Je, Yesu amesulubiwa?
Qurani inaeleza katika Sura 4:157 kuwa Yesu hakusulubiwa: Na kwa (ajili ya) kusema kwao: Sisi tumemuua Masihi Isa, mwana wa
Maryamu, Mtume wa Mungu, hali hawakumwuua wala hawakumsulubu,...
Je, unaendelea kuamini kuwa Yesu amefia msalabani?
unaweza kuniambia Ndiyo, alikufa na baadaye akafufuka.
KWANZA Ufahamu kuwa hakuna mtu aliyeshuhudia muda aliofufukia.
Wao walilikuta kaburi alilolala Yesu likiwa tupu na wakahitimisha kuwa amefufuka, kwa sababu wanafunzi na mashahidi wengine walimwona akiwa hai baada madai ya kusulubiwa. Je, haiwezekani kuwa, kama inavyodai Qurani, kwamba hajafa msalabani?
Waweza kuuliza , Ushahidi upo wapi?
Majibu . Hebu tutazame vifungu vya Biblia ambavyo vinaunga mkono hitimisho hilo.
Je, unayapa uzito zaidi yale aliyoyasema Yesu au tetesi za wanafunzi, mitume, na mashahidi wengine?
Bila shaka, zaidi ni kwa kile alichosema Yesu mwenyewe.
Hiyo ni kwa mujibu wa vile alivyosema Yesu: Matayo 10:24
Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.
Unaweza kuniambia tena , Lakini Yesu mwenyewe amesema kuwa atafufuka miongoni mwa wafu: Luka 24:46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, Kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
JIBU ,Kuteseka mara nyingi kunatiwa chumvi zaidi katika Biblia kwa kutumia msamiati wa kufa, kama Paulo aliovyosema katika 1 wakorintho 15:31 Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu nilikonako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku. (yaani ninateseka kila siku).
Huu ni ushahidi mwengine:
1. Msalabani, Yesu alimsihi sana Mungu amsaidie: Matayo 27:46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Katika Luka 22:42, inasimuliwa kuwa; Akasema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si
mapenzi yangu, bali yako yatendeke. (Kombe hilo ni kombe la mauti.)
2. Ombi la Yesu asife msalabani lilikubaliwa na mungu, kwa mujibu wa Luka, mwandishi wa Waebrania, na Yakobo. Kwa hiyo, vipi afie msalabani?
Luka 22:43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. Hili linamaanisha kuwa malaika amemuhakikishia kuwa Mungu hato mwacha bila ya kumpa msaada:
Waebrania 5:7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.
Maombi ya Yesu yalisikilizwa, jambo linalomaanisha kuwa maombi yake yalijibiwa na Mungu kwa wema:
Yakobo 5:16 ...Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Yesu mwenyewe amesema katika Matayo 7:7-10 Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona, bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka?
Ikiwa maombi ya Yesu yote yalikubaliwa na Mungu, likiwemo lile ombi lake asife msalabani, sasa itakuwaje mng`ang`anie kuwa amefia msalabani?