Nitafurahi kama utanieleza kuhusu Memorandum kwa undani kwa sababu najua machache tu kuhusu hili.
Kwa ufupi nachojua kuhusu memorandum ni hiki:
Wamisionari wa Kikristo walipoingia Tanganyika na Zanzibar walikuta Wamisioari wa Ki-Islamu wameshafika mapema na Uislamu tayari umetanda kwenye njia zote wa Watumwa.
Lakini pia Wamisionari wa Kikristo walikuta hakuna Shule.
Ukisoma historia ya Wakoloni wa kutoka mataita ya Kikristo na Mataifa ya Ki-Islam kila mahali, yanajitokeza haya. walipora rasilimali, wote walieneza dini zao kwa ajili ya kujenga mahusiano ya kimila na watawaliwa, lakini palijitokeza utofauti kwenye suala la Elimu. Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule na Mahospitali; Wamisionari wa Kiarabu walijenga misikiti bila shule, bila mahospitali--ukiaondia Dhehebu la Ismailia, ambao ni Waislamu tofauti sana na Suni na madhehebu mengine ya Kiislamu ambao wameshamiri Tanzania.
Baada ya Uhuru wa Tanganyika, na Baadaye Zanzibar, Viongozi wetu Nyerere na Karume walirithi mahospitali na shule nyingi zaidi za Makanisa kuliko zilizo chini ya Misikiti. Nyerere alikuwa Mkristo mwenye upeo mpana wa Imani ya Kikristo. Kwa hiyo aliona haja ya kujenga taifa lenye usawa pasipo kubagua watu kidini.
Zile shule na Mahospitali ya Kanisa vilitaifishwa na kuwa mali ya Wakristo, Waislamu na Wapagani. Lakini serikali ambayo imekuwa chini ya Tanu, ASP na baadaye CCM ilishindwa kuziendesha hizi taasisi zenye asili ya Dini ya Kikristo ikaomba wenye nazo warudishiwe kwa sababu huduma ilikuwa hovyo kabisa hadi majengo yakawa yanataka kuanguka katika baadhi ya taasisi hizo. Wenye hizo taasisi asilia (yaani makanisa) walirudishiwa baadhi ya shule zao na mahospitali. Najua wapo waliokataa kuzipokea--mfano ukiwa Baptist Hospital ya Mbeya Mjini ambayo sasa inaitwa META.
Baadae Serikali iliomba kuchangia uendeshaji wa hizi taasis ambazo wenye nazo walirudishiwa. Hili ndilo lililozaa MoU unayoisema wewe. Sasa naomba unipe upande wako wa uelewa wa jambo hili la MoU.