Truth Matters sidhani kama hii ni issue ya CDM,jambo la msingi hapa ni Mhe. Lipumba kujitokeza hadharani na kutolea ufafanuzi shutuma hizi nzito.CHADEMA wanafurahisha sana. Wao UDINI upo issue ikihusu waislamu tu. Wakati maaskofu wanawataka waumini wamchague mtu atakayelinda TUNU za kikristo walichekelea tu na kusifu kwa sababu wangepata kura za bure. Ni chizi gani asiyejua CHADEMA huwezi kuitenganisha na Ukristo. Msidhani watu ni wajinga!
Inachofanya TanzaniaDaima ni kukipigia kampeni chadema katika hili na kuidhoofisha cuf ila nikinyume kabisa ila inazidi kukifanya kipendwe na wale watu Wenye kufuata mikumbo ya kidini. Waislamu wanapaswa kuelewa maendeleo yetu hayaji eti kwakupewa sapport na chama flani ila kwakujituma. TanzaniaDAIMA inajenga chuki zaidi kwa waislamu kuichukia chadema.
Staili ya uandishi wa gazeti hili la Mbowe ni wa hatari kwani itafika hatua waislamu na wakristo kupigana kwa chokochoko kama hizi.
Nimekuuliza hayo ni maneno ya Prof Lipumba? naona bado unarusha. Unanchekesha.
Hivi Lipumba ni lini alitangaza kuwa atagombea 2015?
Nimekusoma,nataka kuweka vitu wazi kabisa na watu wafaham uhalisia,
Uislam kama uislam ni mfumo uliokamilika kimaisha,,uislam hauwez kuwa subset ya siasa,bali siasa inaweza kuwa ni subset ndan ya uislam,
Uislam na sisi waislam hatuhitaji backup ya chama chochote kile ili tuweze kusurvive na kukamilisha mafundisho ya imab yetu kwa maslahi ya maisha ya sasa na ya baadae baada ya kuondoka hapau limwenguni,
Huyo lipumba na hao masheikh kuapishana na kwmba wampgie kura lipumba au cuf kwa maslahi yao kisiasa mwaka 2015 hiyo haina chcchte cha kufanya kipewe nafas ndan ya uislam na mustakabali wa waislam,CUF haijasema ikija madarakani basi itasimamisha sharia za kiislam ndan ya jamhuri hii,mimi siwapi like ya aina yyte katika hilo,
Ila kitu kikubwa hapo ni kwamba uislam na waislam hatutaweza kukaa kimya pindi tunapoona wanasiasa na siasa zao wanatuingilia kwenye mambo na taratibu zetu,we muslims,we are peaceful to somebody who is peaceful to us,torelant to someone who is torelant to us,we obey the law.,we serve god,we release regular charities n etc,but if somebody/someone puts his/her hand upon us intentionally we can send him/her to the cemetary...
Kwaiyo hao wanaoapishana na lipumba labda wawe wanaapishana kwa kuchelea masahibu yanayowakuta ndan ya nchi hii kwa kuwa kwao upande flan wa ushabiki wa siasa za chama fulani,kwaiyo kama wao wanaamin kwa kuwa upande huo wa chama cha siasa wanaweza kupata haki zao za kidunian ni wao kama wao,lakin tofaut na hapo uislam umetuweka wazi kabisa na namna ya kuyaendea maisha haya ya ulimwengu,samahani kama nitakuwa nakuhubiria dini...
Point yangu kuu ni kwamba UISLAM kwa ujumla wake hauhitaji siasa au wanasiasa ili uweze kusimama na kuish kwa ukamilifu wake,uislam unahitaji waislam walio committed kwa kufuata qur an na sunnah za mtume wetu s.a.w pekee,
Japo nakiri ya kwamba mifumo na tawala mbali mbali za kilimwengu zinachangia katika kuufanya uislam ukwazike au usikwazike kutokana na sera,miundo na maono ya vyama husika,
Tanzania daima iwe makini katika kuyaendea mambo ambayo yanagusa hisia wa watu moja kwa moja kabla ya kukimbilia kuyaandika na kuyareport,
Iangalie impact yake kichama,kitaifa na kimaono ya walio wengi pia,isiandike tuh ili iuze,hiyo haitakuwa na tija wala maana yyte.
Umeandika mengi sana, lakini kwangu mimi niliye ziona video za masheikh wenu wakubwa kabisa hapa Tanzania ambazo nadhani ndizo walizo ziona Tanzania Daima ambazo masheikh wenu wakikiri kuwa walikubaliana kuwa kura zote za waislamu apewe kikwete kwasababu ni mwislamu mwenzao kuliko Padri Slaa ambae amepanga akiingia madarakani atachukua raslimali za watu wa kusini na kuzipeleka nje ya nchi ukizingatia kusini wengi ni waislamu na baadae Lipumba alikri kufanya makubaliano hayo hata siku ya kwenda kuapishwa Kikwete alienda tu si kwa sababu hajui nini kilifanywa na masheikh laah hasha bali alienda kwa masilahi ya dini yake sasa basi kama tutaendesha nchi kwa namna hiyo tunalipoteza na tanzania Daima kama chombo chenye haki ya kukemea naona kipo sawa kwa swala hilo hata juzi kuna video hapa ililetwa ya Ole Medeye akiwaambia wamasai wenzake wawafukuze wachaga Arusha na kamwe wasikubali kuongozwa na wachaga kuanzia ubalozi,serikali za mitaa, ubunge, umeya... wamekemea lakini kama kuna vitu huwa vinatokea na wanavifumbia macho kwasababu labda kimefanywa na dini fulani au kabila fulani hapo issue nyingine....wewe ni kati ya waislamu mnao jitambua ndiyo maana unaweza kuona kuwa hata kama lipumba akija msikitini kwenu kuwaapisha unajua unacho kifanya kwa maana utaendelea na msimamo wako lakini je ni waislam wangapi wanao potoshwa na hao masheikh kwa kurubuniwa nakina Lipumba na kikwete...Je kwa swala hili ulitaka gazeti la Tanzania Daima waandike nini juu ya siasa hizo chafu!? wamekosea nini? ningeweza kuwaelewa kiasi kama matamshi hayo yange tolewa na kiongozi wa kidini lakini si kwa mwenyekiti wa chama tena msomi kama Prof. Lipumba...Vyombo hivi vikemee yote maovu bila kujali dini wala kabila....
Uchaguzi wa mwaka 2015 baada ya Kikwete kuwasaliti yaani kwenda kinyume na makubaliano yao ya mwaka 2010 baada ya kuzidiwa alimwita Lipumba na masheikh wakubwa akawaomba waokoa jahazi ili Parid slaa asiende magogoni ndipo wakaanza harakati za misikitini kuwa kura za cuf apigiwe Kikwete ilikura za waislmu wasizigawe na kumpa nafasi Padri wa chama cha vidole viwili akaenda ikulu ni bora kikwete maana zimwi likujualo halikuli likakumaliza lakini baada ya kikwete kuingia tena ikulu akawageuka waislamu wenzake ndipo Lipumba akaenda kumsemea msikitini tena na alizunguka nchi nzima makubaliano ilikuwa ni mahakam ya kadhi, OIC na nafasi za juu wapewe upendeleo waislamu lakini Kikwete akawaambie maaskofu wamekataa, huu ulikuwa unafiki mkubwa sana wa kikwete kwani walicho kisema maaskofu juu ya mahakama ya Kadhi ni kuwa grama za mahakama hizo zigaramiwe na waislamu wenyewe na siyo serikali na maaskofu hawana jeuri ya kuzuia dini furani isitimize guzo za imani yake maana hata wao sidhani kama wanaweza kwenda kuwauliza waislamu juu ya kushiriki ekaristi takatifu....ukishikisha ubong kwenye video hiyo utaona utumbo wa kikwete na lipumba....Uchaguzi upi huo? na kuna tatizo lipi hapo? Na hayo ni maneno ya Prof Lipumba?
Unanshangaza!
Usiogope kumwelimisha pengine iko siku atajiunga na mwanga......Madam samahani, sikujua ka nabishana na mnazi wa CUF, Kila la kheri ktk kujiokoa na kifo cha kisiasa, maana CDM hawa sio watu wazuri kabisa, wanakaba mpaka penati
Sasa hapo kibaya kipo wapi?mbona Chadema mnajenga kitu kibaya na kuonekana Mnadhamira nyengine dhidi ya uislam
Nimekusoma,nataka kuweka vitu wazi kabisa na watu wafaham uhalisia,
Uislam kama uislam ni mfumo uliokamilika kimaisha,,uislam hauwez kuwa subset ya siasa,bali siasa inaweza kuwa ni subset ndan ya uislam,
Uislam na sisi waislam hatuhitaji backup ya chama chochote kile ili tuweze kusurvive na kukamilisha mafundisho ya imab yetu kwa maslahi ya maisha ya sasa na ya baadae baada ya kuondoka hapau limwenguni,
Huyo lipumba na hao masheikh kuapishana na kwmba wampgie kura lipumba au cuf kwa maslahi yao kisiasa mwaka 2015 hiyo haina chcchte cha kufanya kipewe nafas ndan ya uislam na mustakabali wa waislam,CUF haijasema ikija madarakani basi itasimamisha sharia za kiislam ndan ya jamhuri hii,mimi siwapi like ya aina yyte katika hilo,
Ila kitu kikubwa hapo ni kwamba uislam na waislam hatutaweza kukaa kimya pindi tunapoona wanasiasa na siasa zao wanatuingilia kwenye mambo na taratibu zetu,we muslims,we are peaceful to somebody who is peaceful to us,torelant to someone who is torelant to us,we obey the law.,we serve god,we release regular charities n etc,but if somebody/someone puts his/her hand upon us intentionally we can send him/her to the cemetary...
Kwaiyo hao wanaoapishana na lipumba labda wawe wanaapishana kwa kuchelea masahibu yanayowakuta ndan ya nchi hii kwa kuwa kwao upande flan wa ushabiki wa siasa za chama fulani,kwaiyo kama wao wanaamin kwa kuwa upande huo wa chama cha siasa wanaweza kupata haki zao za kidunian ni wao kama wao,lakin tofaut na hapo uislam umetuweka wazi kabisa na namna ya kuyaendea maisha haya ya ulimwengu,samahani kama nitakuwa nakuhubiria dini...
Point yangu kuu ni kwamba UISLAM kwa ujumla wake hauhitaji siasa au wanasiasa ili uweze kusimama na kuish kwa ukamilifu wake,uislam unahitaji waislam walio committed kwa kufuata qur an na sunnah za mtume wetu s.a.w pekee,
Japo nakiri ya kwamba mifumo na tawala mbali mbali za kilimwengu zinachangia katika kuufanya uislam ukwazike au usikwazike kutokana na sera,miundo na maono ya vyama husika,
Tanzania daima iwe makini katika kuyaendea mambo ambayo yanagusa hisia wa watu moja kwa moja kabla ya kukimbilia kuyaandika na kuyareport,
Iangalie impact yake kichama,kitaifa na kimaono ya walio wengi pia,isiandike tuh ili iuze,hiyo haitakuwa na tija wala maana yyte.
Msituchanganye jamani mbona tulikuwa tunaishi maisha mema haya yametoka wapi?
mkuu,kwa hili nakubaliana nawe na ndivyo ilivyo kwa dini nyingine pia hata ukristo nao ni hivyo hivyo.kuna shida moja inatusumbua sana wanadamu.mie naweza kuitwa Juve,mkristo,kiongozi wa jamii,nikaamua kwa matakwa yangu kuitumia imani yangu kwa sapoti ya baadhi ya wendawazimu wenzangu ndani ya dini yangu,kupata sapoti ya wakristo wote ili kujinufaisha kisiasa.hii haina maana wakristo wote watakubaliana nami kwa vile tu ni mkristo mwenzao!na hii si sahihi,hivyo hawa wanaonipinga wanatenda haki na wanastahili sapoti ya umma wote hata wale wasio wakristo kwa sababu ngazi yangu kama kiongozi haishii kwa wakristo wenzangu tu na uongozi wangu naunadi kwa taswira ya dini yangu tu wakati si uongozi wa kidini,this is wrong na napaswa kukemewa LAKINI wale wanaokemea ni muhimu wakaelekeza ujumbe wao specifically kwangu na kikundi changu ndani ya ukristo na si ukristo wote.unapojumuisha ukristo wote,utaubebesha ukristo tatizo la mtu mmoja,utaiaminisha dunia na hasa wasio wakristo kwamba ukristo mzima unashiriki njama yangu,kwa hiyo utaibua tension ambayo haikupaswa kuwepo kabisa na utakuwa umetumika na mimi bila kujijua UNLESS tatizo langu lizungumzwe halafu ukristo ukae kimya bila kuchukua hatua na mamlaka ya nchi nilimo kama kiongozi nayo ikae kimya then hapo tuna haki ya kupata mashaka na kushutumu mfumo mzima na hatutakiwi kulikalia hili kimya na kwa muktadha huo nasema Tanzania daima wamefanya kazi yao.ni sisi wenye kiongozi wetu Lipumba na nchi yetu na dini zetu tuchukue habari hii na kuihakiki kwa kutazama elements hizo hapo juu,je,habari ikoje?bwana Lipumba kaongea hayo,je CUF wanazungumza au wamekaa kimya?je,dola imemhoji kama akina Mbowe au imekaa kimya?je,viongozi wa dini ya kiislam wanamzungumza au wamekaa kimya?je,waislam wanamzungumzia vipi huyu bwana na hoja zake?(kama wewe Big Show kama muislam umeshaeleza ya kwako,je wengine?)tukipata majibu haya then tutajua tuhangaike na nani anayeharibu nchi!mwisho naomba niseme,tuangalie kauli wanazotoa hawa viongozi wetu,kama yupo msikitini au kanisani na anazungumzia mambo ya msikitini na kanisani hamna shida,tutasema huyu si Lipumba au Juve wa kitaifa,lakini kama yupo msikitini au kanisani anazungumzia mambo ya utaifa pale,hapo tuhangaike nae!the case is vice versa kwa viongozi wa dini.kama Juve ni kiongozi wa dini,anatumia jukwaa la kitaifa kuzungumza mambo ya kitaifa kwa muktadha wa kazi yake kama mhubiri wa amani na upendo na ukosoaji wa jamii,hapo hakuna shida.lakini kama atatumia jukwaa la kitaifa kuzungumza mambo ya dini yake kama dini na si kundi la jamii linalo-exercise haki yake(kwa tafsiri sahihi ya neno HAKI),huyo nae tuhangaike nae!
Lakini mbona hukanushi contents za Tanzania daima kama ni kweli au za kutunga? Mbona unahamisha hoja kutoka kwenye maneno ya Lipumba msikitini na kuifanya hoja kuwa Tanzania daima? Ulitegemea habari hii waiandike Al- Nuur?
kashfa zaidi za mwenyekiti wa chama cha wananchi (cuf), profesa ibrahim lipumba kuendesha kampeni za kidini kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao zimezidi kuanikwa.
Wakati kashfa nyingine iliyomtuhumu kutoboa siri ya namna alivyofanya kampeni za kuwashawishi watu wa dini yake kumchagua aliyekuwa mgombea wa urais kupitia ccm kwa misingi ya kidini, ikiwa bado inarindima, lipumba anatuhumiwa kutoa maagizo kwa waumini wa kiislamu kuchagua mgombea wa dini hiyo mwaka 2015.
Mkanda wa video ulionaswa na tanzania daima unamuonyesha kiongozi huyo wa ngazi ya juu kabisa wa cuf akiwahamasisha waislamu kuungana na kushikamana kupigania haki zao za kiraia.
Katika mkanda huo uliorekodiwa katika msikiti wa mtambani jijini dar es salaam, mara baada ya swala ya ijumaa unamwonyesha profesa lipumba akiwataka waumini kupigania haki zao ambazo alisema kwa sasa hawazipati.
Lipumba aliwaambia waumini hao kuwa serikali imewatupa na kuwafanya waishi kama raia wa daraja la nne ndani ya nchi yao.
Kwenye mkanda huo wa video, profesa lipumba anasikika akiwataka waislamu kujipanga kikamilifu kisiasa ili kuzuia kile alichokiita uuzwaji wa nchi na rasilimali zake.
Alisema kuna mafisadi wamejipanga kuchukua nchi na kuiuza jumla huku wakiungwa mkono na watu ambao hakuwataja.
Alifafanua kuwa mafisadi hao wanaendesha biashara ya madisko inayoambatana na uchafu wa kila aina, biashara ya vileo na dawa za kulevya.
kwahiyo ndugu zangu waislamu tupo njiapanda katika nchi yetu. Tuna rasilimali kubwa zinazidi kugunduliwa, lakini siasa zetu zinazidi kuwa na matatizo na sisi waislam tupo chini. Utajiri huu unatolewa macho, wanahitajika watu ambao ni mafisadi waweze kushika nchi, na hao ndio wanaoungwa mkono washike nchi halafu waweze kuiuza nchi yote kwa ujumla.
kwahiyo, huu ni wakati wa kuwa macho kwamba tupo njiapanda. Hii neema, utajiri unaogunduliwa ikiwa hatutajipanga vizuri, neema hii itabadilika kuwa balaa, neema hii badala ya kumsaidia kila mtanzania aweze kuneemeka na neema hii, itageuka kuwa balaa dhidi yetu, alibainisha profesa lipumba.
Aliwaeleza waumini hao kuwa kwa sasa waislamu wanapaswa kushiriki kikamilifu katika harakati za siasa za nchi kama walivyoshiriki wazee wao wakati wa kudai uhuru.
kwamba kila mwananchi, kila mtanzania awe raia wa daraja la kwanza. Apate fursa ya uhuru wa dini yake, apate fursa ya kuelimishwa kwa kadiri ya uwezo ambao mwenyezi mungu amempa bila kubaguliwa, apate fursa ya kupata huduma bora za afya, apate fursa ya kushiriki kikamilifu katika uendeshaji wa serikali, apate fursa ya uendeshaji wa uchumi wa nchi yetu.
kazi ipo kwetu, na ndugu zangu sisi tunapozungumza hapa tumejitoa mhanga. Kwamba hii ni nchi yetu sote, tunamuogopa mwenyezi mungu tunamuogopa mwenyezi mungu na huu mwezi wa ramadhan, aliweka mkazo profesa lipumba.
Katika kusherehesha kauli ya profesa lipumba, mhadhiri wa kiislamu, ustaadhi said ricco alisema kuwa waendesha madisko aliowakusudia profesa lipumba ni mwenyekiti wa chadema, freeman mbowe, maelezo ambayo hayakukanushwa na kiongozi huyo wa cuf.
Katika hatua ya kushangaza, waumini waliohudhuria ibada hiyo walilishwa kiapo na ustaadhi ricco cha kuahidi kumpigia kura profesa lipumba katika uchaguzi mkuu wa 2015 ili awe rais wa tanzania, huku mwenyewe akishuhudia kitendo hicho bila kusema chochote.
Gazeti hili lilifanya juhudi za kumpata profesa lipumba ili atoe ufafanuzi wa kauli zake, lakini ilishindikana kutokana na simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani.
Hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi, hakuweza kujibu chochote.
Naibu katibu mkuu wa cuf tanzania bara, julius mtatiro alipoulizwa kuhusu kauli za mwenyekiti wake, alisema hajui chochote kwani huwa haambatani naye anapokwenda kusali misikitini.
mimi sijui chochote kwa sababu huwa siambatani naye misikitini, nakushauri umtafute yeye mwenyewe azungumze maana yeye ndiye aliyerekodiwa akitoa kauli hizo, siyo mimi mtatiro, alisema.
Lakini mtatiro alipokumbushwa jinsi alivyosimama kidete kumtetea lipumba katika tuhuma za awali kuhusiana na suala hilo la kampeni za kidini, na vipi sasa ashindwe kutoa kauli, kiongozi huyo alisisitiza kutoongea lolote, na kudai hayo ni masuala binafsi ya mwenyekiti wake na sio msimamo wa chama chao.
Hivi karibuni profesa lipumba alikaririwa akikiri kwamba alihamasisha kuunganisha nguvu kati ya ccm na cuf ili kumwezesha rais kikwete kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa kigezo cha udini.
Kashfa hiyo ambayo haijakanushwa na lipumba iliibua mjadala mkubwa, huku cuf wakijitahidi kumtetea bila mafanikio.
Aidha, licha ya video hiyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii, ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini haijawahi kusema lolote kuhusiana na suala hilo.
tanzania daima