Leonardo Da-Vinci

Leonardo Da-Vinci

Hapo napo ndo nashindwa kuwaelewa maana hilo ndo kimbilio la watu wavivu wa kufikiri. Hamtaki kuchambua mambo kwa kisingizio cha roho mtakbtifu kwamba ili mtu aijue biblia na aielewe lazima awe na roho mtakatifu. Sitaki nikuulize kama unamjua huyo roho mtakatifu kiundani au unamjua juu juu tu kwa maana hiyo ni mada nyingine ya kujadili kirefu. Anyway nikuache kwa leo maana umejitahidi sana kujieleza na kujibu kulingana na uelewa wako hoja mbalimbali ambazo watu wamekulenga wewe. Nakupongeza kwa hilo but one thing to remember is that fungua macho na moyo wako so that you can learn kuhusu dini zote and be free in what you beleave. Utakuwa na uhakika na kile unachokiamini kuliko kung'ang'ania imani ambayo haikupi uhuru wa kuichallenge na imani nyingine. Hapa ninachokushauri ni kusoma basics zake tu. You'll be free.

Mimi nilijifuna na bado najifunza kuhusiana na dini zingine na imani zingine pia [nadhani unajua tofauti ya imani na dini] hivyo hili lisikutie shaka

Kwenye inami ya Kikristo kuna mambo kama sio wa imani hiyo huwezi kuaelewa kwakuwa huwezi kuyajua,ili uweze kuyajua ni hadi pale utakapokuwa kwenye imani hiyo hivyo kuyaita uvivu wakufikiri kwasababu tu huyajui ni uvivu wakufikiri kuliko hata uvivu wenyewe ulivyo

Nakushauri kama kitu hukijui kama ulivyosema hapo juu ni bora ujaribu angalu kuuliza ili uelewe ni kitu gani

Iliniuliza namna ninavyojua kama andiko hili ni la roho mtakatifu au vipi nimekuambia,badala ya kunichallenge kupitia nilichokuambia unaniambie eti mi mvivu wa kufikiri

Haya mkuu,kila la kheri!
 
Huyo Eiyer kama umemsoma ni mbumbumbu wa mambo mengi....Anatumia maswali yasiyo na msingi wowote kama defensive mechanism yake ya kuficha ombwe la uijinga wake....

Nakubaliana na wewe kuwa hana Free mind katika kuchangia kitu...Mtu wa namna hiyo kujadiliana naye ni uzezeta fujo....

Mwanzo ulisema kuwa nauliza maswali ambayo hata mimi siwezi kuyajibu,hii inamaana kuwa ni maswali magumu

Leo unasema mimi ni mbumbumbu wa mambo mengi na nauliza maswali ambayo hayana msingi,ajabu sana hii

Any way,asante sana mkuu na ubarikiwe!
 
Wewe sijui ni.mtu wa aina gani......Unaponiuliza swali "hivi unajua".....Maana yake umejiridhisha mimi sijui....Sasa ni jukumu lako wewe kunijuza....
Hapana,kama nimejiridhisha nisingekuuliza
Sijaongelea mambo ya Pope lakini naona umeongelea....Vipi unawazimu nini...??? Rejea maana ya neno Papa ujue...Ni neno la kawaida kabisa likimaanisha (Baba)... Kwa hiyo swala la kuanza sijui kutumika lini hilo halina tabu.....
Umeshindwa kupata mantiki ya nilichokisema kwakuwa hujui hata kwanini kanisa katoliki unalodai kuhusika na Biblia lina Papa na kwanini anaitwa hivyo

Pole sana
Hiyo roho na kweli ni ipi...??? Kama ni kusoma nimesoma hayo maandiko.....
Kama wewe ni Mkristo hii ni aibu sana kwa kuuliza swali hili

Kama wewe sio Mkristo nakushauri ukausome Ukristo na uuelewe kisha uje hapa uulize maswali
Nilichogundua ni kuwa wewe hujui kitu chochote zaidi ya kuuliza maswali mengi yasiyo na msingi ili uonekane unajua....Anyway ni defensive mechanism yako...
Kuna mambo unashindwa kuyatofautisha

Unaposoma jambo na ukashindwa kulielewa inawezekana kuna mambo yafuatayo
Huna uwezo wa kuelewa
Huna uwezo wa kusoma vyema
Nilivyoviandika havieleweki

Hilo la tatu naliondoa kwenye uwezekano wa lenyewe kuwa sababu ya wewe kutokunielewa kwasababu umeshajichanganya sana

Mwanzo ulisema nauliza maswali ambayo mimi mwenyewe siwezi kuyajibu,hii inamaana maswali yangu ni magumu,leo unasema sijui kitu

Mtu asiejua kitu anawezaje kuuliza swali gumu?

Hii inathibitisha kuwa wewe ni either huna uwezo wa kuelewa au hujui kusoma vizuri
Uliambiwa upitie hints usome sidhani kama hata ulisoma.....
Inawezekana hata hujui unachoongea

Mtu anapokuambia kuwa chakula fulani ni kizuri bila kukuambia ni kizuri kwasababu gani atakuwa ana matatizo kwani inawezekana hata hicho chakula hakijui au alihadithiwa tu na hajawahi kukila au kukijua kwani kama angekuwa na ujuzi huo ni wazi angeweza kutueleza hata hicho anachotaka tukisome kina nini ili tusipoteze muda bure

Pia kuna wengine wamesoma mambo na hawajayaelewa na wanakuja na kutuambia nasi tukasome wakati hata kueleza walichokielewa hawawezi

Yanini tupoteze muda?
Kingine nilichogundua kuhusu wewe ni kuwa wewe ni msomaji wa vile vijarida vya propaganda vya watu binafsi wanajifanya ni wachambuzi wa mambo....Lakini huwezi kukaa chini na kusoma vitabu vya Great Phillosophers hasa wa mambo ya Religion ili upanue uelewa wako...
Suala la ku assume ni tatizo kubwa huenda zaidi ya tunavyofikiri

Mtu hata hajui umesoma nini lakini anakuja na kuanza ku assume kuwa umesoma vijarida halafu huyo huyo aliyesoma vijarida anaweza kuuliza maswali ambayo yamekosa majibu

Kaazi kweli kweli
Pole sana baki na ujinga wako......
Asante sana na wewe hongera na baki na werevu wako!
 
Ngoja nikupe contradiction 1 tu kuhusu kukamatwa kwa yesu halafu uniambie roho mtakatifu wako wangapi. Mathayo 26:48. Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara akisema nitakeyembusu huyo ndiye; mkamateni. Yohana 18:4. Basi yesu hali akijua yote yatakayompata, akatokea akawaambia ni nani mnayemtafuta? Sasa nani yuko sahihi kati ya mathayo na yohana juu ya kukamatwa kwa yesu? Nani alikuwa na roho mtakatifu wa kweli kati yao? Jibu kwanza hayo.

Hakuna contradiction yoyote hapo. Japo umechukua sentensi moja moja kwa kila mwandishi hata hivyo hakuna contradiction kabisa. Ukitaka kuilewa Biblia vzr soma muktadha mzima wa tukio.

Mathayo mwandishi anaelezea matukio kabla ya askari kumkamata Yesu, yaani kumtambua kwake, na namna ya kumkamata. Yuda alikwishatoa ishara kuwa atakayembusu huyu ndie Yesu ndio akamatwe. Kitabu cha Yohana kwa upande wake kinaelezea namna Yesu alivyokuwa anajua wakati wa mateso yake umefika (hali akijua yote yatakayompata) hakusita kuwakaribia na kujitoa mwenyewe kwa watesaji. Yohana anakazia zaidi utayari wa Yesu kujikabidhi mikononi mwa watesaji, na Yohana hajatilia mkazo kwenye matukio ya kabla. Hata hivyo Yohana hajakanusha kuwa Yuda alimbusu Yesu au kuwa Yuda alishatoa ishara hiyo.

Kwa maana rahisi zaidi kama tukio lilikuwa na scenes 1,2,3,4, - kama vile (1)mipango ya busu la usaliti, (2)kitendo cha busu lenyewe, (3)Yesu kumzodoa Yuda kwa kumpa busu la usaliti na kumtaka atekeleze haraka alichokusudia na (4)kisha Yesu kuhoji kundi hili la askari wanamtafuta nani, Yohana amekazia scene ya mwisho na ndio maana anaanza na neno Basi hali Yesu akijua............ ambapo kwa Kiingereza imeanza na Jesus, therefore....., Hapa, maana yake mwandishi anaonesha kulikuwa na matukio kadhaa yamefanyika kabla ya hapo kisha ndio anaendelea na tukio ambalo yeye analizungumzia.

Niseme tu kwa ufupi, haiwezekani mashahidi kama vile waandishi wa habari waandike kwa mtiririko uleule, maneno yaleyale, tone ileile na kwa kusudi na hadhira ileile. Ikitokea hivyo ujue mwandishi ni mmoja na wengine wamekopi tu. Sivyo ilivyo kwa Biblia (rejea maelezo ktk post yangu ya juu).

Pili, pamoja na kutofautiana ktk uandishi, pointi za muhimu kama usaliti, busu, Yuda, kukamatwa kwa Yesu mbele ya wanafunzi wake, mateso yake na kuwambwa kwake msalabani, na zaidi sana kufufuka kwake ndio kitu cha msingi zaidi, na waandishi na matukio yote yanathibitisha kuwa haya yalitukia kweli. Ndio maana nikasema hakuna contradiction za msingi.

Mwisho narudia tena Biblia sio maneno ya Mungu ila ni NENO la Mungu. Jumla ya maneno na ujumbe wake ni kuhusu upendo usiopimika wa Mungu kwa wanadamu kupitia Yesu Kristo.
 
Hpo ndipo mtu mwenye akili timamu ataanzia kuutafuta ukweli

Kuna vita inaendelea ndugu yangu ya kumpaka matope huyu aliyebadilisha historia ya dunia!

Na hawataishinda vita hii. Hakuna mtu, taifa wala mamlaka yoyote itakayoshinda dhidi ya Yesu. Yanayosemwa leo Biblia ilishayatabiri miaka mingi iliyopita. Hakuna jipya.
 
Mambo ya imani magumu sana...
Sababu watu wanakuwa na 'pre-conditioned mind'..

Da Vinci zile architects zake zote alozofanya juu ya zana za kisayansi pindi zilipogunduliwa na kufanyiwa kazi na kutoa mafanikio mazuri, hazikuleta tabu kwa walimwengu..
Lakini pale michoro yake ilipohusisha imani za kidini watu walipojaribu kuzitafsiri, shida kubwa ikaibuka kwa wale waliokinzana na tafsiri za waliotafsiri..

Lakini kuna vitu ambavyo watu wengi hukubaliana, mfano wa falsafa kuwa 'history is written by those who hanged heroes','history is written by the winner','history is a set of lies agreed upon' na mambo kama hayo mengi yanayohusisha uandishi wa kumbukumbu za kihistoria..

Hapo tunaweza kujiuliza maswali juu ya hii kazi ya Da Vinci juu ya Monalisa

Kwanini ilimchukua miaka mingi (takribani zaidi ya 12) hadi kufa kwake akiwa anachora hiyo picha?..

Kwanini alitumia codes kuchora picha kama hizo, alihofia nini?.
 


Hi Post Nilitoa Kwenye Group Moja La Uislam Walitamani Kuniua.
Nilisema Hivi

"katika Kitabu Cha ASILI YA MAJINI,sheikh Dr Ahmad H.Sakr Uk116 Anasema
Hadithi Ya Mtume Inathibitisha Jambo Hili.

Aliposema Iwapo Mtu Ataingia Katika Uhusiano Wa Kindoa Na Mkewe Anatakiwa Ataje Jina La Mwenyenzi Mungu Ajilinde Kwa M/Mungu Dhidi Ya Shetani Aliyefukuzwa Mbali Na Rehema.
Vingenevyo Shetani Hujiviringisha Katika Dhakari(sehemu Ya Siri Ya Mwanaume) Ya Mtu Huyo Atashirikiana Naye Katika Tendo Hilo.
............................................
Duuu,hi Hatari Sasa!

Tafakari Yetu Kuwa Huyo Jinni Anayeshiriki Naye Tendo La Ndoa Pamoja Naye Kwa Mkewe Ametumwa Na Huyohuyo Mungu Wao.
~Hiyo Ni Kesi Ya Ngedere Kumpelekea Nyani!
Unadhani Nin Kitatokea!

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
Wana Ndoa Wakislam Poleni Sana.
NJOONI KWA YESU MUOKOLEWE, NDUGU WAISLAM





Katika hiyo Hadith kipi kilichokutatiza?...
 
Madai kwamba Yesu kristo hakufa msalabani hayajaanza leo
siku ya tatu ya kufufuka kwake ndipo yalipobuniwa na tangu hapo karne na karne yamekuwa hivyo.

Wanaokataa kifufuka kwa kristo Yesu ,Mt.Yohana katika nyaraka zake amewaita hao ndio wapinga kristo.

Pia kwa baadhi ya imani kukiri kwamba Yesu kristo alifufuka ni SAWA na kukiri kwamba MAUTI ilishindwa kwa kristo Yesu. Uelewe kuwa NGUVU ya mauti ni kifo. Ushindi wa Yesu juu ya mauti na kuzimu ndilo pigo kuu ambalo linamkera mkuu wa giza.

Aidha, hamwezi elewana juu ya mada hii hiyo.Ninyi mnaongea lugha mbili tofauti.Mmoja anazungumza kwa jicho la kiroho,maana imeandikwa mambo haya yafahamika kwa namna ya rohoni; mwingine anaongea mambo hayo hayo akiongea kimwili hapo KATU hamtakaa mkaelewana.Maana hata peponi penu panatofautiana.Wakati hawa wengine pepo yao itawabidi wavikwe miili mipya,hawataowa wala kuolewa,maana watafanana na malaika; hawa wengine wameambiwa pepo yao iko chini katikati ya miguu ya wanawake.

Neema ya kristo iingilie kati tu.
 
Madai kwamba Yesu kristo hakufa msalabani hayajaanza leo
siku ya tatu ya kufufuka kwake ndipo yalipobuniwa na tangu hapo karne na karne yamekuwa hivyo.

Wanaokataa kifufuka kwa kristo Yesu ,Mt.Yohana katika nyaraka zake amewaita hao ndio wapinga kristo.

Pia kwa baadhi ya imani kukiri kwamba Yesu kristo alifufuka ni SAWA na kukiri kwamba MAUTI ilishindwa kwa kristo Yesu. Uelewe kuwa NGUVU ya mauti ni kifo. Ushindi wa Yesu juu ya mauti na kuzimu ndilo pigo kuu ambalo linamkera mkuu wa giza.

Aidha, hamwezi elewana juu ya mada hii hiyo.Ninyi mnaongea lugha mbili tofauti.Mmoja anazungumza kwa jicho la kiroho,maana imeandikwa mambo haya yafahamika kwa namna ya rohoni; mwingine anaongea mambo hayo hayo akiongea kimwili hapo KATU hamtakaa mkaelewana.Maana hata peponi penu panatofautiana.Wakati hawa wengine pepo yao itawabidi wavikwe miili mipya,hawataowa wala kuolewa,maana watafanana na malaika; hawa wengine wameambiwa pepo yao iko chini katikati ya miguu ya wanawake.

Neema ya kristo iingilie kati tu.


HILI ULILOLIANDIKA NI KAMA ULIKULA TAMBUU YA KIBANIANI NA KUMWAGA MAPOVU YA CHOKAA, KWANI HUJAWEKA USHAHIDI WA KITABU CHOCHOTE WALA AYA YOYOTE YA BIBLIA


MAOMBI YALIKUBALIWA

Bwana Yesu Kristo wakati alikamatwa na Mayahudi na alikaribia kuteswa katika mikono ya watu, alimwomba Mungu sana.

Alianguka mbele Yake,alimkumbusha ahadi yake na alilia kuomba msaada
wa Mwenyezi Mungu.

Biblia inasema kwamba:

Yesu alienda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba akisema; Baba yangu ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke walakini si kama nitakavyo mimi bali kama utakavyo wewe. (Mathayo 26:39).


Bwana Yesu Kristo alikuwa na yakini kwamba maombi yake yamekubaliwa na ndiyo maana alipoona hali imekuwa mbaya zaidi hata kinyume cha matarajio yake, akashangaa kwa kusema "Eloi, Eloi, Lama Sabakthani? Yaani Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniwacha? (Mathayo 27:46 na Marko 15:34).

Alilia hivyo kwa sababu Bwana Yesu alikuwa na yakini ya kukubaliwa maombi yake na ya kupata msaada wa Mwenyezi Mungu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu hukubali maombi ya waja wake, na Biblia inashuhudia kwamba maombi ya Bwana Yesu yalikubaliwa, inasema kwamba:

"Yeye katika siku hizo za mwili wake alimtolea yule aliyeweza kumuokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na mchozi akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu. (Waebrania 5:7).

Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wa kumuokoa na kuwasalimisha watu, alimwokoa Bwana Yesu pia
kutoka kifo cha laana, kikombe cha mauti.

Na baada ya kukubaliwa maombi Bwana Yesu alimshukuru sana Mungu wake, "akasema Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia nami nilijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote. (Yohana 11:41-42).

Sasa wakati Biblia inatangaza kwamba Bwana Yesu alimuomba Mungu kuondolewa kikombe na kifo cha msalaba, Mwenyezi Mungu alikubali maombi yake.

Lakini leo wapo baadhi ya wapinzani wa Yesu ambao wanasema kwamba Mwenyezi Mungu hakujali maombi na machozi ya Yesu wala hakumsaidia kumsalimisha kutoka hila za Mayahudi.

Na kikundi hiki cha Mapadri hata hawajali kufuta na kubadilisha aya za Biblia, ili waweze kutimiza matamanio na malengo yao.

Hata wanasahau kwamba kwa njia hii wanamfedhehesha Bwana Yesu na wanamtenganisha na Mwenyezi Mungu.

Lakini sisi Waislamu tunaamini kwamba Bwana Yesu alikuwa mpendwa wa Mwenyezi Mungu na alikubaliwa maombi yake.


YESU ALIKUWA HAI

Wakati wa kuondoka kutoka chumba kile alituma ujumbe kwamba wanafunzi wake wamkute Galilaya. (Mathayo 38:7 na Marko 16:7).

Baada ya kupata ujumbe huu wanafunzi wote walifika Galilaya. Baadhi yao walidhani kwamba Yesu ameshafariki tayari.

Katika somo hili Biblia inasema kwamba:

"Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona Roho. Akawaambia mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Tazama mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikeni-shikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Basi walipokuwa hawajaamini kwa majeraha, huku wakistaajabu, aliwaambia mna chakula chochote hapa? Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Akakitwaa, akala mbele yao. (Luka 24:36-43).

Tena Biblia inaondoa shaka ya kwamba Yesu hakufia msalabani bali aliendelea na uhai wake baadaye na aliendelea kukutana na wanafunzi wake.

Biblia inasema:

"Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; Kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
(Yohana 20:20-21).


Bwana Tomaso bado alidhani kwamba huyu siyo Yesu bali ni Roho yake. Bwana Yesu aliondoa hata shaka yake pia.

Biblia inasema kwamba:

"Basi wanafunzi wengine wakamwambia, tumemuona Bwana. Akawaambia, nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Basi, baada ya siku nne, wanafunzi wake walikutana ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu na milango imefungwa,
akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Kisha akamwambia Tomaso, lete hapa kidole chako; uitizame mikono yangu. Ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiye amini bali aaminiaye. (Yohana 20:26-27).


Kwa njia hizi zote Bwana Yesu alithibitisha kwamba tangazo lile la kifo na kuuawa kwake lilikuwa la uwongo.

Yeye hakufia msalabani.

Alisalimika .

Sasa kabla ya kumaliza somo hili naomba usome andiko hili. Biblia inasema:

" Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu,mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; tena kama Kiristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote" (1Wakorintho 15:12-19).

Katika aya hizi imeelezwa kwamba kama watu hawatafufuka, Bwana Yesu pia hatafufuka. Na sote tunajua kwamba wafu watafufuka katika Akhera wala siyo katika dunia hii. Hivyo ndivyo Bwana Yesu pia atafufuka katika Akhera wala siyo katika dunia hii.

Biblia inasema kwamba: "Wafu hawawezi kurejea duniani." (Ayubu 7:9).
na kama Kristo hakufufuka , basi imani yenu ni bure. Mngalimo katika dhambi zenu.

Yaani hakuna faida yoyote kuamini kifo cha laana na kufufuka kwake.

Habari ya tatu imeelezwa kwamba waliolala katika Kristo wamepotea.

Na ya nne, hao ni maskini kuliko watu wote.


Enyi ndugu Wakristo, sisi tunawapendeni msife mioyo. Hamna kosa bali hamkujua. Basi sasa jiungeni na dini ya Kiislam. Karibuni sana, Dini ya Kiislam itawapatieni kila heshima. Na hiyo ni njia moja ya kusalimika, Muda wa kutosha mmeupoteza tayari.


Harakisheni kueleka kwenye njia iliyonyooka, Dini ya Mwenyezi Mungu yaani ISLAM.
Karibuni sana.
 
Tatizo la Biblia inajichanganya sanaa. Inasema Adam na Hawa walikuwa ni binadamu wa kwanza kushushwaa duniani lakini hapo hapo ina hadithia tena kuwa mtoto wa Adam alikwenda kuoa nchi ya mbali....Unapata picha gani ? Mimi ni muumini ya dini ya Kiislamu na kwa kweli namshkuru sana MUNGU mimi kuwa tu Muislam ni baraka kubwa. Yesu kama mmoja wa mitume wa MUNGU nna aamini hakuwahi kuwa na Mwanamke kwa maana ya kuoa ( Quran ingeandika ) kama alioa. Tatizo la Biblia imedanganya hata maisha ya Yesu yenyewee - Yesu hakufa msalabani. Niko tayari kupigwa risasi ya kichwa kwa kuamini hivyoo
 
muthe_x;

leonardo da vinci ni moja ya wanasayansi waliojaribu kufanya kila aina ya ubunifu . Aliweza fanya ubunifu wa mwanzo kabisa wa baroon, aliweza kubuni aina ya mwanzo kabisa ya kifaru [kifaa cha vita] na vingine vingi…lakini pia alikua na kipaji cha ajabu cha uchoraji mfano picha maarufu ya monarisa.
Lakini kitu kilicho amsha umakini juu ya mtu huyu ni suala lake la kudai ya kuwa yesu kristu alimuoa marry Magdalena na alikua na watoto wawili ambao kizazi chao kipo huko ulaya..kwa ufupi ni hayo tu


Leonardo Da Vinci hajawahi kusema kwamba Yesu alimuoa Mary Magdalene. Watu wanatafsiri hivyo kutokana na painting yake iitwayo "The last Supper" inayoonyesha Yesu na wanafunzi wake wakila karamu ya mwisho ambapo mtu ambaye yuko karibu kabisa na Yesu ni mwanamke.

Na pia ni lazima waelewe aliye kaa pembeni ya Yesu sio mwanamke ni mwanafunzi wa Yesu anayeitwa Yohane,ni ustadi wa kifasihi ulitumiwa na Leornado kwa lengo la kuonesha ya kuwa Yohane ni mwanafunzi aliyependwa zaidi na Yesu na alikuwa karibu nae baada ya Petro!
 
Leornado di Pierro da Vinci alikuwa ni mchoraji alipenda kujua vitu vingi sana na aliamini ya kuwa binadamu tumejaliwa akili ambazo zinaweza kufikiria chochote na pia tunaweza tukifanisha tunachowa kwa kuwa na bidii.aliishi katika kati ya karne ya 15 na 16 Florence Italy katika kipindi cha renaissance ....kipindi ambacho watu walikuwa wanashindana ubunifu....da Vinci aliichA michoro ambayo ilikuja kuwa na manafaa miaka takribani 300 baada ya kifo chake kwani ilitoa ideas kwa invertors wa vitu mbalimbali kama vile helicopter,vifaru,maparachuti,maroboti "vitruvian man"....nk...nimekuwa nikifuatila historia ya huyu jamaa kwa karibu cjawahi kuona sehemu yeyote ya kuwa amesema Yesu alimuoa Mary Magdalene .Haya madai katika karne ya 21 yamekuzwa na novel ya "Da Vinci Code"iliyoandikwa na Dan Brown aliyechukua hiyo claim kutoka ktk novel nyingine inayoitwa Holy Blood Holy Grail ambayo waandishi wake waliichukuwa hiyo claim kutoka ktk mislead historical source.....na Dan Brown alipoandika novel yake aliinsist on this coz alijua watu wengi watavutiwa na novel yake and he could make a lot of money na akafanikiwA kufanya alichotaka kwani aliuza sana hiyo novel hasa ulaya na kupotosha watu wengi kwa kitu ambacho ni rubbish.....
and it can't be true ...mwenye proof aitoe.....!!!
 
Tatizo la Biblia inajichanganya sanaa. Inasema Adam na Hawa walikuwa ni binadamu wa kwanza kushushwaa duniani lakini hapo hapo ina hadithia tena kuwa mtoto wa Adam alikwenda kuoa nchi ya mbali....Unapata picha gani ? Mimi ni muumini ya dini ya Kiislamu na kwa kweli namshkuru sana MUNGU mimi kuwa tu Muislam ni baraka kubwa. Yesu kama mmoja wa mitume wa MUNGU nna aamini hakuwahi kuwa na Mwanamke kwa maana ya kuoa ( Quran ingeandika ) kama alioa. Tatizo la Biblia imedanganya hata maisha ya Yesu yenyewee - Yesu hakufa msalabani. Niko tayari kupigwa risasi ya kichwa kwa kuamini hivyoo

risasi huto pigwa ila balaa la jehanum si dogo
 
Art....
 

Attachments

  • 1404549957884.jpg
    1404549957884.jpg
    90.1 KB · Views: 163
Kitabu cha ufunuo wa Peter kipo,hata kwa fragment,kitafute kwenye pdf ukisome.Kingine kizuri kukisoma ni matendo ya Peter;kuna vita kali mle ndani, kati yake na Simon the magician.Kama mtu wa imani basi imani yako itaimarika!

Mkuu unaweza kutusaidia link hapa tuka download... ni vizuri kujadili kwa hoja kama hizi na si kwa hisia binafsi... good
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom