Umeandika mengi sana, lakini kwangu mimi niliye ziona video za masheikh wenu wakubwa kabisa hapa Tanzania ambazo nadhani ndizo walizo ziona Tanzania Daima ambazo masheikh wenu wakikiri kuwa walikubaliana kuwa kura zote za waislamu apewe kikwete kwasababu ni mwislamu mwenzao kuliko Padri Slaa ambae amepanga akiingia madarakani atachukua raslimali za watu wa kusini na kuzipeleka nje ya nchi ukizingatia kusini wengi ni waislamu na baadae Lipumba alikri kufanya makubaliano hayo hata siku ya kwenda kuapishwa Kikwete alienda tu si kwa sababu hajui nini kilifanywa na masheikh laah hasha bali alienda kwa masilahi ya dini yake sasa basi kama tutaendesha nchi kwa namna hiyo tunalipoteza na tanzania Daima kama chombo chenye haki ya kukemea naona kipo sawa kwa swala hilo hata juzi kuna video hapa ililetwa ya Ole Medeye akiwaambia wamasai wenzake wawafukuze wachaga Arusha na kamwe wasikubali kuongozwa na wachaga kuanzia ubalozi,serikali za mitaa, ubunge, umeya... wamekemea lakini kama kuna vitu huwa vinatokea na wanavifumbia macho kwasababu labda kimefanywa na dini fulani au kabila fulani hapo issue nyingine....wewe ni kati ya waislamu mnao jitambua ndiyo maana unaweza kuona kuwa hata kama lipumba akija msikitini kwenu kuwaapisha unajua unacho kifanya kwa maana utaendelea na msimamo wako lakini je ni waislam wangapi wanao potoshwa na hao masheikh kwa kurubuniwa nakina Lipumba na kikwete...Je kwa swala hili ulitaka gazeti la Tanzania Daima waandike nini juu ya siasa hizo chafu!? wamekosea nini? ningeweza kuwaelewa kiasi kama matamshi hayo yange tolewa na kiongozi wa kidini lakini si kwa mwenyekiti wa chama tena msomi kama Prof. Lipumba...Vyombo hivi vikemee yote maovu bila kujali dini wala kabila....