26, 2009
 2. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi kweli Hon. RA anasikiliza vitu kama hivi??
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 25, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mmmhh...huyu kweli mkereketwa. Raisi anafanya kazi "nzuri" kweli? Wow...
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mmmh Ze oriniginale comedy... Charger ya Laptop inaisha... Bora nisubiri umeme urudi... Ha ha ha haaaaaaaaaaa
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hakika nitamjibu!
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Thanks Invisble kwa audio. Nimemsikililiza huyu Mzee, na sikubaliani naye kabisa kabisa. Huyu Mzee bado anaishi miaka ya 70 & 80. Halafu anaweka chama chake mbele ya nchi.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa kama yeye anasema wanaolumbana wamalizane kwenye vyombo husika i.e. Chama n.k. na siyo kwenye vyombo vya habari kwa nini yeye asingesema hayo kwenye kikao cha chama chake hadi kuitisha mkutano na wanahabari wa kutoka kwenye vyombo vya habari na kusema wanaolumbana wasilumbane kwenye vyombo vya habari? What the hell?
   
 8. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee kaboa from the getgo didnt even bother listen till the end!! Seems CCM is more important to him than Tanzanians...He needs to retire from politics..wakati wake umepita!!
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Uzee unamwingia haraka..he can not argue out of box of CCM!!

  Uhuru wa vyombo vya habari na kuutumia kwa faida ya taifa je haoni hili?

  Ufisadi CCM yeye amekuwepo miaka yote hiyo..je haoni mchango wa vyombo vya habari?
   
 10. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkulu Invisible, nimekubali kama ilivyotabiliwa kwenye thread ya mwanzo kuwa malecela anaweza kuja kuzima au kutoa mwelekeo feki basi ndivyo mambo yalivyo. Kwanza inaonyesha hakubaliani na habali za ufisadi maana anasema ''kama kuna mafisadi basi ndio hao waliokwisha fikishwa mahakamani....'' Kuhusu Chenge kuendelea kushika nyazifa anasema ''Chenge ni mtuhumiwa bado haijathibitika.....'' swali...Mramba kashahukumiwa? maana wanataka kutoa sahihi yake kwenye pesa ya TZ kwa kuwa ni fisadi...''

  Msimamo wa Malecela ni kupiga bit vyombo vyahabali kuachana na jitihada zilizosaidia kufichua uovu wa CCM. Msisitizo mkubwa kauweka kwenye swala la kumegeka kwa chama na hakutaka kutolewa nje ya mstari huo kila alipoulizwa maswali. Naona anataka hatua zichukuliwe kufuta baadhi ya magazeti akidai hayana cha kuandika na kuwa sihi waTZ kuacha kuyanunua. Kakiri udhaifu wa serikali kutotoa tamko juu ya malumbano yanayoendelea.

  Wandishi wahabali wamemuuliza maswali mazuri lakini walionekana kuwa na nidhamu ya woga kidogo isipokuwa Kubenea. Nadhani walitakiwa kupewa kama saa moja hivi kwaajiri ya maswali na majibu tu ili tumuone nae anavyojikanyaga.

  Hatahivyo, moto ni ule ule wapiganaji kila mtu kwa nafasi yake tukaze buti. Hakuna jipya Malecela ni wale wale. Imenihuzunisha kutumia umri na uzoefu wake katika siasa kutupiga politic zisizokuwa na msingi na kuponda vyama vingi
   
 11. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Asijekurithisha tu huo ubunge kuendeleza libeneke.
   
 12. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu tumbukiza na swala la ukomo wa wabunge kwenye makala yako. Naona watu wanafanya siasa kama ajira ya kuzeekea ndio matatizo yake hayo wanatumia uzee wao kuwapiga politic vijana
   
 13. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  We are giving too much attention to expired leaders who have long lost touch with the people.

  How many Tanzanian think that Kikwete is doing the heck of a good job?

  P'se Get this promiscuous Malecela out of here, he doesnt represent the way I feel about my lackluster president, and neither is any of my very long extended familly.
   
 14. K

  Koba JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  .....seems kwake wanaotakiwa kujadili haya matatizo kwake ni vyombo vitatu tuu serikali,chama cha mafisadi na viongozi wenzake...watu wanataka justice yeye anaita malumbano na nani kamwambia wanachi wanavurugwa na hizi debate...nawashauri tuendelee na hizi debate maana ndio zimefichua mengi kuliko bunge lao la mafisadi!
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  % kubwa ya ufisadi umeibuliwa na Vyombo vya habari ndo akina Slaa wakapenyezewa!

  Anaubeza mchango wa vyombo vya habari wakati yeye anatumia vyombo hivyo hivyo kutoa dukuduku!

  Kwa nini hakusubiri Bunge au akatumia chama?
   
 16. p

  p53 JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyu mzee kweli ni tingatinga la ccm.duh siamini nilichokisikia..
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu, Malecela anazungumza kama makamu mwenyekiti wa CCM, ni muhimu sisi tuifahamu lugha yake kwanza...Huyu sii kiongozi wa serikali na hana nguvu huko..
  Pili, alichosema ni ukweli mtupu.. kwani kama kweli hawa jamaa wanaotaka kumeguka CCM watoke! hizi habari za kutuzuga hata sisai wananchi hatufahamu wanachosimamia ni kutuzidishia hasira tu.. Waondoke CCM, wananchi tujue moja kama ni hao Mafisadi wanatishia kuondoka waondoke.. na kama kuna wale wanaojiona wasafi na CCM sio mahala pao - waondoke...
  Jamani ndilo sisi wananchi tunachotaka kuona na tunatarajia mtu yeyote mwenye kujali maslahi ya Taifa atakuwa amechukua maamuzi ya maana isipokuwa wale wanaotaka kutubeza..sio kuitisha vikao kila siku kujitangaza wajkati bado wamo ndani ya chungu wakipikwa..
   
 18. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mzee Malecela nafikiri ni mlolongo wa vinara wa CCM waliotumwa na Mwnyekiti ili kumfagilia njia kutokana na kugubikwa na skandali kila kukicha, ambapo ni wenzake ndani ya CCM ambao wamejitokeza kumkosoa.

  Ingawa nashindwa kujua kwa nini waandishi wa habari hawakumuuliza kuwa kama yeye Malecela ameona vyombo vya habari ni muhimu katika kutuma ujumbe wake badala ya vikao vya Chama au Bunge, kwa nini anawakataza wengine kuvitumia hivyo hivyo vyombo vya habari kujisafisha??. Kwa kiasi fulani waandishi walishindwa kumbana huyu mzee.:mad:

  Ila kwenye aliyoeleza, hapa nimeona alitumwa kufanikisha mambo matatu yafuatayo;
  1. Kuvionya vyombo vya habari kuwa sasa viko karibu vitafungiwa kwa kuandika wasiyoyapenda wakuu.
  2. Badala yake wanataka, vyombo vya habari vimsaidie raisi (yaani vimpambe), na moja kati ya mapambo ni kuwa viwahabarishe wananchi na wafadhili kuwa tayari mafisadi wameshachukuliwa hatua na JK.
  3. Lakini kubwa zaidi ni kuwa Mzee Malecela pia alitumwa kumpiga mkwara Dr. Mwakyembe na wenzake (Prof. Mwandosya n.k) ambao inaelekea wana nia ya kumpinga Kikwete in 2010. Hili ameliweka wazi kwamba Kikwete atakuwepo hadi 2015 na akina Mwandosya ni vema tu wakatumia vipesa vyao kwengine maana hawataweza kupambana na BOT ya Kikwete.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,587
  Likes Received: 82,207
  Trophy Points: 280
  Mkandara, tumeshaambiwa kwamba CCM ina utamaduni wake wa kumuachia Rais akae madarakani awamu mbili. Huu utamaduni ni wa ajabu sana wala haukuzingatia kabisa maslahi ya Taifa. Rais aliye madarakani anavurunda kila kukicha lakini kwa kuwa chama chake kina utamaduni wa kuhakikisha anakaa madaraka kwa awamu mbili basi Watanzania tunyamaze tu na kumuacha jamaa akiendelea kutuburuza na udhaifu wake katika nyanja zote za uongozi hadi 2015!!! Ama kweli CCM imeshika utamu :(!!!!! Mungu inusuru nchi yetu
   
 20. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kama anazungumza kama mwenyekiti wa CCM, je ni sawa alivyozungumzia mambo ya chama nyumbani kwake Sea View?

  Je Makamu Mwenyekiti wa CCM hana ofisi? Nini kilichomzuia kuzungumza ofisini kwake?


  Nakumbuka Mrs Malecela wiki iliyopita alizushiwa press conference ambayo hakuwa aware nayo na akaahidi kuongea na waandishi wa habari siku za usoni.

  Je mkutano na waandishi wa habari alioahidi Mrs Malecela ndio huu ? au Mrs Malecela ni tofauti na muda wake haujawadia?
   
Loading...