Hakuna chochote cha kupigania katika maisha

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,404
Nguo zako zile bora kabisa kuna mtu kwake ni matambara tu.

Akiba yako kwenye akaunti ya Benki ni sawa na mchango wa mtu katika sherehe tu.

Boyfriend au Girlfriend wako au mchumba ni Ex wa mtu!

Hivyo ni nini hasa cha kujivunia?

Maisha ni mafupi sana na madogo mno kujisikia kuwa mkubwa ama bora kuliko mtu wengine.

"Tupo sote uchi hadi kufa" aliwahi kusema Steve Jobs. Gwiji muanzilishi wa iPhone(ambaye kwa sasa kifo kimemchukua kwa maradhi ya Cancer)

"Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa sote Kukabiliwa na kifo".

Naumia kuona watu ambao hujivunia utajiri, uzuri, akili, kiwango cha elimu, umaarufu na vitu vingine vya tamaa za kimwili, kwani hakuna jambo umefanya la mafanikio katika maisha yako ambamo halijafanywa na mtu mwingine ama kupitia

Cheo unachomiliki ofisini leo kilikuwa kinamilikiwa na mtu mwingine kabla na kitatwaliwa na mtu mwingine baadaye, wala hujui mtu huyo anaweza kuwa nani

Kuna jambo moja tu la thamani la kujivunia ambalo ni "MAISHA ndani ya Mwenyezi MUNGU Muumba".

HIVYO ni vema kuwa mwema kwa Jamaa zako na daima tengeneza Marafiki!

Daima kumbuka kwamba watu unaowakanyaga wakati ukiwa njiani kukwea ngazi kwenda juu huenda wakawa ni walewale utakaowakuta kwenye safari yako ya kuteremka ngazi

Hivyo jitahidi usiwe tatizo kwa watu wengine au kufanya maisha magumu kwa mwingine kwa kutumia nafasi yako, kwa sababu kwa wewe kufanya hivyo ipo siku watu hao hao wanaweza kuwa kikwazo kwako siku moja mbeleni.

Kumbuka,hata jani la mgomba wa ndizi kuna siku litanyauka na kuwa majani makavu yasiyo na ukijani tena!

Tafadhali usiwe na Ubinafsi, Wajulishe marafiki wengine kuwa sote tupo njia moja.

Kama siku moja utajisikia kulia, niite. Sina ahadi ya kukufanya ucheke lakini naweza kulia na wewe.

Kama siku moja unataka kukimbia kwenda mbali usiogope simu yangu.Niite nami nakuahidi kukimbia bega kwa bega na wewe!

Lakini, kama siku moja utapiga simu yangu na haina majibu basi njoo kwangu, Huenda nakuhitaji wewe.

Siku moja, mmoja wetu hatutakuwa naye hapa tena na utasikitika juu yake lakini ukiwa umechelewa kwani hutokuwa na nafasi hiyo tena!

Machozi yanaweza kukutoka!, lakini itakuwa umechelewa. Kwa hiyo, mkumbushe na kumwambia kila mtu kama vile ambavyo mimi nimefanya!

Tuma kwa marafiki zako na wapendwa bila kujali mara ngapi unazungumza nao au ukaribu wenu.

Nini maoni yako?
 
Akiba yako kwenye akaunti ya Benki ni sawa na mchango wa mtu katika sherehe tu.

Boyfriend au Girlfriend wako au mchumba ni Ex wa mtu!

".

Naumia kuona watu ambao hujivunia utajiri, uzuri, akili, kiwango cha elimu, umaarufu na vitu vingine vya tamaa za kimwili, kwani hakuna jambo umefanya la mafanikio katika maisha yako ambamo halijafanywa na mtu mwingine ama kupitia

Cheo unachomiliki ofisini leo kilikuwa kinamilikiwa na mtu mwingine kabla na kitatwaliwa na mtu mwingine baadaye, wala hujui mtu huyo anaweza kuwa nani

Kuna jambo moja tu la thamani la kujivunia ambalo ni "MAISHA ndani ya Mwenyezi MUNGU Muumba".

HIVYO ni vema kuwa mwema kwa Jamaa zako na daima tengeneza Marafiki!
Kaka kuhusu mpenzi Eti ni x wa mtu, hii chai, kwani mi mpiga nyeto tu- au ndo mkono wangu ilikuwa mkono wa mtu pia🤣😂.

Haya Eti akiba ya benki ni mchango wa harusi kwa mtu, zile hela za bhakhresa ushaona kapewa nani Kama mchango 🤣😂.

Kaka Mimi ni jobless pro max, nani kaumiliki u Jobless wangu🤓
 
Wewe una urithi wa mijengo Kariakoo mtaa wa Congo 🤣🤣🤣
 
Anko Manyanza , sote tunajua kuwa ipo siku tutakufa. Lakini tunapaswa kuishi na kutenda kana kwamba hakuna kifo! Binadamu ukiwazia sana kuhusu kifo, kuna mambo hautayafanya, au utafanya mambo ya kisengerenyuma (kama kujijengea kaburi). Ni bora kutenda kwa kiwango cha juu cha ubinadamu wako ukiwa hai, bila kujali baada ya kifo utapokelewa wapi..!!!
 
Anko Manyanza , sote tunajua kuwa ipo siku tutakufa. Lakini tunapaswa kuishi na kutenda kana kwamba hakuna kifo! Binadamu ukiwazia sana kuhusu kifo, kuna mambo hautayafanya, au utafanya mambo ya kisengerenyuma (kama kujijengea kaburi). Ni bora kutenda kawa kiwango cha juu cha ubinadamu wako ukiwa hai, bila kujali baada ya kifo uapokelewa wapi..!!!
Uko wapi kesho tule futari pamoja ?
 
Back
Top Bottom