Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

duh kweli wewe ni Godbless! Kwa maelezo haya kama serikali itashikia bango issue hii basi jeshi litapoteza heshima na wala si kujijengea heshima!
 
Long live Lema Arusha tunajivunia kuwakilishwa na ww mjengoni.
 
(hata hivyo namshukuru Mungu kwakunirudisha bungeni)nimeipenda Hii simpatii picha Lukuvi nguo zimembana je,siku nazo hazikimbii ili bunge lianze tuone miongozo ya Lukuvi!
 
Ujumbe alioutoa Lema ni kwamba ni sawa kwa CHADEMA kufanya makosa iwapo makosa hayo pia yanafanywa na vyama vingine. Naona mashabiki wa CHADEMA mnashangilia hili, sijui kama mmeelewa ina implication gani in the future!

Lema anasema "Hili ni jaribu kubwa kwa Serikali ya Kikwete na kama Mbunge ningeshauri fanyeni kama hamjaona jambo hili..." : hapa anamaanisha kuna makosa yanatakiwa kufumbiwa macho ili kukidhi mahitaji ya kisiasa. Je, huu ndio uongozi mnaoutaka watanzania? Hayo ndio mabadiliko yanayowafanya muandamane barabarani kila siku?

Safari barabarani, akili kichwani...

Ndo maana kila siku nasema humu mapenzi ya kizidi yanakua upofu
 
Kamanda Lema karibu tena jembe.Namwamini Mungu ambaye hajawahi kukuacha uabike hato kuacha kwamwe hata utimilifu wa dunia hii.Tulio nyuma yako ni jeshi kubwa mno endelea kututangulia mbele tutafika hata kama njia yetu imesongwa sn.MOROGORO tumekuandalia msafara mkubwa sn wa kukusindikiza mbungeni JAN
 
Hii inaitwa The return of Lema - season one.
najivunia kuwa mpiga kura wa arusha mjini, hakika kura yangu haikupotea.

"mheshimiwa Lema tunakupenda na kukuthamini kama mtoto mchanga"
 
"Wabunge wenu wanaendelea kufanya ngojera Bungeni ambayo inaitwa " nitaje majina au Nisitaje " eti kutaja majina ya wezi na yenyewe inahitaji Itafaki "
Hapa ajibu ZZK maana ndiye alisema ana majina halafu hakutaja kama alivoahidi! Jembe likirudi bungeni lazima majina yatajwe tuu!!
 
Serikari na JWTz wasikurupuke ktk kulishughurikia swala la askali mkweli
 
Lema ndiyo kaandika au kaandikiwa haya maelezo.

Kumbe "masalia" mpo wengi namna hii???
Ninaendelea kuwatambua kwa "utambulisho wenu rasmi".

Yaani hata maelezo hii ni ya "kuchakachua"???
 
Mkuu Omutwale hilo dongo lipo aya ya ngapi??

Hili siyo dongo?
...Ziko pesa zetu , Uswisi , Dubai , New Jersey , na sehemu mbali mbali Duniani na Wabunge wenu wanaendelea kufanya ngojera Bungeni ambayo inaitwa " nitaje majina au Nisitaje "eti kutaja majina ya wezi na yenyewe inahitaji Itafaki , hata hivyo namshukuru Mungu kanirudisha Bungeni.
Godbless J Lema. (Mb Arusha)
 
Back
Top Bottom