Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Status
Not open for further replies.

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,060
Reaction score
309
KASHFA zaidi za Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuendesha kampeni za kidini kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao zimezidi kuanikwa.

Wakati kashfa nyingine iliyomtuhumu kutoboa siri ya namna alivyofanya kampeni za kuwashawishi watu wa dini yake kumchagua aliyekuwa mgombea wa urais kupitia CCM kwa misingi ya kidini, ikiwa bado inarindima, Lipumba anatuhumiwa kutoa maagizo kwa waumini wa Kiislamu kuchagua mgombea wa dini hiyo mwaka 2015.

Mkanda wa video ulionaswa na Tanzania Daima unamuonyesha kiongozi huyo wa ngazi ya juu kabisa wa CUF akiwahamasisha Waislamu kuungana na kushikamana kupigania haki zao za kiraia.

Katika mkanda huo uliorekodiwa katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, mara baada ya swala ya Ijumaa unamwonyesha Profesa Lipumba akiwataka waumini kupigania haki zao ambazo alisema kwa sasa hawazipati.

Lipumba aliwaambia waumini hao kuwa serikali imewatupa na kuwafanya waishi kama raia wa daraja la nne ndani ya nchi yao.

Kwenye mkanda huo wa video, Profesa Lipumba anasikika akiwataka Waislamu kujipanga kikamilifu kisiasa ili kuzuia kile alichokiita uuzwaji wa nchi na rasilimali zake.

Alisema kuna mafisadi wamejipanga kuchukua nchi na kuiuza jumla huku wakiungwa mkono na watu ambao hakuwataja.

Alifafanua kuwa mafisadi hao wanaendesha biashara ya madisko inayoambatana na uchafu wa kila aina, biashara ya vileo na dawa za kulevya.

"Kwahiyo ndugu zangu Waislamu tupo njiapanda katika nchi yetu. Tuna rasilimali kubwa zinazidi kugunduliwa, lakini siasa zetu zinazidi kuwa na matatizo na sisi Waislam tupo chini. Utajiri huu unatolewa macho, wanahitajika watu ambao ni mafisadi waweze kushika nchi, na hao ndio wanaoungwa mkono washike nchi halafu waweze kuiuza nchi yote kwa ujumla.

"Kwahiyo, huu ni wakati wa kuwa macho kwamba tupo njiapanda. Hii neema, utajiri unaogunduliwa ikiwa hatutajipanga vizuri, neema hii itabadilika kuwa balaa, neema hii badala ya kumsaidia kila Mtanzania aweze kuneemeka na neema hii, itageuka kuwa balaa dhidi yetu," alibainisha Profesa Lipumba.

Aliwaeleza waumini hao kuwa kwa sasa Waislamu wanapaswa kushiriki kikamilifu katika harakati za siasa za nchi kama walivyoshiriki wazee wao wakati wa kudai uhuru.

"Kwamba kila mwananchi, kila Mtanzania awe raia wa daraja la kwanza. Apate fursa ya uhuru wa dini yake, apate fursa ya kuelimishwa kwa kadiri ya uwezo ambao Mwenyezi Mungu amempa bila kubaguliwa, apate fursa ya kupata huduma bora za afya, apate fursa ya kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa serikali, apate fursa ya uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu.

"Kazi ipo kwetu, na ndugu zangu sisi tunapozungumza hapa tumejitoa mhanga. Kwamba hii ni nchi yetu sote, tunamuogopa Mwenyezi Mungu Tunamuogopa Mwenyezi Mungu na huu mwezi wa Ramadhan," aliweka mkazo Profesa Lipumba.

Katika kusherehesha kauli ya Profesa Lipumba, mhadhiri wa Kiislamu, Ustaadhi Said Ricco alisema kuwa waendesha madisko aliowakusudia Profesa Lipumba ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, maelezo ambayo hayakukanushwa na kiongozi huyo wa CUF.

Katika hatua ya kushangaza, waumini waliohudhuria ibada hiyo walilishwa kiapo na Ustaadhi Ricco cha kuahidi kumpigia kura Profesa Lipumba katika uchaguzi mkuu wa 2015 ili awe Rais wa Tanzania, huku mwenyewe akishuhudia kitendo hicho bila kusema chochote.

Gazeti hili lilifanya juhudi za kumpata Profesa Lipumba ili atoe ufafanuzi wa kauli zake, lakini ilishindikana kutokana na simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani.

Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakuweza kujibu chochote.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alipoulizwa kuhusu kauli za mwenyekiti wake, alisema hajui chochote kwani huwa haambatani naye anapokwenda kusali misikitini.

"Mimi sijui chochote kwa sababu huwa siambatani naye misikitini, nakushauri umtafute yeye mwenyewe azungumze maana yeye ndiye aliyerekodiwa akitoa kauli hizo, siyo mimi Mtatiro," alisema.

Lakini Mtatiro alipokumbushwa jinsi alivyosimama kidete kumtetea Lipumba katika tuhuma za awali kuhusiana na suala hilo la kampeni za kidini, na vipi sasa ashindwe kutoa kauli, kiongozi huyo alisisitiza kutoongea lolote, na kudai hayo ni masuala binafsi ya mwenyekiti wake na sio msimamo wa chama chao.

Hivi karibuni Profesa Lipumba alikaririwa akikiri kwamba alihamasisha kuunganisha nguvu kati ya CCM na CUF ili kumwezesha Rais Kikwete kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kigezo cha udini.

Kashfa hiyo ambayo haijakanushwa na Lipumba iliibua mjadala mkubwa, huku CUF wakijitahidi kumtetea bila mafanikio.

Aidha, licha ya video hiyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii, ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini haijawahi kusema lolote kuhusiana na suala hilo.

Tanzania Daima
 
Huyu Lipumba kuna mtu kamtia uchizi, vitu anavyozungumza utafikiri mtoto wa darasa la pili. Yawezekana Lipumba mwenyewe ni project ya CCM kwenye mambo ya udini amabayo CCM wanajua udini unaweza kuwatoa kwenye tundu la sindano 2015.
 
Hivi jamani tutumie kipaza sauti gani kupaza sauti zetu zisikike kwa Tendwa ili aweze kutenda haki kwa vyama vyote? Amani ya nchi hii ikipotea huyu mzee tutafukua kaburi lake na kuichoma moto mifupa ili kumaliza hasira zetu. Kwanini amepewa mamlaka halafu anayatumia vibaya hivyo? Kwanini Tendwa hakemei mambo haya?
 
CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!
 
Lipumba akapokea bonge la package toka CCM,
Lake ni haribuharibu, initial yake kaweka pembeni, mapene kwanza uprof badae
 
Lipumba anahasira sana na JK alimsaliti sasa naye anaiga nyenendo za Jk za kupata kura za waislam kazi kweli kweli
 
Msimamo wa Tanzania Daima dhidi ya Waislam unajulikana sana hata kwa Muislam Muasi ndio maana haukuweka kambi pale Sumbawanga kanisa lilipotangaza kuwatenga Wakristo wote walompa Kura Mh.kessy, Rev Mtikila alipotengeneza na kusambaza Waraka wa kuwataka Wakristo wote wasimpe kura Jakaya 2010, halikupiga kambi kuripoti Mgombea aliekusanya Viongoz wa Dini Singida ili waingie kwenye Kampeni, siku nyingine likapige kambi makanisani lije litoe Habari kuwa wakristo kupitia Jukwaa lao walitangaza kuinyima Serikal ya Jakaya Ushirikiano na ifikapo tarehe 1july,2013 wakristo wote wawe wamejitoa CCM. Tangu mmeanza Vita zenu dhidi ya Uislam na Waislam kama kuna kitu kimepatikana basi ni kuwatia Ujasiri Waislam, Jifunzen kuendesha Siasa zenu bila ya kukabiliana na Uislam, maana hii dini mmeikuta na mtaiacha
 
Kama anadhani waislamu ndiyo kundi linalohadaika kirahisi anajidanganya...
 
Kwa nini awashambulie madj wa Chadema badala ya magaidi wa CCM walioshika nchi?kwa nini azungumzie matatizo yajayo ya kufikirika(ya serikali mpya chini ya Chadema)badala ya kuzungumzia haya yaliyopo sasa chini ya CCM na tunayaona?wenye akili tushamwelewa.akachukue buku 7 Lumumba!
 
Turufu ya mwisho kwa ccm ni kutafuta support ya vyama vinavyochechemea ambapo CUF walishakubaliana tangu 2010, NCCR kwa sasa mwenyekiti wake anaripoti kwa mwenyekiti wa ccm kulingana na makubaliano ya nafasi ya ubunge aliyopewa, mwenyekiti wa TLP anaandaliwa mafao yake ya unaibu waziri mkuu, mkataba na DP uko mbioni kukamilika, UDP anaendelea kulipwa part-time
 
Msimamo wa Tanzania Daima dhidi ya Waislam unajulikana sana hata kwa Muislam Muasi ndio maana haukuweka kambi pale Sumbawanga kanisa lilipotangaza kuwatenga Wakristo wote walompa Kura Mh.kessy, Rev Mtikila alipotengeneza na kusambaza Waraka wa kuwataka Wakristo wote wasimpe kura Jakaya 2010, halikupiga kambi kuripoti Mgombea aliekusanya Viongoz wa Dini Singida ili waingie kwenye Kampeni, siku nyingine likapige kambi makanisani lije litoe Habari kuwa wakristo kupitia Jukwaa lao walitangaza kuinyima Serikal ya Jakaya Ushirikiano na ifikapo tarehe 1july,2013 wakristo wote wawe wamejitoa CCM. Tangu mmeanza Vita zenu dhidi ya Uislam na Waislam kama kuna kitu kimepatikana basi ni kuwatia Ujasiri Waislam, Jifunzen kuendesha Siasa zenu bila ya kukabiliana na Uislam, maana hii dini mmeikuta na mtaiacha

huwakilishi waislam wowote wewe na wala waislam hawadanganyiki kirahisi kama unavyotaka kuwachota hapa.wala sie wakristo hatudanganyiki kirahisi ili tukujibu hoja yako kwa hasira na kuanzisha mjadala wa kidini hapa.udini umezaliwa Lumumba,utakua na kustawi Lumumba,utaishi Lumumba na utafia Lumumba.haya nenda kadoee daku kwa Lumumba boy mwenzio Lipumba!kamsimulie riwaya hii mkiwa kwenye foleni ya buku 7 Lumumba na sio hapa jf!
 
Huyo nyie mwacheni tu ataona matokeo ya anacho kinadi 2015. anaweza asipate hata MBUNGE mmoja na hata DIWANI. Huwezi kuamini kuwa huyu ni PROF.
 
huwakilishi waislam wowote wewe na wala waislam hawadanganyiki kirahisi kama unavyotaka kuwachota hapa.wala sie wakristo hatudanganyiki kirahisi ili tukujibu hoja yako kwa hasira na kuanzisha mjadala wa kidini hapa.udini umezaliwa Lumumba,utakua na kustawi Lumumba,utaishi Lumumba na utafia Lumumba.haya nenda kadoee daku kwa Lumumba boy mwenzio Lipumba!kamsimulie riwaya hii mkiwa kwenye foleni ya buku 7 Lumumba na sio hapa jf!

wapi nimeandika kuwa haya mawazo yanawakilisha waislam? Haya ni mawazo yangu kama vile ulivoweka yako japo wewe umejikweza kujifanya kuwasemea wengine, kila usichopenda kusikia wewe usitumie nafsi ya wingi kuleta utetezi, hapa ni eneo la mjadala wa wazi, hutaki kusoma usichopenda kisemwe changanya yeboyebo zako, mnaleta thread za kidini mnataka zijibiwe ki biolojia? Wewe ni nani hapa mpaka uwapangie watu cha kuchangia na kwa namna gani wachangie? Umeambiwa na nan kuwa kila mwenye kuweka comment yake basi anataka ajibiwe kias cha kusema eti nataka kuleta udin? Ww si bure huko Mtaa Ufipa wenzio watakuwa wanakuchinja sikumoja moja ndo maana ukihamuka unatafta Kisu kwa nguvu zote!
 
hahahahahhahahaa haya bana...habari yako bwana tendwa
 
Mkuu unahangaika andika vizuri basi hata yasomeke kwani umelewa pombe ukecopy copy ovyo hovyo bila hat kuhariri ukabandika, elimu yako ni ya wapi wewe?

message sent!​ Ndio maana ya maandishi, ni kupeleka habari na iwapo limefanyika hayo madalhabibi si issue.
 
wapi nimeandika kuwa haya mawazo yanawakilisha waislam? Haya ni mawazo yangu kama vile ulivoweka yako japo wewe umejikweza kujifanya kuwasemea wengine, kila usichopenda kusikia wewe usitumie nafsi ya wingi kuleta utetezi, hapa ni eneo la mjadala wa wazi, hutaki kusoma usichopenda kisemwe changanya yeboyebo zako, mnaleta thread za kidini mnataka zijibiwe ki biolojia? Wewe ni nani hapa mpaka uwapangie watu cha kuchangia na kwa namna gani wachangie? Umeambiwa na nan kuwa kila mwenye kuweka comment yake basi anataka ajibiwe kias cha kusema eti nataka kuleta udin? Ww si bure huko Mtaa Ufipa wenzio watakuwa wanakuchinja sikumoja moja ndo maana ukihamuka unatafta Kisu kwa nguvu zote!

matusi haya yanaonyesha ujumbe umefika na ndio haswaa lengo langu,si bora mtaa wa ufipa wana visu,mie nina sime ndefuu,ikishakuchoma unaisikilizia huku ukibwabwaja ovyo ovyo,huku ukitamani niendelee kama ambavyo utaendelea kunichokoza hapa..moja..mbili..si unaona..ananiandikia kapost kengine,!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom