Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Lipumba achochea tena udini: Waumini walishwa kiapo!

Status
Not open for further replies.
Mkuu chama,
Kiukweli muda mwingine nashindwa kuelewa hivi gazeti kama hili linaloandika habari za kuleta taharuki katika jamii, inamaana waandishi wake wote wanakubaliana na machapisho kama haya. Nilifikiria kuona watu kama Mohamedi Mtoi akitoa msimamo wake ktk mambo kama haya. Inamaana ndugu yetu amekubaliana na habari hii yenye athari kubwa kwa pande zote za imani?. Hili gazeti nila ajabu na pia nathubutu kusema waandishi ni wa ajabu kweli. Shukrani kwa THE BIG SHOW kwakuwa muazi na hawa ndio watu tunaowataka katika siasa zetu. Au ni kwakuwa Mohamedi Mtoi aliipata kazi TanzaniaDaima kama kipozeo cha kuandikwa kwa bandiko lake lile la Hawa ndio maadui wa uislamu na waislamu Tanzania? Nikimaanisha analinda kibarua chake. Ritz.

Mkuu CHAMVIGA
Ndoto za Mohamedi Mtoi ni kuchukua nafasi ya Kibanda kwa mantiki hii hata akiambiwa akachambishe nguruwe yupo tayari kwa hili; hiki ni kichekesho mtu kuandika nakala ya maadui wa Uislamu wakati yeye mwenyewe Uislamu haujui; namshauri atafute namna nyingine ya kuganga njaa hili la kutumia dini kuganga njaa zake ni hatari kubwa sana kwa jamii inayomzunguka.
 
Last edited by a moderator:
Sasa nahama CUF rasmi....Mwenyekiti wangu unaleta utengano na amegeuka kuwa mwanaharakati wa Kiislamu..
 
Dini ni tamu uongo ukiwa mwingi, ukweli na uchungu wa dini unafahamika, hofu ya ni uwezo wa kuelewa kwa baadhi yetu
 
KASHFA zaidi za Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuendesha kampeni za kidini kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao zimezidi kuanikwa.

Wakati kashfa nyingine iliyomtuhumu kutoboa siri ya namna alivyofanya kampeni za kuwashawishi watu wa dini yake kumchagua aliyekuwa mgombea wa urais kupitia CCM kwa misingi ya kidini, ikiwa bado inarindima, Lipumba anatuhumiwa kutoa maagizo kwa waumini wa Kiislamu kuchagua mgombea wa dini hiyo mwaka 2015.

Mkanda wa video ulionaswa na Tanzania Daima unamuonyesha kiongozi huyo wa ngazi ya juu kabisa wa CUF akiwahamasisha Waislamu kuungana na kushikamana kupigania haki zao za kiraia.

Katika mkanda huo uliorekodiwa katika Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam, mara baada ya swala ya Ijumaa unamwonyesha Profesa Lipumba akiwataka waumini kupigania haki zao ambazo alisema kwa sasa hawazipati.

Lipumba aliwaambia waumini hao kuwa serikali imewatupa na kuwafanya waishi kama raia wa daraja la nne ndani ya nchi yao.

Kwenye mkanda huo wa video, Profesa Lipumba anasikika akiwataka Waislamu kujipanga kikamilifu kisiasa ili kuzuia kile alichokiita uuzwaji wa nchi na rasilimali zake.

Alisema kuna mafisadi wamejipanga kuchukua nchi na kuiuza jumla huku wakiungwa mkono na watu ambao hakuwataja.

Alifafanua kuwa mafisadi hao wanaendesha biashara ya madisko inayoambatana na uchafu wa kila aina, biashara ya vileo na dawa za kulevya.

“Kwahiyo ndugu zangu Waislamu tupo njiapanda katika nchi yetu. Tuna rasilimali kubwa zinazidi kugunduliwa, lakini siasa zetu zinazidi kuwa na matatizo na sisi Waislam tupo chini. Utajiri huu unatolewa macho, wanahitajika watu ambao ni mafisadi waweze kushika nchi, na hao ndio wanaoungwa mkono washike nchi halafu waweze kuiuza nchi yote kwa ujumla.

“Kwahiyo, huu ni wakati wa kuwa macho kwamba tupo njiapanda. Hii neema, utajiri unaogunduliwa ikiwa hatutajipanga vizuri, neema hii itabadilika kuwa balaa, neema hii badala ya kumsaidia kila Mtanzania aweze kuneemeka na neema hii, itageuka kuwa balaa dhidi yetu,” alibainisha Profesa Lipumba.

Aliwaeleza waumini hao kuwa kwa sasa Waislamu wanapaswa kushiriki kikamilifu katika harakati za siasa za nchi kama walivyoshiriki wazee wao wakati wa kudai uhuru.

“Kwamba kila mwananchi, kila Mtanzania awe raia wa daraja la kwanza. Apate fursa ya uhuru wa dini yake, apate fursa ya kuelimishwa kwa kadiri ya uwezo ambao Mwenyezi Mungu amempa bila kubaguliwa, apate fursa ya kupata huduma bora za afya, apate fursa ya kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa serikali, apate fursa ya uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu.

“Kazi ipo kwetu, na ndugu zangu sisi tunapozungumza hapa tumejitoa mhanga. Kwamba hii ni nchi yetu sote, tunamuogopa Mwenyezi Mungu Tunamuogopa Mwenyezi Mungu na huu mwezi wa Ramadhan,” aliweka mkazo Profesa Lipumba.

Katika kusherehesha kauli ya Profesa Lipumba, mhadhiri wa Kiislamu, Ustaadhi Said Ricco alisema kuwa waendesha madisko aliowakusudia Profesa Lipumba ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, maelezo ambayo hayakukanushwa na kiongozi huyo wa CUF.

Katika hatua ya kushangaza, waumini waliohudhuria ibada hiyo walilishwa kiapo na Ustaadhi Ricco cha kuahidi kumpigia kura Profesa Lipumba katika uchaguzi mkuu wa 2015 ili awe Rais wa Tanzania, huku mwenyewe akishuhudia kitendo hicho bila kusema chochote.

Gazeti hili lilifanya juhudi za kumpata Profesa Lipumba ili atoe ufafanuzi wa kauli zake, lakini ilishindikana kutokana na simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani.

Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakuweza kujibu chochote.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro alipoulizwa kuhusu kauli za mwenyekiti wake, alisema hajui chochote kwani huwa haambatani naye anapokwenda kusali misikitini.

“Mimi sijui chochote kwa sababu huwa siambatani naye misikitini, nakushauri umtafute yeye mwenyewe azungumze maana yeye ndiye aliyerekodiwa akitoa kauli hizo, siyo mimi Mtatiro,” alisema.

Lakini Mtatiro alipokumbushwa jinsi alivyosimama kidete kumtetea Lipumba katika tuhuma za awali kuhusiana na suala hilo la kampeni za kidini, na vipi sasa ashindwe kutoa kauli, kiongozi huyo alisisitiza kutoongea lolote, na kudai hayo ni masuala binafsi ya mwenyekiti wake na sio msimamo wa chama chao.

Hivi karibuni Profesa Lipumba alikaririwa akikiri kwamba alihamasisha kuunganisha nguvu kati ya CCM na CUF ili kumwezesha Rais Kikwete kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kigezo cha udini.

Kashfa hiyo ambayo haijakanushwa na Lipumba iliibua mjadala mkubwa, huku CUF wakijitahidi kumtetea bila mafanikio.

Aidha, licha ya video hiyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii, ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini haijawahi kusema lolote kuhusiana na suala hilo.


Tanzania Daima

Wote tunafahamu maana ya 'pumba'. Maana yake hakuna kitu cha maana. Na katika maongezi 'pumba' maanake ni kuongea utumbo au nothing useful. Pumba ziko za aina nyingi kutegemea vigezo vinavyotumika, mfano, kwa ukubwa kuna pumba na lipumba. sasa mtu akipewa jina 'pumba' halafu likaongezewa kivumishi na kuwa 'lipumba' basi mtu huyo hana usefulness tena kwenye jamii.
 
Lipumba ameongea sawa sawa sioni tatizo SLAA anapofanya vikao makanisani kwenu sio tatizo? Acheni unafiki. Mnafikiri kumuandika Katika TANZANIA DAIMA gazeti la CHADEMA kuwa mnambomoa kumbe mnamjenga, sisi waislam si wajinga tunajua kila kitu kinachoendelea Kati ya CHADEMA na KANISA.
 
CHADEMA na viongoz wa juu lazima watambue kuwa hili gazeti la TANZANIA DAIMA limekuwa kero kubwa sana,na limekuwa linaumiza sana hisia za waislam ambao kwa namna moja ama nyingine tunaonekana kama ni washabiki wa siasa za CHADEMA au wanachama wa CHADEMA,sikumbuki ni siku gani TANZANIA DAIMA limeandika jambo jema kuhus mirengo ya waislam na siasa zinazofanyika ndan ya CHADEMA.mara nyingi TANZANIA DAIMA imekuwa ni nyenzo ya kubomoa sana zaid ya kujenga,
Liko biased na lina double standards zisizo na mbele wala nyuma,na mara yingi hupenda sana kuchokonoa habari zinazodhoofisha uimara wa chadema,zinazotia doa uimara wa chadema na kuwachokoza wapinzani wenzao na kujenga matabaka ya chuki na wenzao,kwa hali hii inaipa nguvu kubwa sana CCM na kuifanya kazi ya kuindosha madarakani kuwa kama ndoto ya mchana,
ni wakati sasa UMEFIKA TANZANIA DAIMA lifanye kazi kama Magazeti yetu ya AN'NUR AU AL HUDAA,TUJUE MOJA...
mkuu nakukubali sana huna ushabiki "keep it up bro"
 
Mkuu CHAMVIGA
Ndoto za Mohamedi Mtoi ni kuchukua nafasi ya Kibanda kwa mantiki hii hata akiambiwa akachambishe nguruwe yupo tayari kwa hili; hiki ni kichekesho mtu kuandika nakala ya maadui wa Uislamu wakati yeye mwenyewe Uislamu haujui; namshauri atafute namna nyingine ya kuganga njaa hili la kutumia dini kuganga njaa zake ni hatari kubwa sana kwa jamii inayomzunguka.

Mkuu chama bwana mohamedi itabidi ajifunze kutokana na uzoefu. Chama chake kina magumashi mengi sana na yeye anayajua.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo akili yako iko kwenye makalio huwezi kuuona mpaka siku kiona watanzania wanakatana mapakanga ndiyo utaunda tume kuchuguza nini chanzo....kwasasa huwezi kuuona uchochezi unaofanywa na viongozi wako....
Hapo kwenye red ndio munavyofundishwa pale makao makuu kinondoni magogoni mutaisikia tuu labda wapige kura watu wa Arusha wenyewe!
 
mkuu nakukubali sana huna ushabiki "keep it up bro"


Brother Ukweli lazima tuuseme tuh,hata ikiwa namna gani,
Kukimbilia kuyaongea mambo kinafiki na kuficha ficha hisia ni dalili mbaya za kutojiamini na kutokuwa na maono,
SO,the best way ni kusema,tena kuyasema yale yaliyo moyoni kwa uwazi kabisa,
 
jk na lipumba ndio wadini wakubwa.
Bora wao wadini wakubwa kuliko Dr Slaa na Mowe wanatafuta "smpathy vote" kwenye msiba
406957_423048191094849_291533674_n.jpg
 
Bora wao wadini wakubwa kuliko Dr Slaa na Mowe wanatafuta "smpathy vote" kwenye msiba
406957_423048191094849_291533674_n.jpg

Boko Haram,hii wapi??mbona kama vile temeke??
Dah,naona makamanda wenzangu wanapata stafutahi kidogo hapo,hiyo watermelon ya Dr W. Slaa imenona sana kwa kweli,na hii swaum yangu imezidisha kunitamanisha kwa kweli,
 
Prof lipumba amenithibitishia kuwa kwenda shule si kipimo chakueleimika.

He is totaly an idi.ot n insane.
 
Thanks,hapa nazungumza mimi kama muislam,Muslims,We are smarter than that,In addition to that TANZANIA DAIMA MAGAZINE when it comes to such grounds of religious affairs it shows A View attachment 102868 Of its goddamned Double standards to the best level...!!
Kwahiyo kwasababi waislamu upo smart than hivyo basi alichozungumza lipumba na ricco ni sahihi?
 
Hata slaa ni project ya CCM pia, we unadhani ni kwanini ataki kurudisha kadi yao?

dr andgesema hayo maneno wew, na wanachama wote wa cuf na ccm wangeyachora kama tattoo juu ya viuno vya wake zenu, na kutangaza dunia nzima, ila kwa sababu ni project ya CCM hakuna wa kukemea, jamaa anaendelea kutoa cd za udini daily
 
Kwahiyo kwasababi waislamu upo smart than hivyo basi alichozungumza lipumba na ricco ni sahihi?

Mkuu mi huwa sometimes najiuliza mfano aitwe lipumba na slaa geneva kule kila mtu akapewa dakika tano adondoke nondo za uchumi.. sijui nani atatoka mshindi.. ?
 
Pamoja na uanachadema wangu,TANZANIA DAIMA wanatakiwa kuwa makini wanapoandika habari zinazohusu Waislam na uislam, siungani nao kabisa kuhusu mlolongo wa habari za misikitini maana zinachochea chuki ya kidini! CDM isipokuwa makini na Gazeti hili jinsi linavyoandika habari za lipumba misikitini, itajitengenezea kaburi na ile dhana ya udini itaonekana ina mashiko. Achaneni na habari za misikitini/makanisani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom