Leo nimemkumbuka Nape wa 2015. Alidai CHADEMA wanataka kupeleka marehemu Ikulu na kumuacha mzima

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Ilikuwa Septemba 28, 2015 akiwa uwanja wa Samora mkoani Iringa Nape Nnauye ikimfungia 'Turbo' ya maneno makali aliyekuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa dhidi ya mgombea wa chama chake, John Magufuli.

Nape alisema Chadema imeamua kufanya mabadiliko mengi ikiwemo kuacha mgombea mzima(Magufuli) na kutaka kumpeka marehemu Ikulu. Nape alidai pamoja na mashaka aliyonayo alimuomba Mungu amfikishe hai Lowassa Octoba 25 ya mwaka huo ili aone ushindi wa CCM.

Nape alidai Lowassa alikigeuza chama cha mapinduzi kama kichaka cha kujifichia wakiiba Serikalini huku akisema Lowassa hajawahi kufanya kazi bila kuiba kwenye maisha yake kuanzia alipokuwa makao makuu ya chama, AICC, wizara ya Ardhi, mifugo na uwaziri mkuu.

Nape alimsifia Magufuli kama mgombea muadilifu na kumuita tingatinga na hawezi kulinganishwa na mwizi.

Tingatinga lilipokuwa linatengeneza barabara ya utawala wake, mwamba akasimama katikati ya Barabara akidai tingatinga linatengeza barabara isiyopaswa na akumbuke wao ni sehemu ya kiwanda kilichounda tingatinga. Tingatinga likamfyekelea mbali muundaji na timu yake.

Baadae mwamba akaamua akaombe radhi lakini akaishia kuchukuliwa video akitembezwa umbali mrefu kwenye jumba jeupe na kupokea msamaha hewa.

Marehemu kwa Nape bado yuko hai huku tingatinga lenye afya njema akiwa katangulia. Nape ana matokeo mabovu kwenye hesabu za siasa.

 
Ndiyo Utajua Kweli CCM Ni Waasisi WA Siasa Chafu Tanzania
Aliyekuwa Anapiga Push-up Hayupo Mwenzake Kadunda Mpaka Leo Tunapotangaziwa Katwaliwa
 
Ndiyo Utajua Kweli CCM Ni Waasisi WA Siasa Chafu Tanzania
Aliyekuwa Anapiga Push-up Hayupo Mwenzake Kadunda Mpaka Leo Tunapotangaziwa Katwaliwa
Kwa hiyo kupiga push up nalo ni kosa?
 
Back
Top Bottom