Lijue tatizo jipya la kisaikolojia ambapo mtu aliyepata "mafanikio" kwenye maisha yake huamini kwamba watu wake wa karibu wanamchukia

WhatsApp kulikuwa na group la familia sasa ikapita donation kila mtu lazima achangie 30k ya msiba wa bibi,ukichangia lazima group admin atoe mkeka wa watu waliotoa pesa.
Sasa watu wengi walikuwa wanalega lega sana kutoa na mambo mengi pale msibani yalikuwa hayaendi vizuri,nikasema ngoja niokoe jahazi tusijepata aibu bure nikachangia laki 9 badala ya elfu 30,kama kawaida group admin akafanya yake akaweka mkeka kuwa bwana mdogo David ametoa laki 9.....ebaana eeh nilipigwa vijembe sio vya dunia..utasikia watu wengine kwa kupenda sifa ameambiwa atoe elfu 30 yeye ametoa laki 9,mwingine anakuja quotes ule ujumbe anasema watoto wa siku hizi wana dharau sana...daaah
 
Mzee Likud umeonyesha tu unamchukia kaka yako. Mengine uliyoandika ni kama kusindikiza tu hii habari ya kumchukia kaka yako. Kama kujenga ukweni na kusomesha ndugu wa mke ni ABOMINATION basi watu wengi sana wameshafanya hilo kosa. Hata mimi kama nitaoa familia fukara nitawasaidia ninachoweza. Wewe LIKUD bado ni mtu maskini na hela huna. Umekuwa ukitetea shule za Kayumba kwamba ni bora kuliko za binafsi kwa kua umepigika. Kutoka nje ya Afrika sio ishu kabisa. Ni suala la kawaida mno. Punguza chuki kwa ndugu yako.
 
ukijenga nyumba ukweni na kusomesha mashemeji lazima udharauliwe tu mkuu.

Tena kajenga nyumba mbili moja kwa baba mkwe ( kijijini) nyingine kwa mama mke( kijijini)

Source : Yeye mwenyewe anajisifu. Mtu kama huyu usipomdharau basi hutokuja kudharau mtu mwingine tena.
Amewajengea wakwe zake au amejijengea ya kwake ukweni?
 
Hao ndugu zako ni "wachawi", ingawa siwamaamishi wale wachawi "wengine".

Endelea na moyo huo hata katika mambo mengine. Bora uchukiwe kwa kutenda mema kuliko kusengenywa kwa sababu umetenda mabaya.
 
Mzee Likud umeonyesha tu unamchukia kaka yako. Mengine uliyoandika ni kama kusindikiza tu hii habari ya kumchukia kaka yako. Kama kujenga ukweni na kusomesha ndugu wa mke ni ABOMINATION basi watu wengi sana wameshafanya hilo kosa. Hata mimi kama nitaoa familia fukara nitawasaidia ninachoweza. Wewe LIKUD bado ni mtu maskini na hela huna. Umekuwa ukitetea shule za Kayumba kwamba ni bora kuliko za binafsi kwa kua umepigika. Kutoka nje ya Afrika sio ishu kabisa. Ni suala la kawaida mno. Punguza chuki kwa ndugu yako.
ur a poor judge of character
 
WhatsApp kulikuwa na group la familia sasa ikapita donation kila mtu lazima achangie 30k ya msiba wa bibi,ukichangia lazima group admin atoe mkeka wa watu waliotoa pesa.
Sasa watu wengi walikuwa wanalega lega sana kutoa na mambo mengi pale msibani yalikuwa hayaendi vizuri,nikasema ngoja niokoe jahazi tusijepata aibu bure nikachangia laki 9 badala ya elfu 30,kama kawaida group admin akafanya yake akaweka mkeka kuwa bwana mdogo David ametoa laki 9.....ebaana eeh nilipigwa vijembe sio vya dunia..utasikia watu wengine kwa kupenda sifa ameambiwa atoe elfu 30 yeye ametoa laki 9,mwingine anakuja quotes ule ujumbe anasema watoto wa siku hizi wana dharau sana...daaah
Duh pole sana mkuu
 
Familia yenu imejaa malimbukeni wengi sana

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Binafsi sikubaliani na hoja yako!

Na mimi ntatoa tu mfano mmoja kati ya michache niliyonayo...!

Nimezaliwa na kukulia Uswahilini, kama unavyojua Uswahili huwa kuna Vijiwe tofauti tofauti, ambavyo uhusisha watu wanaofahamiana, yani Mtu ataenda Mishe zake, ama mihangaiko yake, na ikifika mida flani unakuta kijiwe kimejaa, hawa wakipiga story hizi hapa, hawa wanaongea kuhusu hili n.k...!

Nilikua miongoni mwa Vijana wadogo kwenye Kijiwe hiki, na wengi wao walikua Ma brother!

Kuna siku anapita Brother akiwa na Usafiri, ndo Usafiri wake wa kwanza, kapaki kijiweni akashuka na kusalimia kila mtu, baadaye akaanza kumwambia Brother mwingine ambaye alikua Best yake sana, kwamba mbona hawatafutani, amtafute basi wapeane michongo, jamaa akamwambia u busy ndo unachangia (Japo hakuwa na issue yoyote, kula kulala).

Brother mwenye gari anamwambia yeye anaenda kumcheki Bi mkubwa wake kama vipi aje home kwao, jamaa akamwambia soon atakuja, basi yule Brother mwenye usafiri akaondoka, Kijiweni wakaanza kumjadiri, kwamba anafanya issue gani mpaka kanunua gari!?

Mwingine akaleta taarifa kijiweni tu kuwa sio gari tu, kanunua na Nyumba Mbezi Beach!

Mmoja akamwambia yule best yake wa muda mrefu kuwa aende home kwao, si kaambiwa kuwa atapewa Mchongo, jamaa akajibu "Aaah, siendi, ataona kama najikomba kwake..!"

Nikashuhudia mara nyingi jamaa akipita kijiweni kwenda kumsalimia Bi. Mkubwa wake lazima asimame ashushe Kioo cha gari asalimie, lakini kuna Mabrother pale kijiweni wengine wanajifanya hawajamuona au kusikia salamu yake, akipita yanaanza maneno, Jamaa atakua anajiskia sana sasa hivi n.k..!

Baada ya yule Brother kugundua kwamba watu pale Maskani ya Mtaa ambao amezaliwa kama vile hawajari hata salamu yake, akawa akipita anapiga tu Hodi... Mwendo.... Baadaye akawa hata Honi hapigi, anapita zake tu kwenda kumcheck Bi. Mkubwa wake...!!

Kuna watu hasa Waswahili mtu wa karibu akipiga hatua, wao ndo wanakua wa kwanza kujiweka mbali nae, halafu huku pembeni wanaanza kuongea maneno yasio na maana!!!

Badala ya kuendelea kuwa karibu nae ili kupata maujanja how come from no where jamaa kapata pesa....!

Na watu ambao wanajiweka mbali nawe, na wewe kaa mbali nao, coz ukilazimisha, wanaweza kukushusha kwa njia zozote zile ili muendelee kuwa level moja...!
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Wewe unaesoma Uzi huu bila shaka :

1. Umewahi KUKUTANA na mtu mwenye tatizo kama hili. Au

2. Wewe mwenyewe una tatizo hilo ila hujui kama upo nalo.

Tatizo hili mara nyingi humkuta mtu ambae amepiga hatua kidogo kwenye maisha au amepata breakthrough kiuchumi jambo ambalo yeye analitafsiri kama mafanikio..

Mtu huyu ataanza kuamini kwamba watu waliomzunguka hususani watu wake wa karibu ambao yeye ana amini amewazidi ki maisha, wanamchukia ama wanamuonea wivu and he will start to act and behave accordingly.

Ninayo mifano hai miwili:

1. Mpangaji wetu mwaka 2003.

Huyu jamaa alikuwa ndo kamaliza shule pale udsm. Alikuja kupanga nyumbani kwetu. Mwanzoni maisha yake yalikuwa magumu sana alikuwa analala chini na alidumu katika hali hiyo for almost 2 months. Mbaya zaidi wapangaji wenzake walikuwa wanamtangaza kwa watu kwamba analala chini.

Alipopiga buu baa alinunua gari halafu pale kwenye chumba na sebule alichopanga akaweka tv Kali fenicha na Mziki mnene..

Mbaya zaidi akawa anapiga muziki kwa sauti ya juu. Wapangaji wenzake wakimwambia apunguze sauti akawa anawafanyia ukaidi. Wakamshitaki kwa mshua( baba mwenye nyumba) ambae yeye alikuwa haishi hapo.

Mshua alipozungumza na jamaa, jamaa akasema wanamuonea wivu tu.

Baada ya tabia ya jamaa kuendelea mshua akampa notice. Jamaa kaondoka na kwenda kupanga sehemu nyingine huku akiwa ana amini kwamba amefukuzwa kwenye nyumba kwa sababu watu wanamuonea husda " mafanikio" yake na sio kwa sababu ya usumbufu wake kwa majirani.

Mfano wa pili: my own brother.

1. He is my own brother from the SAME -FATHER MOTHER.

2. Tumezaliwa tumbo moja ila mimba mbalimbali.

3. He is the first born in our family. He was born in the 70s. Mimi namfuata mara ya 5 am the last born in the family.

4. Alikuwa mtu wa kwanza kwenye familia yetu na partly kwenye ukoo wetu;

I. Kufika chuo kikuu
ii. Kununua gari.
Iii. Kutoka nje ya Tanzania ( sio nje ya Afrika/ hajawahi toka nje ya Afrika).

iii. Kujenga nyumba.

iv. Kujenga nyumba ukweni( he will be the first and the last to do this kind of abomination)

Kwa sababu hiyo jamaa kwa muda mrefu sana amekuwa akiamini sana kwamba yeye ndio mtu mwenye mafanikio kuliko watu wote kwenye familia yetu na partly ukoo wetu.

Na amekuwa aki behave accordingly. Hata tembea yake akija kwenye vikao na matukio ya familia na ukoo huwaga anatembea kama mtu ambae ametoka kucheza mpira wa ndondo amechoka jambo ambalo tafsiri yake kisaikolojia ni kwamba anaamini ameshayamaliza na kwamba nyinyi watu wengine mnacheza...

Watu wanamchora wanamuona to bishoo kwa sababu some of us have more money than him.

Kama wewe unaesoma Uzi huu upo kwenye kundi hilo please wacha mara moja tabia hiyo kwa sababu mwisho wa siku watu wenye tatizo hili huwaga wanaishia kuwa wachawi hasa pale unapoona watu ambao unadhani wewe unapesa kushinda wao, wana mafanikio makubwa kushinda wewe and they dont act strangely as you do.

Ogopa sana mchawi wa namna hii kwa sababu yupo tayari hata kuchinja n'gombe mmoja kila siku ili usifanikiwe...
Mafanikio yanaonyesha tabia yako halisi ambayo inafichwa na dhiki/shida.
 
Binafsi sikubaliani na hoja yako!

Na mimi ntatoa tu mfano mmoja kati ya michache niliyonayo...!

Nimezaliwa na kukulia Uswahilini, kama unavyojua Uswahili huwa kuna Vijiwe tofauti tofauti, ambavyo uhusisha watu wanaofahamiana, yani Mtu ataenda Mishe zake, ama mihangaiko yake, na ikifika mida flani unakuta kijiwe kimejaa, hawa wakipiga story hizi hapa, hawa wanaongea kuhusu hili n.k...!

Nilikua miongoni mwa Vijana wadogo kwenye Kijiwe hiki, na wengi wao walikua Ma brother!

Kuna siku anapita Brother akiwa na Usafiri, ndo Usafiri wake wa kwanza, kapaki kijiweni akashuka na kusalimia kila mtu, baadaye akaanza kumwambia Brother mwingine ambaye alikua Best yake sana, kwamba mbona hawatafutani, amtafute basi wapeane michongo, jamaa akamwambia u busy ndo unachangia (Japo hakuwa na issue yoyote, kula kulala).

Brother mwenye gari anamwambia yeye anaenda kumcheki Bi mkubwa wake kama vipi aje home kwao, jamaa akamwambia soon atakuja, basi yule Brother mwenye usafiri akaondoka, Kijiweni wakaanza kumjadiri, kwamba anafanya issue gani mpaka kanunua gari!?

Mwingine akaleta taarifa kijiweni tu kuwa sio gari tu, kanunua na Nyumba Mbezi Beach!

Mmoja akamwambia yule best yake wa muda mrefu kuwa aende home kwao, si kaambiwa kuwa atapewa Mchongo, jamaa akajibu "Aaah, siendi, ataona kama najikomba kwake..!"

Nikashuhudia mara nyingi jamaa akipita kijiweni kwenda kumsalimia Bi. Mkubwa wake lazima asimame ashushe Kioo cha gari asalimie, lakini kuna Mabrother pale kijiweni wengine wanajifanya hawajamuona au kusikia salamu yake, akipita yanaanza maneno, Jamaa atakua anajiskia sana sasa hivi n.k..!

Baada ya yule Brother kugundua kwamba watu pale Maskani ya Mtaa ambao amezaliwa kama vile hawajari hata salamu yake, akawa akipita anapiga tu Hodi... Mwendo.... Baadaye akawa hata Honi hapigi, anapita zake tu kwenda kumcheck Bi. Mkubwa wake...!!

Kuna watu hasa Waswahili mtu wa karibu akipiga hatua, wao ndo wanakua wa kwanza kujiweka mbali nae, halafu huku pembeni wanaanza kuongea maneno yasio na maana!!!

Badala ya kuendelea kuwa karibu nae ili kupata maujanja how come from no where jamaa kapata pesa....!

Na watu ambao wanajiweka mbali nawe, na wewe kaa mbali nao, coz ukilazimisha, wanaweza kukushusha kwa njia zozote zile ili muendelee kuwa level moja...!
True masikini mara nyingi tunajishtukia sana
 
WhatsApp kulikuwa na group la familia sasa ikapita donation kila mtu lazima achangie 30k ya msiba wa bibi,ukichangia lazima group admin atoe mkeka wa watu waliotoa pesa.
Sasa watu wengi walikuwa wanalega lega sana kutoa na mambo mengi pale msibani yalikuwa hayaendi vizuri,nikasema ngoja niokoe jahazi tusijepata aibu bure nikachangia laki 9 badala ya elfu 30,kama kawaida group admin akafanya yake akaweka mkeka kuwa bwana mdogo David ametoa laki 9.....ebaana eeh nilipigwa vijembe sio vya dunia..utasikia watu wengine kwa kupenda sifa ameambiwa atoe elfu 30 yeye ametoa laki 9,mwingine anakuja quotes ule ujumbe anasema watoto wa siku hizi wana dharau sana...daaah
Yaani kukosa pesa ndio chanzo cha matatizo ya afya ya akili
 
Mimi Sina maneno mengi ila wahenga wetu hawakukosea.

Mchumia ukweni, urudi na deni.

Hivyo kaka hizo Nyumba mbili sio za kwake Wala watoto wake.

Wakiachana leo na mkewe, yeye atapata thamani ya Nusu Nyumba ya mjini wakati automatic mkewe atakuwa na Nyumba mbili na Nusu.

Kuhusu elimu ni ukweli unamwonea kijicho
Na hili lipo wazi.
 
Ulivyoandika tu inaonesha dhahili unamchukia, sasa wewe Hadi kutembea unampangia atembee vipi? Acheni makasiriko na maisha ya watu...! Na hapo ulipo unaomba muda wowote limkute baya ili upate la kusema......si tulisema? Kiko wapi??
 
Brother, I will never try to kill a Judas knowing that he will end up hang himself.

Siwezi kumfuatilia kwa chochote cause I don't like his behaviour.

Kuhusu kutowahi kutoka nje ya Afrika hilo ndilo limemfanya anichukie mpaka leo kwa sababu Mimi nimewahi toka nje ya Afrika mara nyingi na sijaenda kimasomo.

Nimeenda nje ya Afrika before him so amejenga chuki kwa sababu aliamini yeye ndo alipaswa kuwa ameenda abroad before me.

Niliposikia kajenga ukweni kwao nilijisikia vibaya sana na Mimi nikajenga nyumba nje ya mji nikawapa zawadi wazazi wangu baba na mama waishi. Pamoja na kwamba baba na mama hawakuwa na shida ya nyumba lakini nilifanya hivyo kuwapa ile faraja " mtoto wetu katujengea nyumba"

He is hating on me for that mkuu haongei na Mimi toka 2019.

Ndio maana nikasema ukisha kuwa na hii mentality ya kudhani kwamba wewe umefanikiwa kushinda watu wengine na kwamba they envy on you u can end up being a witch when u realize that they are actually richer than you and they dont give a inch about you.

Kuna tajiri mmoja maarufu jijini Dar anatoka mkoa jina siutaji yeye ana ofisi kubwa sana hapo mjini. Na yeye ana tabia hii.

Yeye alicho kifanya ni kuwafunga ndugu zake wote walio Soma au wanao pambana kutoka.

Kuwafunga vipi?

Kawaajiri kwenye biashara na makampuni yake. Maana yake ni kwamba yeye ndo anaamua wapate hela kiasi gani kwa mwezi.

Ukionekana umepiga hatua kidogo kimaendeleo anasema unamuibia.

Mkuu Mimi kwa filosofi yangu ya maisha ni ngumu mno kumuonea wivu mtu kwa sababu naamini kwa vitendo:

1. Duniani tunapita( duniani tupo stendi)

2. We did not create this world it was rather given to us or forced upon us.

Yani nimuonee wivu wa kimaendeleo mtu ambae nimekutana nae stendi.
We na kaka yako acheni utoto
 
ukijenga nyumba ukweni na kusomesha mashemeji lazima udharauliwe tu mkuu.

Tena kajenga nyumba mbili moja kwa baba mkwe ( kijijini) nyingine kwa mama mke( kijijini)

Source : Yeye mwenyewe anajisifu. Mtu kama huyu usipomdharau basi hutokuja kudharau mtu mwingine tena.
Kwanini kujenga ukweni ni vibaya mkuu? Mimi nina mpango huo siku za mbeleni maana kwetu mambo 'safi kiaina' ila mke wangu akienda kwao mpaka najisikia vibaya wanapolala watoto wangu maana ni nyumba mbavu za mbwa. Kuna ubaya gani nilijenga nyumba ndogo ya 15m Kwa mfano. Maana kwao hakuna mwenye uwezo wa kufanya hivyo....
 
Naskia ukifanikiwa unakua unadhani watu hawakuthamini tena, wanaishi na wewe kinafki ili wafaidi pesa zako.

Ndo maana wanasema 'It's lonely at the top'
Kuwa na fedha mfukoni ni kitu kingine kabisa. Kwa wanaume ni rahisi zaidi kujua hili. Ukiwa na fedha mfukoni unaweza kuwa na confidence ya kufa mtu na ukamwa-approch demu mkali sana. Au kwenye kikao unaweza kuwa na ujasiri wa kuwa mzungumza mkuu. Ukikosa fedha sasa... demu yule yule utamuona kama anadharau na hutathubutu hata kutoa salaam. Kikao ndiyo kabisa mtu anajificha na anaona aibu...
 
Back
Top Bottom