Listening Audio Booth:John Malecela: Alichoongea

Kama Malecela ameona vyombo vya habari ni muhimu katika kutuma ujumbe wake, kwa nini anawakataza wengine kuvitumia hivyo hivyo vyombo vya habari kujisafisha??. :mad:

Hapa nimeona alitumwa kufanikisha mambo matatu yafuatayo;
  1. Kuvionya vyombo vya habari kuwa sasa viko karibu vitafungiwa kwa kuandika wasiyoyapenda wakuu.
  2. Badala yake wanataka, vyombo vya habari vimsaidie raisi (yaani vimpambe), na moja kati ya mapambo ni kuwa viwahabarishe wananchi na wafadhili kuwa tayari mafisadi wameshachukuliwa hatua na JK.
  3. Lakini kubwa zaidi ni kuwa Mzee Malecela pia alitumwa kumpiga mkwara Dr. Mwakyembe na wenzake (Prof. Mwandosya n.k) ambao inaelekea wana nia ya kumpinga Kikwete in 2010. Hili ameliweka wazi kwamba Kikwete atakuwepo hadi 2015 na akina Mwandosya ni vema tu wakatumia vipesa vyao kwengine maana hawataweza kupambana na BOT ya Kikwete.

mkuu analysis yako ina kaukweli haya hicho kipengele cha 3..
 
Sababu kubwa ya Press Conference ya Mzee Malecela sio Malumbano ya Viongozi wa CCM.CCM walikuwa na nafasi ya kujadili malumbano hayo katika vikao vya Ndani vya CCM.....Message aliyokuwa anataka kuitoa Dr.Malecela ni kwamba""Mwanachama yeyote wa CCM asithubutu kufikiria kugombea Urais 2010,nafasi hiyo bado ni ya Kikwete,ni utaratibu wa CCM kumuacha Rais amalizie vipindi vyote viwili""Message hiyo Dr Malecela ameipa msisitizo.

Kuna fununu kuwa kuna baadhi ya WanaCCM wanataka kumshinikiza JK asigombee tena katika kipindi kijacho...JK ni mdhaifu kukiwa na kelele nyingi za namna hiyo,kwa hiyari yake mwenyewe anaweza kusema "Mimi sasa basi!! Mwanachama mwingine mwenye uwezo aendeleze kazi hii"...Dr Malecela analijua hilo...ameamua kwa makusudi kuchukua nafasi ya kufanya campaign ya kuwatia Uoga wanaoshinikiza kumuondoa Kikwete,Kazi ndio imeanza.Maneno ya Dr Malecela yatakuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari Tanzania...

Ningependa na kufurahi kama kuna Mwanahabari ambaye angemuomba Mzee Malecela sasa apumzike Ubunge wa Mtera....kwa miaka 75+ kuweza kwenda kasi na maendeleo ya Jimbo si rahisi,lakini kwa maelezo yake inaonekana bado atagombea Ubunge huko Mtera!
 
Mzee Malecela anasema kuwa kwenye ukumbi wa NEC kuna maneno ya Baba wa Taifa yanasema "mimi ninang'atuka lakini naendelea kuamini bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba...."

Halafu anaendelea kusema mwaka 1992 wakati wakipitisha ripoti ya Nyalali kuruhusu vyama vyingi wakati yeye ni Waziri Mkuu "ndipo Baba wa Taifa alisema maneno haya."

Nyerere aling'atuka lini na vyama vingi viliruhusiwa lini? Malecela, of all the people, asiwe loose na hizi facts.

i296_Malecela.jpg"
 
Unataka kutwambia kuwa swali aliloulizwa kuhusu yeye kugombea uRais 2010 alipanga na huyo mwandishi. Manake Malecela hakuja kwa huo mkutano na kulizungumzia hilo, bali kalizungumza baada ya kuulizwa.

Nikija kwa Malecela, alichozungumza ni haki yake. Ila jamaa ni mwanasiasa jasiri, kapitia vipindi vigumu sana ila bado CCM anaipa kipaumbele mno yote ni ktk kulinda maslahi, nadhani anaelekea kuchukua nafasi ya Kawawa. Manake Kawawa kila atakachozungumza atataja Chama (CCM).
 
Malechela, anasahau kwamba hiyo mifumo ya chama na serikali haiko imara, IMELEGEA, IMEFITINIKA.ANALIJUIA HILO. Mifumo Haiaminiki!! na ndiyo maana watu wanalumbana. kwa kuita press conference naye anaendeleza malumbano. NI UZANDIKI ULE ULE. ASIJIDANGANYE KWAMBA CCM NI IMARA KAMA ILE YA ENZI ZILE.

Kuhusu Chenge kutuhumiwa, anajaribu kutumia weledi wa lugha wa enzi zile kulinda,na kutetea vitu vya hovyo, ANASAHAU MZEE WETU KWAMBA MTUHUMIWA, WA WIZI WA NG'OMBE HATA MMOJA TU, ANAKUWA LUPANGO, NA SIO NYUMBANI KWAKE.sembuse kiongozi anayetuhumiwa kukosa maadili, bado ni kiongozi wa kamati ya maadili (mjumbe).

ahsante,
 
This old man is finished. I cant believe after so many decades as a parliamentarian, he dares suggest that the constitutionally provided for election every 5years is just a matter of Protocol and is done basi tuu kama kujaza mafuta gari ikiwa njiani lakini de facto Kikwete president mpaka 2015. Although I recognize this to be a fact, to give authenticity to it is a shame. It should occur because there is no opposition! Lakini sio kwasababu ndio 'tradition' kama antavyotaka iwe huyu mzee. He is living in the past.
 
zingine zoooote zilikuwa ni blah blah blah.......one msg...JK kuendelea kuwa Rais mpaka 2015.
Ujumbe mwingine ni kuwa sasa JK yuko na CCM yenyewe.......CCM Mtandao kama bado walikuwa wako kwenye dreams zao..........kalaghabao
 
Nimefurahi sana kwa Mzee Malecela kuwakumbusha wana-CCM kuwa chama kina utaratibu wake wa kushughulikia mambo.

Huu ujumbe ni muhimu kwa wanasiasa wachanga ambao hawaelewi vizuri umuhimu wa utaratibu huu.

Chama Cha Mapinduzi hakifanyi mambo kiholela-holela bali issues zote ni lazima ziongelewe kwenye vikao halali na ndipo maamuzi ya Chama hutolewa. Baada ya hapo huwa ni utekelezaji tu hata kama hukufurahia maamuzi hayo.

Kinyume cha hapo basi labda mwanasiasa husika ni mgeni na chama na atatakiwa ajifunze mengi.

Haiwezekani hata siku moja watoto wa nyumba moja mnagombana halafu mnakwenda katikati ya mtaa mkirushiana maneno, haikubaliki, ni lazima wazee watatoka ndani na kuwakemea.

Kwangu mimi nadhani inatosha, hawa wanaolumbana wamesikia kama hawawezi basi 'WAMEGUKE'

I love CCM
 
Sababu kubwa ya Press Conference ya Mzee Malecela sio Malumbano ya Viongozi wa CCM.CCM walikuwa na nafasi ya kujadili malumbano hayo katika vikao vya Ndani vya CCM.....Message aliyokuwa anataka kuitoa Dr.Malecela ni kwamba""Mwanachama yeyote wa CCM asithubutu kufikiria kugombea Urais 2010,nafasi hiyo bado ni ya Kikwete,ni utaratibu wa CCM kumuacha Rais amalizie vipindi vyote viwili""Message hiyo Dr Malecela ameipa msisitizo.

Kuna fununu kuwa kuna baadhi ya WanaCCM wanataka kumshinikiza JK asigombee tena katika kipindi kijacho...JK ni mdhaifu kukiwa na kelele nyingi za namna hiyo,kwa hiyari yake mwenyewe anaweza kusema "Mimi sasa basi!! Mwanachama mwingine mwenye uwezo aendeleze kazi hii"...Dr Malecela analijua hilo...ameamua kwa makusudi kuchukua nafasi ya kufanya campaign ya kuwatia Uoga wanaoshinikiza kumuondoa Kikwete,Kazi ndio imeanza.Maneno ya Dr Malecela yatakuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari Tanzania...

Ningependa na kufurahi kama kuna Mwanahabari ambaye angemuomba Mzee Malecela sasa apumzike Ubunge wa Mtera....kwa miaka 75+ kuweza kwenda kasi na maendeleo ya Jimbo si rahisi,lakini kwa maelezo yake inaonekana bado atagombea Ubunge huko Mtera!

Duh, Mkuu Mwawado,

Nadhani kama si hii teknolojia kuendelea kwa kiasi tulipofikia leo basi ningeweza walau kuamini maneno yako japo kwa asilimia hamsini.

Lakini tumemsikia Mzee Malecela akiongea na kusisitiza sababu ya press conference ni kuwasihi wanaolumbana waache kufanya hivyo na zaidi akasisitiza vyombo vya habari na waandishi wazingatie kufanya kazi zao kwa maslahi ya taifa na si vinginevyo.

Sasa hizo quotes zako zimetoka kwenye clip nyingine au ni hii tuliyowekewa hapa? Au tumeshakuwa mabingwa wa malumbano kiasi cha kwamba hatutaki kusema ukweli na tunatafuta vichochezi?

Tujadili kauli yake kama alivyoongea na wala tusijena mawazo yetu tukasema ni ya Mzee Malecela.
 
Last edited:
Na yeye Mzee Malecela aache kujificha ficha kwa kusingizia vyombo vya habari........malumbano yepi hayo.........aseme tu wazi......Dr. Mwakyembe na Mh Rostam acheni malumbano........hii mambo ya sijui CCM kumeguka its none issue........we got him loud and clear na kwa msisitizo........JK kuendela hadi 2015....SIMPLE!!............suala la malumbano ni cover-up..........
 
Mzee Malecela anasema kuwa kwenye ukumbi wa NEC kuna maneno ya Baba wa Taifa yanasema "mimi ninang'atuka lakini naendelea kuamini bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba...."

Halafu anaendelea kusema mwaka 1992 wakati wakipitisha ripoti ya Nyalali kuruhusu vyama vyingi wakati yeye ni Waziri Mkuu "ndipo Baba wa Taifa alisema maneno haya."

Nyerere aling'atuka lini na vyama vingi viliruhusiwa lini? Malecela, of all the people, asiwe loose na hizi facts.

i296_Malecela.jpg"

sasa si useme Nyerere "aling'atuka" lini? au maneno hayo aliyasema lini? Ukiwa unajua jambo na unalo uhakika weka tu masahihisho siyo mashindano!
 
Hahahaha point...!

Wakati mwingine wanaboa.! Kama unaona mtu kasema kitu siyo sahihi, weka kitu sahihi siyo ukae pembeni na kutegea ili umrukie "aha!! gotcha!". Kama hutaki kusema unachokijua na unauhakika nacho usikosoe! Wakati mwingine naona ni upuuzi tu!
 
Mzee malecela ni sawa tu na mtu ambaye anaishi katika ujima.Yaani hadi leo bado ana hutuba za vitisho kwa wanaotaka kutumia haki zao kikatiba sababu tu hataki swahiba wake apingwe.Namshauri ajifunze kukaa kimya asije umbuka kama mzee msekwa.
 
Mzee Malecela anasema kuwa kwenye ukumbi wa NEC kuna maneno ya Baba wa Taifa yanasema "mimi ninang'atuka lakini naendelea kuamini bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba...."

Halafu anaendelea kusema mwaka 1992 wakati wakipitisha ripoti ya Nyalali kuruhusu vyama vyingi wakati yeye ni Waziri Mkuu "ndipo Baba wa Taifa alisema maneno haya."

Nyerere aling'atuka lini na vyama vingi viliruhusiwa lini? Malecela, of all the people, asiwe loose na hizi facts.

i296_Malecela.jpg"

Kuhani, kwa hili Mzee Malecela yuko sahihi. Mwalimu aling'atuka mara mbili, katika nafasi mbili tofauti. Mwaka 1985 aling'atuka na kuachia u-rais wa nchi, lakini aliendelea kubaki na kofia ya Mwenyekiti wa Chama. Mwaka 1992 aling'atuka Uenyekiti wa Chama (CCM). Hayo maneno aliyasema wakati anang'atuka Uenyekiti.

Ambacho nashindwa kumuelewa yeye na viongozi wenye hulka kama yake, ni kwa nini wanadhani kuwa CCM hii ya sasa ni "madhubuti"? Kwa kuwa tu wanashinda chaguzi haina maana kuwa ni madhubuti! CCM baada ya kuwa kwenye siasa/utawala kwa miaka takribani 55 (1954 - 2009), bado kina wanachama milioni 4 tu na kinasumbuliwa na vyama vilivyo na uhai usiozidi miaka 15! Huu ni mpambano wa mtu mwenye malaria vs mwenye kipindupindu, hakuna madhubuti hapo.
 
jamani huyu mzee alikuwa kimya kwa muda mrefu ammeamua kutoa albamu yake sijui karecord studio gani?anatufanya watanzania vipofu anatuletea mambo ya mwaka 70,na kuna tetesi anataka kumrithisha mtoto wake wa kike jimbo lake pindi atakapostaafu
 
Sasa kama yeye anasema wanaolumbana wamalizane kwenye vyombo husika i.e. Chama n.k. na siyo kwenye vyombo vya habari kwa nini yeye asingesema hayo kwenye kikao cha chama chake hadi kuitisha mkutano na wanahabari wa kutoka kwenye vyombo vya habari na kusema wanaolumbana wasilumbane kwenye vyombo vya habari? What the hell?

Nilikuwa natafuta neno la kiswahili la hicho alichokifanya Jumanne nikalikosa lakini kwa kiingereza ni rhetoric. Yaani anakataza wanachama kulambana katika vyombo vya habari huku yeye akitumia vyombo hivyo hivyo kuendeleza malumbano hayo hayo. Kama angekuwa serious na anachokisema ni bora yeye mwenyewe kama mjumbe wa kudumu wa kamati kuu angetumia vikao vya chama kusema hayo aliyo yasema. Sasa unategemea watakao kuwa wameguswa na kauli zake watumia vikao vya chama kumjibu au nao wataitisha mkutano na waandishi wa habari? Nadhani maigizo haya sasa yanapoelekea ni kuleta uchafuzi wa hali ya kisiasa nchini na hakuna upande utakao faidika na matokeo haya. Kwani CCM hawana jinsi ya kutatua matatizo yao wenyewe hadi watusumbue umma wa watanzania wote? Naanza kuamini sasa huenda CCM imeshuhudia uongozi mbovu na dhaifu katika kipindi hiki kuliko wakati wowote katika historia.
 
Kama hajui chanzo cha malumbano je' ana authority gani kuwataka watu waache kuongelea au kuandika juu ya hayo malumbano, je kama chanzo chake ni sahihi??? This is old school ujamaa political tactics that have helped keep CCM in power for the last few decades and the rest of the nation in poverty. The truth is CCM is slowly self destructing from the inside and imejaa uozoo tupu and that is what worries him most....
 
Viongozi wa CCM wanashindwa kuelewa ya kua soga zimepitwa na wakati maelezo yake na majibu ya waandishi wa habari Hakujibu lolote mbali na kijikanyaga na kutoa vitisho kwa vyombo vya habari.Nilitegemea katika majibu au maelezo yake aelezee au afafanue nini chanzo cha malumbano?Na si lawama kwa vyombo vya habari Kweli vipo vyombo vya habari ambavyo vinatumiwa na mafisadi kuwachafulia majina wanaopinga ufisadi na cha kusikitisha baadhi yake vinamilikiwa na mafisadi ambao wako katika CCM na tena ni viongozi wamo katika kamati kuu za CCM.Kama kweli alikua anania ya kuonya kuhusu malumbano kwanini wasiitane katika vikao vyao na kuwekana sawa,kitendo cha yeye kutaka malumbano yakomeshwe kwa mujibu wa maelezo yake ya mwanzo kwamba malumbano yote yafanyike katika vikao vya chama basi kauli hizo hangelizitoa huko huko huko kwenye vikao vya chama.Pili kuna vyombo vingi vya habari ambavyo vinafichua maovu na ufisadi baada ya serikali na viongozi kuvisifu kwa msaada wanaoutoa na kushirikiana navyo ndiyo vinapigwa vita.Kiini cha Malumbano kinaeleweka,kwanza uozo uliopindukia na ufisadi katika chama cha mapinduzi na serikali kwa wale wenyeuchungu wanajua ya kua kutoa malalamiko katika vikao vya chama ni kutwanga maji kwenyekinu kwani chama kilisha nunuliwa zamani na mafisadi.Pili maamuzi ya serikali na Rais katika mambo mbalimbali ambayo yanatia mashaka.Swala la EPA,BOT,Buzwagi Dowans.Katika haya na mengine kunamaswali mengi kuliko majibu.Mfano mpaka sasa tunaendelea kushuhudia malumbano kuhusu swala la Dowans lakini hatujasikia kauli yoyote toka kwa Rais au serikali hatua gani zinzchukuliwa kuhusu tatizo hilo.Kwa mtu mwenyeakili timamu na anaejiheshimu ni aibu kuendelea kukaa kimya wakati mambo yanayotendeka katika chama na serikali hata mtoto mdogo wa darasa la kwanza anaweza kuona.Hicho ndio chazo cha malumbano.Hivyo Mh.Malecella huko ndiyo kwa kutafuta mchawi wenu na sio katika vyombo vya habari.Vyombo vya habari haviwezi kuandika kuhusu ufisadi kama haupo.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom