Leonardo Da-Vinci

Leonardo Da-Vinci

Labda nikuulize
Una ushahidi wa haya madai yako?

Yapo lakini hayayafanyi madai yako kuwa kweli!

Hapana!

Hebu leta hizi document!

Hapa unatakiwa ujue kutofautisha mambo ya kawaida na neno la Mungu
Neno la Mungu ni yeye mwenyewe anaelisimamia,hivyo kuwa makini sana na hii kitu!

Unajuaje kuwa neno hili ni la mungu na hili ni la mwanadamu ktk biblia?
 
kuna baaadhi ya wakristo hawapendi kabisa kuhoji mambo ya kanisa na imani kwa ujumla hata ukimwambia vinginevyo hataki hata kukubali hata kama ni kweli. mimi ni mkristo lakini nimejiruhusu kuhoji kila ninapoona inahitajika kufanya hivyo. na kamwe kuhoji kwangu hakutawahi kuja kunivunjia imani yangu juu ya mungu ila kuna imarisha kila siku. ila kila siku ninapohoji juu ya makanisa na taratibu za kuaabudu za makanisa huwa napata tabu sana kuziamini baadhi ya taratibu. ambazo zimejengwa na watu kama mimi na wewe. na kila mmoja akisema ndio taratibu sahihi au kafunuliwa na mungu kufanya hivyo.

imeandikwa tuitafute kweli nayo itatuweka huru.
kama watu wanaogopa kuhoji hiyo kweli itapatikana wapi?
kama kanisa linawaficha watu mambo fulanifulani je hiyo kweli itapatikana wapi?
kama kanisa linawaona wanaohoji wamepotoka je hiyo kweli itapatikana wapi?

BIG UP SANA MKUU hayo ndo yanayotutofautisha binadamu na viumbe wengine. Ndo maana mungu ametupa akili ili tuchanganue mambo
 
Mkuu kuna hii documentary inaelezea jinsi biblia ilvyo tengenezwa icheki kaka tuje tushee understandings "banned from the bible"

Mkuu,kuna hadithi nyingi sana ambazo zinaelezea "utengenezwaji wa biblia" hii ina kipi ili misipoteze muda tu?
 
Kaka unajua Kuwa biblia agano jipya lilikuwa compiled kwa initiative ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara ambaye ni mchamungu na yeye ndo aloanzisha mchakato wa kutengeza biblia agano jipya na yeye na watu wake ndo walokuwa na uamuzi kipi kiwekwe na kipi kisiwekwe inasemaekana baada ya kifo cha yesu viliandikwa vitabu vingi sana na waandishi wengi mmoja wao ni Mary Magdalene kitabu chake hakikuzingatiwa kwa kipindi kile ni sababu ya mtazamo wa jamii ya enzi izo towards wanawake. Siyo maneno yangu mkuu na mie nimepitia pitia hizi documentariea na google.

Una hakika kuwa haya unayosema ni kweli?
Ushahidi uko wapi kuthibitisha ukweli wa haya?
 
Dah! Kweli hii ishu ngumu, yani we huoni tatizo hapo. Hebu jiulize we utengeneze robot lako ambalo kila linachofanya we ndo unaliongoza halafu likuue wewe unaejua siri zake halafu useme hakuna tatizo? Ndugu yangu mi nashindwa kuelewa uwezo wako wa kufikiri.

Inawezekana wewe Mungu unaemjua wewe ni tofauti na wangu

Halafu ninavyojua mimi hadi mungu awe Mungu ni pale ambapo hakuna kinachomshinda,kaka mungu wako wewe hawezi kuwa mwanadamu basi anakosa sababu ya kuwa Mungu kwasababu kuna mambo yanamshinda

Mungu wangu anajua na kuweza kula kitu ndio maana akawa mwanadamu na kuja kula kulala na sisi na hiyo ni ishara ya upendo mkubwa sana kwetu!
 
Kaka unajua Kuwa biblia agano jipya lilikuwa compiled kwa initiative ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara ambaye ni mchamungu na yeye ndo aloanzisha mchakato wa kutengeza biblia agano jipya na yeye na watu wake ndo walokuwa na uamuzi kipi kiwekwe na kipi kisiwekwe inasemaekana baada ya kifo cha yesu viliandikwa vitabu vingi sana na waandishi wengi mmoja wao ni Mary Magdalene kitabu chake hakikuzingatiwa kwa kipindi kile ni sababu ya mtazamo wa jamii ya enzi izo towards wanawake. Siyo maneno yangu mkuu na mie nimepitia pitia hizi documentariea na google.

Tatizo la Eiyer hataki kuamini Biblia yote imeandikwa/andaliwa na kanisa Katoliki....Yani namshangaa sana..kama haamni Vatcan ni vyema pia angetupa hiyo Biblia yake mbali...
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la Eiyer hataki kuamini Biblia yote imeandikwa/andaliwa na kanisa Katoliki....Yani namshangaa sana..kama haamni Vatcan ni vyema pia angetupa hiyo Biblia yake mbali...

Hivi unajua kanisa Katoliki halikuwepo wakati Yesu anapaa kwenda mbinguni?

Hivi unajua kuwa kanisa Katoliki halikuwepo karne ya kwanza?
 
Hivi unajua kanisa Katoliki halikuwepo wakati Yesu anapaa kwenda mbinguni?

Hivi unajua kuwa kanisa Katoliki halikuwepo karne ya kwanza?

Huenda Kanisa lililokuwa linajulikana kwa jina kama "Katoliki" ni kweli lilikuwa halipo kipindi hicho....LAkini taratibu zilikuwepo...Maaana kanisa lilianza kuenea sana maeneo mengi ya ulimwengu wakaamua kuliita Catholi..(Universla),,,,,Iliyo enea...Rejea maana ya Catholic kwa ki-Giriki ndo utajua maana..

Kama unasemea kanisa kwa jina sawa..

Anyway!! Wewe ni mjuaji...Nimekubali kuwa mimi sijui naomba nijuze hapa sasa hivi "kanisa gani lilikuwa karne ya kwanza"? Utaratibu wao wa kuabudu ulikuwaje....? Baada ya kupaa KAnisa gani lilikuwa...? Tafadhali nijuze sitaki porojo..
 
Kama walikuwa na uwezo wa kuandika biblia how do you think wanashindwa kuficha familia ya yesu? Biblia yenyewe inajicontradict kwenye maisha ya yesu kuanzia ukoo wake, maisha yake, kukamatwa kwake, kufa kwake, kufufuka kwake na mwisho kupaa kwake kwenda mbinguni. So kwa wenye akili na wanaotaka kujua ukweli juu ya ukristo lazima wataibuka na maswali mengi ambayo yanasababisha mtu kutoiamini biblia na hivyo kuifanyia utafiti. Yesu alikuwa myahudi lakini historia yake inapatikana zaidi ktk lugha tofauti na za kiyahudi the question is still there WHY???

Jamani tuseme mara ngapi Biblia haikuandikwa na mtu? Hapakuwa na kikao au kazi ya kuandika Biblia. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali tena wengine kwa malengo ambayo kabla hawakujua yangeweza kuwa Biblia. Waandishi hawa walivuviwa na Roho Mtakatifu na kujikuta wakinakili ujumbe wa Mungu kwa wanadamu kwa njia ya ya Roho Mtakatifu. Sasa hapa inabidi mtu uanze na kujua Roho Mtakatifu ni nani, anafanyaje kazi kupitia wanadamu, nk.

So far hakuna contradiction yoyote ya msingi kuhusu kuzaliwa, maisha na kufa kwa Yesu Kristo. Kama ipo iweke mezani
 
Huenda Kanisa lililokuwa linajulikana kwa jina kama "Katoliki"
Hii sentensi yako iko sawa kweli?
ni kweli lilikuwa halipo kipindi hicho....LAkini taratibu zilikuwepo...Maaana kanisa lilianza kuenea sana maeneo mengi ya ulimwengu wakaamua kuliita Catholi..(Universla),,,,,Iliyo enea...Rejea maana ya Catholic kwa ki-Giriki ndo utajua maana..
Kwa mtazamo wako Wakristo wa kwanza walikua wanasali kama Wakatoliki?
Hivi unajua kiongozi wa kwanza wa kanisa Katoliki alikuwa mwaka gani?

Unajua neno Papa lilianza kutumika mwaka gani?

Hebu nijibu kwanza hayo
Kama unasemea kanisa kwa jina sawa..
Kibiblia neno kanisa lina maana zaidi ya moja sijui wewe unazungumzia ipi
Anyway!! Wewe ni mjuaji...
How do you know this?
Nimekubali kuwa mimi sijui naomba nijuze hapa sasa hivi "kanisa gani lilikuwa karne ya kwanza"? Utaratibu wao wa kuabudu ulikuwaje....? Baada ya kupaa KAnisa gani lilikuwa...? Tafadhali nijuze sitaki porojo..
Utaratibu wa kumuabudu Mungu wa kanisa la kwanza ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli baasi

Soma matendo ya Mitume utajua haya yote!
 
Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu ..!!

Hapo napo ndo nashindwa kuwaelewa maana hilo ndo kimbilio la watu wavivu wa kufikiri. Hamtaki kuchambua mambo kwa kisingizio cha roho mtakbtifu kwamba ili mtu aijue biblia na aielewe lazima awe na roho mtakatifu. Sitaki nikuulize kama unamjua huyo roho mtakatifu kiundani au unamjua juu juu tu kwa maana hiyo ni mada nyingine ya kujadili kirefu. Anyway nikuache kwa leo maana umejitahidi sana kujieleza na kujibu kulingana na uelewa wako hoja mbalimbali ambazo watu wamekulenga wewe. Nakupongeza kwa hilo but one thing to remember is that fungua macho na moyo wako so that you can learn kuhusu dini zote and be free in what you beleave. Utakuwa na uhakika na kile unachokiamini kuliko kung'ang'ania imani ambayo haikupi uhuru wa kuichallenge na imani nyingine. Hapa ninachokushauri ni kusoma basics zake tu. You'll be free.
 
Jamani tuseme mara ngapi Biblia haikuandikwa na mtu?. Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vilivyoandikwa na watu mbalimbali tena wengine kwa malengo ambayo kabla hawakujua yangeweza kuwa Biblia. Waandishi hawa walivuviwa na Roho Mtakatifu na kujikuta wakinakili ujumbe wa Mungu kwa wanadamu kwa njia ya ya Roho Mtakatifu. Sasa hapa inabidi mtu uanze na kujua Roho Mtakatifu ni nani, anafanyaje kazi kupitia wanadamu, nk.
So far hakuna contradiction yoyote ya msingi kuhusu kuzaliwa, maisha na kufa kwa Yesu Kristo. Kama ipo iweke mezani

Ngoja nikupe contradiction 1 tu kuhusu kukamatwa kwa yesu halafu uniambie roho mtakatifu wako wangapi. Mathayo 26:48. Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara akisema nitakeyembusu huyo ndiye; mkamateni. Yohana 18:4. Basi yesu hali akijua yote yatakayompata, akatokea akawaambia ni nani mnayemtafuta? Sasa nani yuko sahihi kati ya mathayo na yohana juu ya kukamatwa kwa yesu? Nani alikuwa na roho mtakatifu wa kweli kati yao? Jibu kwanza hayo.
 
Hii sentensi yako iko sawa kweli?

Kwa mtazamo wako Wakristo wa kwanza walikua wanasali kama Wakatoliki?
Hivi unajua kiongozi wa kwanza wa kanisa Katoliki alikuwa mwaka gani?

Unajua neno Papa lilianza kutumika mwaka gani?

Hebu nijibu kwanza hayo

Kibiblia neno kanisa lina maana zaidi ya moja sijui wewe unazungumzia ipi

How do you know this?

Utaratibu wa kumuabudu Mungu wa kanisa la kwanza ni kumuabudu Mungu katika roho na kweli baasi

Soma matendo ya Mitume utajua haya yote!

Wewe sijui ni.mtu wa aina gani......Unaponiuliza swali "hivi unajua".....Maana yake umejiridhisha mimi sijui....Sasa ni jukumu lako wewe kunijuza....

Sijaongelea mambo ya Pope lakini naona umeongelea....Vipi unawazimu nini...??? Rejea maana ya neno Papa ujue...Ni neno la kawaida kabisa likimaanisha (Baba)... Kwa hiyo swala la kuanza sijui kutumika lini hilo halina tabu.....

Hiyo roho na kweli ni ipi...??? Kama ni kusoma nimesoma hayo maandiko.....

Nilichogundua ni kuwa wewe hujui kitu chochote zaidi ya kuuliza maswali mengi yasiyo na msingi ili uonekane unajua....Anyway ni defensive mechanism yako...

Uliambiwa upitie hints usome sidhani kama hata ulisoma.....

Kingine nilichogundua kuhusu wewe ni kuwa wewe ni msomaji wa vile vijarida vya propaganda vya watu binafsi wanajifanya ni wachambuzi wa mambo....Lakini huwezi kukaa chini na kusoma vitabu vya Great Phillosophers hasa wa mambo ya Religion ili upanue uelewa wako...

Pole sana baki na ujinga wako......
 
Hapo napo ndo nashindwa kuwaelewa maana hilo ndo kimbilio la watu wavivu wa kufikiri. Hamtaki kuchambua mambo kwa kisingizio cha roho mtakbtifu kwamba ili mtu aijue biblia na aielewe lazima awe na roho mtakatifu. Sitaki nikuulize kama unamjua huyo roho mtakatifu kiundani au unamjua juu juu tu kwa maana hiyo ni mada nyingine ya kujadili kirefu. Anyway nikuache kwa leo maana umejitahidi sana kujieleza na kujibu kulingana na uelewa wako hoja mbalimbali ambazo watu wamekulenga wewe. Nakupongeza kwa hilo but one thing to remember is that fungua macho na moyo wako so that you can learn kuhusu dini zote and be free in what you beleave. Utakuwa na uhakika na kile unachokiamini kuliko kung'ang'ania imani ambayo haikupi uhuru wa kuichallenge na imani nyingine. Hapa ninachokushauri ni kusoma basics zake tu. You'll be free.

Huyo Eiyer kama umemsoma ni mbumbumbu wa mambo mengi....Anatumia maswali yasiyo na msingi wowote kama defensive mechanism yake ya kuficha ombwe la uijinga wake....

Nakubaliana na wewe kuwa hana Free mind katika kuchangia kitu...Mtu wa namna hiyo kujadiliana naye ni uzezeta fujo....
 
Last edited by a moderator:
Kaka unajua Kuwa biblia agano jipya lilikuwa compiled kwa initiative ya jamaa mmoja ambaye alikuwa ni tajiri na mfanyabiashara ambaye ni mchamungu na yeye ndo aloanzisha mchakato wa kutengeza biblia agano jipya na yeye na watu wake ndo walokuwa na uamuzi kipi kiwekwe na kipi kisiwekwe inasemaekana baada ya kifo cha yesu viliandikwa vitabu vingi sana na waandishi wengi mmoja wao ni Mary Magdalene kitabu chake hakikuzingatiwa kwa kipindi kile ni sababu ya mtazamo wa jamii ya enzi izo towards wanawake. Siyo maneno yangu mkuu na mie nimepitia pitia hizi documentariea na google.

Si kweli, ukumbuke Yesu alipokuwepo watu wengi walikuwa wanaandika habari za Yesu na wengine walikuwa wanaandika habari za kusikia, hivyo injili zao zisingekubaliwa kuwekwa kwenye biblia. Injili kama Maria haikukataliwa isipokuwa haikuingizwa kwenye biblia kwa sababu ilikuwa tu na hadith za Yesu kabla hajaanza kufanya kazi za kinabiii. Ingekuwa nisuala la jinsia basi hata injili ya mtu mmoja aitwae Petro(mwanaume)ingekubaliwa.

Pia ukumbuke Muhammad hakuandika Quran, yeye alikuwa anatamka tu zile aya, quran imeanza kuandikwa kwenye kitabu miaka zaidi ya ishirini baada ya mtume kufariki. Waliosimamia hiyo kazi ya kuiandika quran vitabuni walikuwa Othman, Abu Bakr na Zayd ibn Thabit, na wao baada ya kumaliza kitabu chao waliagiza aya zozote nyingine amabzo zipo nje ya kitabu zichomwe moto na ni marufuku kuzitumia.

Nikirudi nitakuellewesha zaidi.
 
Pia Da Vinci ndo aliyechora michoro iliyopo cistine chapel, hasa mchoro maarufu wa mwanaume aliye uchi wa mnyama uitwao michangelo, hili ni eneo lililopo inner conclave na ndipo makadinali hukusanyika kumchagua papa mpya, I stand to be corrected.
 
Mkuu,ule mchoro wa Sistine Chapel unaitwa last judgement.Aliyechora ni hasimu wa Da Vinci kwa jina MichelAngelo.Kumbe micheangelo si jina la mchoro,ni jina la mchoraji.Da vinci mchoro wake mwingine maarufu ukiacha last supper na MonaLisa unaitwa vitruvian man.Watu wa medicine watakuwa washakutana nao huo mchoro,kwani ni maarufu kwenye mambo yao ya sayansi ya tiba.
 
Its worth it to know for the sake of knowing napend kukazia maarifa kwa kitabu cha ufunuo wataalamu wanasema kuwa kulikuwa na vitabu viwili vya ufunuo kimoja cha peter na kingine cha yohane kilichukuliwa cha yohana kikaachwa cha peter kwa nn? Inasema peter kitabu chake kilkuwa so straight na kinasema aliambiwa Christ kuwa mwishowe wote waovu watasamehewa na maisha yataendelea lakini wahusika wakaona si logic ya kukijumuisha kitabu hicho sababu watu hawatakuwa na hofu ya kuacha mabaya kwa sababu wanajua mwishowe watasamehewa. Jamani narudia haya si maneno yangu

Kitabu cha ufunuo wa Peter kipo,hata kwa fragment,kitafute kwenye pdf ukisome.Kingine kizuri kukisoma ni matendo ya Peter;kuna vita kali mle ndani, kati yake na Simon the magician.Kama mtu wa imani basi imani yako itaimarika!
 
kuna jamaa anaitwa Dan Brown ameandika vitabu mali mbali vinahusu imani za watu....kimojawapo ni hicho cha da vinci code , lost symbols , angels and demons...
nilisoma nikawa napata wakati mgumu kumuelewa... ikanibidi kusoma review ya kitabu kizima...
masuala haya ni imani kuna watu wanaamini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom