Leonardo Da-Vinci

Leonardo Da-Vinci

Naomba nisikujibu kwasababu inaonyesha uelewa wako ni mdogo sana kama hata hujui kanisa ni nini unatakaje tujibishane na wewe habari za kanisa na ukristo ndugu yangu Ally? Mimi na wewe nadhani ni bora tukabishana kuhusiana na CUF,CCM na CDM kuliko habari za Imani tayari unaimani/mawazo yako juu ya Kanisa na ukristo hata nitoe povu vp kukueleza huwezi nielewa

Hiyo ni blah blah ya kukwepa hoja !
 
Mkuu familia sio jambo la siri na wala haliwezi kufunikwa kirahisi kama unavyofikiria kwani hao watoto wa Yesu wasingependa kufahamika kama watoto wa Yesu? Nina mwenye uwezo wa kuifunika hii familia ya Yesu muda karne zote hizo kuna uwezekano Yesu alikuwa karibu na Magdalena lakini sio ukaribu wa kimahaba kama baadhi ya watu wanavyotaka kuwaaminisha watu na huo ukaribu ndio msingi wa huu uvumi wa kua Yesu alizaa na Magdalena

kwaiyo yesu alikua mgumu?
 
Wewe Mchungaji na Yesu wako! Kila akitajwa au akipewa challenge kidogo tu unapagawa! Yeye myahudi na wewe mmatumbi wapi na wapi?

Besides hivi wewe unaweza kutoa criticism yoyote ile dhidi ya Da Vinci kweli? Katika uwanda upi utampinga? Science, maths, astronomy, painting, etc?
Kwani Da Vinchi ni nani?
Maana unaonekana unamuogopa sana!

Halafu kwani hapa tunamzungumzia kwenye eneo gani?
Maana inaonekana hata hujaisoma mada!
 
Umepotoshwa kwa mujibu wa huyo muandishi
huyo William Shao anayetaka kukuaminisha uongo kuwa ni kweli...Mkuu Ant-Catholic wengi huwa wanapotosha mafundisho ya kanisa.....Ukweli ndo huo....Hata hiyo biblia unayoisoma ina vitabu lukuki vilivyo ondolewa na Kanisa kwasababu vilikuwa vya kishabiki zaidi.....Kwakifupi hata hiyo biblia yako imekuwa edited na Kanisa sana sana upande wa agano jipya...

Mfano ni Injili ya Maria, Injili ya Barnaba, Injili ya Thomas, Matendo ya Petro na vitabu vingine vingi viondolewa na kanisa(Catholic) kwasababu vimejaa ushabiki.....Kama unasema kanisa limepotosha basi ni Bora uitupe hiyo Bible yako mbali maana kanisa unalosema limepotosha mambo mengi ndo lime-edit na ku-compile hiyo bible yako.....
Wewe nawe sijui umeibukia wapi
Kwanza hueleweki,hebu jifunze namna ya kujenga hoja halafu uje upya
Pili maneno tu hayawezi kufanya jambo lolote kuwa kweli

Mimi nimesema kanisa Katoliki limepotosha historia wewe badala ya kuja na madai yakiambatanishwa na ushahidi unakuja na maneno tu hapa
Sasa hebu nipe ushahidi wa hayo maneno yako halafu tuendelee!
 
Kwanza ni kweli watu wengi wamekuwa Wakristo kwa kuwa wamezaliwa akakuta wazazi wao wako kwenye madhehebu
Lakini namna yako ya kufikiri kuwa ni LAZIMA kila mfuasi wa kristo awe ameanzia kwenye dhehebu ina matobo matobo sana

Siku hizi watu wanazipata habari za Yesu bila kuanzia kwenye dhehebu lolote,hivyo kusema na lazima utakuwa umejiweka kwenye mazingira mabaya sana

Halafu sijaona msingi wa wewe kujua dhehebu langu kwenye mjadala huu japokuwa nimekujibu swali lako,naomba tu uamini kuwa mimi ni mfuasi wa Kristo,hiyo inakutosha!

mkuu,
sijafikiri kuwa ni lazima, ile lazima yangu ya awali ilikuwa ni utani tu kukutaka utaje dhehebu lako.
msingi wa kutaka kujua dhehebu lako ni kutaka kukuelewa kwa nini unashikilia vitu ambavyo mara nyingi watu wa dhehebu fulani ndio wako hivyo.
mkuu,
mimi ni mtu wa fikra huru na iliyo wazi ninakubali kusikia na kikifanyia kazi, na kujirekebisha inapobidi na ninapoona inafaa.
usinichukilie ni mtu wa fikra nyepesi.

sawa nakuchukilia wewe kuwa ni mfuasi wa kristo usiye na dhehebu unayejifunza mambo ya kristo kipeke yako!!!
 
Wewe ni msomaji wa Biblia gani ambayo Mungu hajajitaja jina lake?
Na kwanini unaisoma Biblia?

mkuu
ninaisoma biblia kwa sababu ina mambo yanayumzungumzia mungu.
biblia ninayoisoma ni ile inayoitwa biblia takatibu yenye agano la kale na jipya.
hakuna sehemu mungu alipotajwa jina lake ambalo labda mimi na wewe tunayajua kuwa ni majina ya watu. amekuwa akiitwa kwa majumuisho tu mungu wa baba zenu, mungu wa isaya, mungu wa jakobo na kuendelea.

kutoka sura 3 mstari wa 14-15 musa alitumwa kwenda kuwaambia watu kitu, akamuuliza mungu watu hao wataniuliza ni mungu gani huyo anaitwa nani, mungu akamjibu musa akamwambia kawaambie MIMI NIKO AMBAYE NIKO amenituma kwenu. sasa mimi niko ni jina? kwa maana ya majina haya tunayoyajua.
mungu hana jina watu wamekuwa wakimuita kwa majina mbalimbali wengine bwana, wengine baba, na mengine mengi ikiwa kuna jina la mungu naomba nijulishe n ami nitakuwa nimejifunza kitu.
 
Kitendo cha wewe kusema kuwa unamuamini Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo tayari wewe ni muamini wa Biblia,sasa niambie ni kitu gani kimekufanya umuamini huyu Mungu ambae ameandikwa kwenye maandiko ambayo huyaamini?[rejea maswali yako uliyoniulia kuwa hayo maandiko umejuaje ni neno la Mungu?]

N kumbuka huyu Mungu hata kama umemjua kupitia tafakari zako bado ni yule wa kwenye Biblia!

mimi nikikuwa nakuuliza maswali yale si kwamba siamini biblia au mungu, rejea post zangu zote utaona, ila nilipishana na wewe uliposema kuwa yale yaliyochaguliwa kuwa katika biblia ndio matakatifu na mungu kawaongoza waliochagua na yale yalioachwa si matakatifu ndio maana hayapo tena na kwamba mungu neno lake halipotei.

hapa tu ndipo mimi na wewe tunapopishana hadi sasa mkuu.
msingi wa maswali yangu ni kuwa una uthibitisho gani kuwa haya yaliyo katika biblia yetu ya sasa ni matakatifu na yaliyoachwa si matakatifu?
mchezo wa binadamu ni mchafu akiwa na nia chafu ili hali ipo katika uwezo wake kwa nini ashindwe kuchakachua.

naamini yaliyo katika biblia na naamini pengine yaliyoachwa kuwa pia ni mazuri kuachwa kwake kuingizwa katika mjumuiko wa biblia ndio tatizo kwangu.
 
Tofauti yangu mimi na wewe ni hii:
Wewe hauiamini Biblia kama ni neno la Mungu na ni kamilifu
Mimi naiamini Biblia kama ni neno la Mungu na ni kamilifu!


umekosa tofauti yangu mimi na wewe ni kuwa wewe unaona vitabu vilivyoachwa kuingizwa katika biblia si vya muhimu ama havipo. na kwamba biblia ni timilifu.
mimi kama ulivyo wewe naiamnii biblia kwa maana yale yaliyoandikwa kwa vitabu vilivyopo sasa vinatosha kunipa elimu fulani. BUT siamini kuwa haijachakachuliwa, na kumbuka ni imani tu ndiyo inayonifanya niimani biblia.

ila kwa kusema naiamini hainikatazi kuhoji pale ninapoona kuna shida. kwani chochote kilichofanywa na binadamu hakikosi kasoro au mapungufu. ni mungu pekee ndiyo mtimilifu. laiti biblia ingekuwa imeshuka toka mbinguni, kwa kuthibitika hivyo nisingekuwa na shaka.
 
Ni mambo mengi sana
Kuanzia madai yao ya kwamba Petro ni papa wa kwanza wa kanisa hilo
Historia nzima ya Ukristo n.k
Mambo ni mengi sana lakini nakushauri kitafute kitabu cha William Shao kinachoitwa MIAKA 2000 YA UKRISTO,HISTORIA ILIYOPOTOSHWA,kitakufungua macho!

sasa mkuu unakuja katika pointi zangu, kama kanisa katoliki huliamini na kumbuka kanisa hilo linaongoza mamilioni ya wakristo na kuamua mambo mengi sana ya ukristo na huku wakidai wanaongozwa na mungu, unapingaje madai yangu kuwa mazao ya kanisa katika ukristo yanakasoro wakati mwingine????????????
na kutokuamini hukuhuku ndiko kunakonilazimisha na mimi nisiamini waliochagua vitabu vipi viingie katika biblia hawakuwa wamefanya hivyo kwa nguvu za mungu bali mapenzi yao wenyewe na sababu zao wenyewe.
 
Sawa lakini naomba ushahidi wa madai yako haya!

Una uhakika na haya maelezo yako?


Wapi nimetaka kuwaaminisha?
Mimi nimesema katafute hicho kitabu wewe unasema nataka kuwaaminisha,kivipi?

Nimepotoshwa kwa mujibu wa nani?

mkuu umemsikia alivyosema,
"vilivyobakizwa nakala zipo vatcan kavunje uchukue"
ndio maana niligusia vatcan kipindi fulani.
hii tu inathibitisha kuwa vipo vitabu vilivyoachwa kwa sababu ya walioviacha zaweza kuwa nzuri au mbaya kwangu mimi naona kitendo cha kuacha hakikua kizuri.
ulisema najiuliza maswali ambayo hayapo na kuwa hakuna kitabu kama cha mary magdalena kama kingekuwa tungeshakiona.

sasa unamsikia ndugu tedo anasema kavunje vatcan?
vitabu vipo na viliachwa makusudi. wao wanadai kwa maslai ya kanisa na imani.
mimi naendelea kusema ni kwa maslai yao binafsi wala sio kanisa.
 
Umepotoshwa kwa mujibu wa huyo muandishi
huyo William Shao anayetaka kukuaminisha uongo kuwa ni kweli...Mkuu Ant-Catholic wengi huwa wanapotosha mafundisho ya kanisa.....Ukweli ndo huo....Hata hiyo biblia unayoisoma ina vitabu lukuki vilivyo ondolewa na Kanisa kwasababu vilikuwa vya kishabiki zaidi.....Kwakifupi hata hiyo biblia yako imekuwa edited na Kanisa sana sana upande wa agano jipya...

Mfano ni Injili ya Maria, Injili ya Barnaba, Injili ya Thomas, Matendo ya Petro na vitabu vingine vingi viondolewa na kanisa(Catholic) kwasababu vimejaa ushabiki.....Kama unasema kanisa limepotosha basi ni Bora uitupe hiyo Bible yako mbali maana kanisa unalosema limepotosha mambo mengi ndo lime-edit na ku-compile hiyo bible yako.....

nakubaliana na wewe asilimia mia kuwa biblia imeeditiwa na kuna vitabu vingi vilivyoachwa.
sikubaliani na wewe kuwa kanisa katoliki lilifanya hivyo kwa mapenzi ya imani ya kikristo . wewe unathibitisha vipi kuwa vitabu vilivyoondolewa vilijaa ushabiki ushabiki gani ushabiki kuhusu nini na ni nani mwenye kusema huu ni ushabiki na huu ni ukweli unaotakiwa watu kujua?
kanisa katoliki lina makasoro mengi si timilifu. na haswa ndiyo sababu nilitaka kujua kama EIYER ni dhehebu gani, kwa sababu alivyoanza kutoa hoja zake alikuwa anataka kufanana na wakatoliki ambao huwa kamwe hawapendi kukosolewa na kuona kila kilichopo katika mafundisho yao ni sahihi pasipo kutafakari zaidi au kujiruhusu kuhoji.

mambo ya imani ni magumu sana. lakini viongozi wa makanisa yetu wana siri nyingi sana ambazo laiti kama wakristo wanaoamini wangepata kuyajua pengine kungekuwa na shida katika kuendelea kufwata makanisa hayo.
mkuu,
mjue mungu na umuamini.
dini na imani ni vitu tofauti japo vinategemeana
 
huyo Mungu unayemuongelea ni wa watu watatu, Ibrahim, Isaka na Yakobo na labda wajukuu wao. Sasa wewe mmatumbi huyo Mungu hawezi kuwa wako. Wako yuko huku Africa.

kwikwiiiiikwiii
inawezekana kabisa mkuu, ila upo pia uwezekano kuwa ndiyo huyohuyo wa kwetu afrika na ndiyo huyo wa isaya na yakobo ila namna tu alivyokuwa akiitwa na kufikiwa, sisi tuliamini mito mikubwa ni mungu,milima mawe na vinginevyo pengine ni namna tu ya kumwita na kumuabudu.
 
Neno lilikuwa 'mungu auwawe' na watu wake !?........then wanapata nini !?
Kwa wauaji wa mungu hakuna lawama ?

mkuu Ally,
mungu wetu ni mungu wa mipango na utaratibu ,nilisema ili neno litimie toka uumbaji alijua kuwa itakuwa hivyo siku moja ili iwe vinginevyo,
ukisoma manabii waliokuwa awali walitabiri kuja kwa yesu duniani na kuwa wanadamu watamsaliti wao walioteshwa na mungu kwa hiyo mungu mwenyewe alipanga iwe hivyo ili neno lake liwe hakukuwa na namna bali ni kujishusha na kuruhusu wanadamu aliowaumba yeyey mwenyewe wamuue afufuke na kila aliye hai athibitishe kuwa yeye ni mungu.

ndio maana inasomeka hivi, ilipaswa mwana wa adamu afe ili litimie neno lililosemwa na manabii na mwanadamu apate ukombozi."
 
Ni vyema kwa wasomaji wa Biblia wakaielewa lugha ya Kiiblia.

Kwa mfano inaposema Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, maneno haya waliyatumia kwa sababu amani zile kulikuwa na miungu mingi, hili kutofautisha ni mungu gani wanamtaja iliwapasa watumie lugha hii kwamba wanamaanisha yule Mungu waliyemwabudu baba zao.

Ila Mungu mwenyewe anasema yeye ni Mungu wa watu wote, anasema hivi, tazama mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili hakuna neno gumu lolote nisiloliweza.
 
kinachonishangaza kuhusu mchoro wa Monalisa ni madai kuwa hauna chochote cha maana, bali ni mchoro tu.pia kuna ubishani zile picha hakuchora yeye binafsi bali wafanyakazi wake.
Alafu kinacho shangaza zaidi ni kwamba, wataalamu waliwahi kuichunguza kiundani picha hiyo na kugundua kuna michoro zaidi ya mmoja kwenye ndani ya picha ya Monalisa!
 
mkuu
ninaisoma biblia kwa sababu ina mambo yanayumzungumzia mungu.
biblia ninayoisoma ni ile inayoitwa biblia takatibu yenye agano la kale na jipya.
hakuna sehemu mungu alipotajwa jina lake ambalo labda mimi na wewe tunayajua kuwa ni majina ya watu. amekuwa akiitwa kwa majumuisho tu mungu wa baba zenu, mungu wa isaya, mungu wa jakobo na kuendelea.

kutoka sura 3 mstari wa 14-15 musa alitumwa kwenda kuwaambia watu kitu, akamuuliza mungu watu hao wataniuliza ni mungu gani huyo anaitwa nani, mungu akamjibu musa akamwambia kawaambie MIMI NIKO AMBAYE NIKO amenituma kwenu. sasa mimi niko ni jina? kwa maana ya majina haya tunayoyajua.
mungu hana jina watu wamekuwa wakimuita kwa majina mbalimbali wengine bwana, wengine baba, na mengine mengi ikiwa kuna jina la mungu naomba nijulishe n ami nitakuwa nimejifunza kitu.

...............Yesu, Yehova, Immanuel, Masihi !:cell::noidea:
 
mkuu Ally,
mungu wetu ni mungu wa mipango na utaratibu ,nilisema ili neno litimie toka uumbaji alijua kuwa itakuwa hivyo siku moja ili iwe vinginevyo,
ukisoma manabii waliokuwa awali walitabiri kuja kwa yesu duniani na kuwa wanadamu watamsaliti wao walioteshwa na mungu kwa hiyo mungu mwenyewe alipanga iwe hivyo ili neno lake liwe hakukuwa na namna bali ni kujishusha na kuruhusu wanadamu aliowaumba yeyey mwenyewe wamuue afufuke na kila aliye hai athibitishe kuwa yeye ni mungu.

ndio maana inasomeka hivi, ilipaswa mwana wa adamu afe ili litimie neno lililosemwa na manabii na mwanadamu apate ukombozi."

............uzushi ni dhambi !:faint2::shocked:
 
............uzushi ni dhambi !:faint2::shocked:

Isaya 53 : 5-12
53.5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
53.6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
53.7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
53.8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
53.9 Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
53.10 Lakini Bwana aliridhika kumchubua; Amemhuzunisha; Utakapofanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, Ataona uzao wake, ataishi siku nyingi, Na mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake;
53.11 Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.
53.12 Kwa hiyo nitamgawia sehemu pamoja na wakuu, Naye atagawanya nyara pamoja nao walio hodari; Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, Akahesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom