Uchaguzi 2020 Lissu shughulika na kuhubiri Sera zinazoenda kuondoa kero za watu, malumbano yatakutoa kwenye reli

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Ukiwa kiongozi jitahidi Sana kutoongozwa na hisia au chuki. Watu wa Mpira wanajua jinsi ya kumfanya mpinzani awe na hasira ili akose utulivu mchezoni.

Unamkumbuka beki kisiki Juma Nyoso au Forward Mkolofi Diego Costa.

Sio lazma ujibu au ulumbane kila kitu muda NI machache Sana. Ukipita sehemu ukaanza kutumia muda mwingi kuzungumzia ugonvi na tume unakosa nafasi muhimu kufafanua Sera yako ya maendeleo ya watu.

Watu wanataka Sera zitakazoinua Hali zao za maisha. Wafanye Kazi wapate malipo mazuri, mfumo wa Kodi uwe rafiki wanunue na bidhaa kwa Bei nzuri. Mi nilishangaa mzee moja miaka karibu sabini alivyombana gwajima kwa mifano dhahili kabisa juu ya Bei ya sukari kuwa Mara mbili bara kuliko Zanzibar.

Watu wanataka fedha wanayopokea itoshe kuwapatia Nyumba Bora, elimu Bora, Afya bora. UCHAGUZI sio Lele mama watu wanakuja kumsikiliza Sera sio kukushangaa.

Hayo mengine ya tume na wewe pambaneni kwa kifupi tu.

Tumia Lugha nyepesi Sana. Usitufundishe vifungu vya Sheria jukawaani. Sheria inaitaji fast learner kukuelewa.
 
Hayo anayohubiri Lissu ndio wapiga kura wake tunataka kuyasikia, ndio maana tuko radhi tunyeshewe namvua huku tukimsubiri kama ilivyokuwa bunda, natuko radhi tupigwe mabomu ili tumsikilize kama ilivyokuwa Nyamongo. Pia tutamsubiri mpaka usiku ili tumuone muokozi wetu Kama ilivyokeo leo Moshi.

Hata JPM agalagale, aluke samasoti sisi wananchi tulio wengi hatuwezi kumchagua.

Mtu aliesema hakuleta tetemeko, Kisha akaenda saidia nchi ya msumbiji kwa kupata janga la kimbunga, huku sisi Bukoba tukilala nje.

Mtu aliepuza zuio la Mahakama, kwa kuvunja nyumba zetu kuanzia Kimara mpaka Kibamba, huku akijua anakiuka muongozo wa mahakama.

Mtu ambae anawambia dada zetu wanataka kupanuliwa wapi kama alivyofanya dumila?

Mtu ambae ameshindwa kukemea watu wasiojulikana hata kwa kauli tuu, akiweka maisha yabaadhi ya watanzania wenzetu rehani, na wengine kupotea.

Mtu ambae anatuambia leo vitamvulisho vy machinga havina ulazima, kesho anatuambia ,tukienda benki tunaweza pewa mikopo kwa vitambukisho visivyo na jina,wala tin number, wala picha?

Kiukweli TUNDULISU hata aongee nini sisi tuliokosa ajira lazima tumpigie kura, sisi tulionyimwa mafao lazima tumpigie kura, sisi tuliopewa makato ya heslb 15% kinyume nasheria lazima tumpigie kura,sisi amabo tunajali hatima yamaisha yako mleta mada nawanao nakizazi chako chote na ndugu zako, lazima tumpigie TUNDULISU kura kwa maendeleo ya nchi yetu yaleo na kesho.
 
Lissu anaijua sheria na anazitambua haki zake vizuri ndio maana jiwe akaona dawa ya kuwanyamazisha watanzania ni kummiminia risasi Lissu.
Tunashukuru Mungu alikataa sasa Lissu anatupa elimu ya uraia.
Kwenye mikutano yake tutaenda na chupa za maji pigeni mabomu tuyazoee kabla ya kuingia barabarani mkiharibu uchaguzi.
 
Ukiwa kiongozi jitahidi Sana kutoongozwa na hisia au chuki. Watu wa Mpira wanajua jinsi ya kumfanya mpinzani awe na hasira ili akose utulivu mchezoni...
Kuanika maovu ni strategy nzuri sana. Let the world know how he is being intimidated for future reference and evidence! Sema atumie muda kidogo kwa hilo.... 5 minutes enough the rest sera na remedy for the ailments of the 5 yrs
 
Social media is an echo chamber,In it you either have staunch support and ruthless opposition.Ukikosea kampeni uka-base kuangalia social media inasema NN ,ndo uchukue platform ya kampeni hapo, you are doomed to fail and he has fallen into the trap,and they are going to derail his campaign for the next 30 days.
 
Hayo anayohubiri Lissu ndio wapiga kura wake tunataka kuyasikia, ndio maana tuko radhi tunyeshewe namvua huku tukimsubiri kama ilivyokuwa bunda, natuko radhi tupigwe mabomu ili tumsikilize kama ilivyokuwa Nyamongo. Pia tutamsubiri mpaka usiku ili tumuone muokozi wetu Kama ilivyokeo leo Moshi...
Ungeondoa jazba, ungemuelewa mwandishi
 
Social media is an echo chamber,In it you either have staunch support and ruthless opposition.Ukikosea kampeni uka-base kuangalia social media inasema NN ,ndo uchukue platform ya kampeni hapo,you are doomed to fail..and he has fallen into the trap,and they are going to derail his campaign for the next 30 days.

Kwa hiyo wewe na jiwe mnamhurumia asifeli?
 
Ukiwa kiongozi jitahidi Sana kutoongozwa na hisia au chuki. Watu wa Mpira wanajua jinsi ya kumfanya mpinzani awe na hasira ili akose utulivu mchezoni...

Kwa hiyo wewe, jiwe na Mi-CCM myenzio mnamhurumia Lissu asije mwisho kushindwa uchaguzi ndiyo maana mnampa ushauri huu?

You must be kidding!
 
Ukiwa kiongozi jitahidi Sana kutoongozwa na hisia au chuki. Watu wa Mpira wanajua jinsi ya kumfanya mpinzani awe na hasira ili akose utulivu mchezoni...
Sera Ni porojo Kama huna Katiba nzuri,

Wenye akili hatusililizi sera uchwara, sera kuuu Ni Katiba na utawala wa Sheria

Kama ambavyo Yesi alitupa amri kuu ya upendo
 
ngombe zake hazielewi,ila tunaotaka mabadiriko ya kweli tunajua ni jinsi gani ana loose focus.
 
Hayo anayohubiri Lissu ndio wapiga kura wake tunataka kuyasikia, ndio maana tuko radhi tunyeshewe namvua huku tukimsubiri kama ilivyokuwa bunda, natuko radhi tupigwe mabomu ili tumsikilize kama ilivyokuwa Nyamongo. Pia tutamsubiri mpaka usiku ili tumuone muokozi wetu Kama ilivyokeo leo Moshi....
Hakuna kipindi chadema wamekosa mgombea kama kipindi hikii.
 
Kuanika maovu ni strategy nzuri sana. Let the world know how he is being intimidated for future reference and evidence! Sema atumie muda kidogo kwa hilo.... 5 minutes enough the rest sera na remedy for the ailments of the 5 yrs

CCM ni wajuzi wa fitna ndugu yangu,kama unakumbuka ya ubunge wa lissu utaelewa unachoambiwa.

lissu ni mjuvi nguli wa sheria,but linapokuja swala la kamati ya roho mbaya kukaa kikao,hizo sheria zilizoko kichwani zinakuwa kama mapambo tu.
 
Sera Ni porojo Kama huna Katiba nzuri,

Wenye akili hatusililizi sera uchwara, sera kuuu Ni Katiba na utawala wa Sheria

Kama ambavyo Yesi alitupa amri kuu ya upendo

sasa katiba inabadirishwa kwenye campaign!!!!
 
TAFAKURI BAADA YA HABARI.

Mkemia na Upinzanium!

Mkemia mmoja nguli, PHD (Permanent Head Damage), alijimwambafy kwa wakemia wenzie mpaka wakampa ukuu wa kitengo!
Mara baada ya kushika ofisi alifanya mambo mengi makubwa ikiwa ni pamoja na kununua vinu vingi vya kuchakata madini. ... lakini kubwa zaidi ni pale alipoutangazia umma kuwa lile tatizo la muda mrefu la madini ya 'Mwambium' kuwa na kiasi kikubwa sana cha 'Upinzanium' yeye atalimaliza na si muda mrefu atapata pure 'MWAMBIUM', yaani 99.999% pure.

Wakemia wenzie walipomuambia 'MWAMBIUM' safi kiasi hicho ni hatari na kwamba kiasi fulani cha 'Upinzanium' kinatakiwa kibakie kubalance shobo akawaambia waache kuwashwa ... huku akiwauliza wao walifanya lipi la maana kipindi chao?

Hakuishia hapo, akawatimua mateknishani wawili waliomsaidia sana wakati akiusaka ukuu na kisha kumuajiri mwanasheria, bingwa wa kumsifia, ili awanyamazishe wakemia wenzie.

Waskia sana ... kumbe mkemia alikuwa haijui vizuri 'MWAMBIUM', kwamba ikiwa safi sana na ukaitunza sehemu moja kuzidi uzito unaokubalika huwa inajilipua yenyewe bila shinikizo la nje (SPONTANEOUS REACTION)! Sasa maabara imelipuka na CHAIN REACTION inatishia kuangamiza kiwanda chote! 🤔🤔🤔 ... ama kweli Kemia bila Fizikia ni Maumivu! ... na nshomile waliishasemaga:" "...yakwatilwa mugogo niwe mshuma! (aliyekutwa na mkungu wa ndizi ndiye mwizi!) CASE CLOSED!

KIBURI SI MAUNGWANA!

😅
👊 ✌✌✌💥
 
Hayo anayohubiri Lissu ndio wapiga kura wake tunataka kuyasikia, ndio maana tuko radhi tunyeshewe namvua huku tukimsubiri kama ilivyokuwa bunda, natuko radhi tupigwe mabomu ili tumsikilize kama ilivyokuwa Nyamongo. Pia tutamsubiri mpaka usiku ili tumuone muokozi wetu Kama ilivyokeo leo Moshi...
Utakuwa na hali mbaya sana Magufuli akipita tena kuwa raisi.

Shauri yako punguza chuki.
Magufuli sio malaika, nae anakosea. Mtu huwezi kuwa mwema wakati wote.
 
Back
Top Bottom