Wewe ndiye mjinga kwa kudhani kuwa Biblia yote ina maneno ya Mungu as if imeshushwa tu magically from the clouds.Huna unachokijua zaidi ya dogma uliyolishwa na ukameza mazimamazima kama zuzu.
Hapo nimekugusa kidogo tu,povu zinakutoka.Nikikwambia tujadili John na nani aliandika,kwanini iko tofauti utaweza?Tujadili synoptic problem,Q source, utaweza?Tujadili Matthew,lengo lake nini,alikuwa nani,kwanini kawekwa mwanzo na style yake ya uandishi ilimlenga nani utaweza wewe?
Hujanielewa kabisa au inawezekana huna uwezo wa kuelewa kama utakuwa umesoma maelezo yangu
Hilo litakuwa wazi kwa yoyote ambae atakuja na kusoma maelezo yangu na yako
Hakuna Mungu aliyeshusha wala kuandika Biblia.Ni binadamu walikaa na kuandika yote unayoyaona kwenye hiyo Biblia yako na ndiyo maana kuna contradictions nyingi mno kwenye hivi vitabu.Kusema kuwa walikuwa divinely inspired ndipo wakaandika ni hoja iso mashiko,kwavile the immediate qtn ni kwanini wawe wao na asiwe myahudi Josephus?au Mary of Magdala?Nani anaweka standards kuwa huyu ni divinely inspired na huyu siye?Kajuaje?na wewe na mimi tunajuaje?
Ndugu nakushauri badala ya kuandika tu hebu uwe unasoma maandiko yangu na kama mara moja inakushinda kuelewa basi soma mara nyingi uwezavyo ili ukija kujibu ujibu kwa hoja ambayo inakuwa na mashiko
Hiki ulichokiandika hapa nimeshakitolea maelezo nikikujibu tena tutakuwa tunarudia kitu kile kile bila sababu ya msingi
Kabla ya kujibu nilichokuandikia unaendelea kuongeza maswali na kwa mwendo huu yatakushinda tu,madai yako ya kuwepo kujikinza kwenye Biblia hujayatolea maelezo ya kutosha hivyo nayaacha kama yalivyo
Biblia haikuandikwa siku moja kwa pamoja kutoka source moja.Lazima uelewe ukweli huu kwanza.Maisha ya Yesu na mafundisho yake yalianza kuandikwa miaka zaidi ya hamsini baada ya kufa kwake.Kulikuwa na waandishi wa mwanzo kabisa kuanzia 60-150AD ambao miongoni mwao ndiye huyu Mark wa gospel according to Mark inayoishia 16:8 kabla ya viongezeo.Hizi kazi za mwanzo ndizo original manuscripts au original source/primary source ya vitabu vya hii Biblia unayoitumia.Kwahiyo baadaye zilifuata additions humo,translations na revisions nyingi tu(ambazo zilifanywa na watu pia) mpaka ikapatikana hii Biblia ya sasa.
Unajua unaweza kuwa unasema kweli lakini ili iwe kweli na watu wakubali sio tu wewe kuandika hapa bali ni kuambatanisha na ushahidi ndugu yangu
Kusema tu sijui injili ilikuwa inaishia hapa au pale utakuwa kama vile unapiga story za kwenye kahawa tu
Najua kuwa biblia haikuandikwa siku moja lakini kitendo cha wewe kudai kuwa haikuandikwa kutoka kwenye source moja kinanilazimu nikudai uniambie hiyo source nyingine ni ipi au zipi kama ziko nyingi na unipe ushahidi wa hilo na uj\niambie umejuaje
Kuamini kuwa kitabu kilichoandikwa 60AD kwa Kigiriki au Kiebrania ni sawasawa kabisa kwa asilimia mia na unachokisoma leo kwenye Lugha ya Kiingereza au Kiswahili baada ya misukosuko mingi ya kijamii na kisiasa ya tawala za kipagani na hata za kidini iliyotokea katika sehemu ambazo vitabu hivi viliasiliwa, ni umbumbumbu usio mfano na sitashangaa nikisikia wewe ni mmoja wapo wa mateja yaliyokubuhu katika maombi ya manabii feki wa zama hizi waliochipukia kwa wingi duniani na kutapeli watu wengi wasio na maarifa kuhusu imani wanazofuata.
Usiwe unapenda ku assume kwa sababu sio sahihi kwa mtu makini kufanya hivyo
Tatizo lako unadhani kila mtu anafuata mambo kimkumbo wakati sio kweli,unapojadiliana na mtu usi assume kuwa hajui,weka nondo zako kisha umpime,so far sijaona chochote ulichokiweka hapa ambacho ni cha msingi naona unaleta maoni yako tu kitu ambacho siwezi kukijadili kwani siko hapa kujadili maoni bali fact
Halafu usiniwekee maneno ambayo sikuandika.Hakuna niliposema kuwa mtu akiongea na mitume basi anachoandika ni neno la Mungu.Nilichohoji ni kwanini vitabu vingine viliondolewa kwenye Biblia na vingine viliachwa na nilikupa mfano wa codex sinaiticus uende ukasome,na ungeona kuwa kulikuwa na barua ya Barnabas ambayo ilikuja kuondolewa baadaye.
Una matatizo makubwa sana ya kuelewa wewe
Jifunze kwanza historia ya Ukristo na Biblia kabla ya kuanza kutoa povu kwa vitu usivyovielewa vizuri.
Sijazungumza chochote kuhusiana na historia sijui umejuaje kuwa sijui historia
Una assume sana wewe,hebu punguza!