Henry Kilewo
JF-Expert Member
- Feb 9, 2010
- 899
- 1,108
SIKUOGOPA NILIPOONA MWANAJESHI ANAPIGA PICHA NA MIMI - GODBLESS LEMA.
Jana ilikuwa ni sikukuu ya Noel , nilikuwa kijijini kwetu hivyo sikupata fursa ya kusoma habari za magazeti na vyombo vingine vya taarifa za habari , asubuhi hii nimepitia taarifa mbali mbali nakuona taarifa ya JWTZ kuhusu mtu anayedhaniwa kuwa Mwanajeshi kupiga picha na Wabunge wawili Mimi Godbless Lema pamoja na Joshua Nasari.
Kwanza niseme huyu Mtu aliyesikiliza mkutano wetu na kuomba kupiga picha na sisi ni kweli atakuwa ni mwanajeshi sasa wa kambi hipi na wapi nawaachia Jeshi wafanye uchunguzi wao , lakini ushahidi wa haraka tu ni kwamba hata kabla ya kupiga picha na sisi alikuwa amekaa na na Askari Polisi ambao walikuwa wanalinda Usalama wa Mkutano, sasa swali la kujiuliza inawezekanaje Askari Polisi wakasima na Mtu aliyevaa nguo za Jeshi wakati sio Mwanajeshi na walikuwa wanaongea?
Hata hivyo kwa ufupi sana , Askari mdogo huyu kama atafukuzwa kazi kwa sababu ya picha aliyopiga na sisi basi tutaendelea kuthibitisha double standard ya utawala katika Taifa letu , huyu kapiga picha taarifa inatolewa na JWTZ , lakini wako wengi ambao ni wanajeshi wa vyeo vikubwa ambao sio tu wanapiga picha na viongozi wa Chama Tawala bali ni wafanya Kazi wa CCM , kwa mfano Wakuu wa Mikoa Tanzania ni Wajumbe wa kamati ya Mkoa ya Siasa ya CCM na pia hata Wakuu wa Wilaya ni Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya kupitia CCM , jaribuni kufanya tafiti zenu ndipo mtakapoelewa kwamba ni Wanajeshi wangapi wa vyeo vikubwa wako na wanafanya kaza na Chama Tawala kama Viongozi wa CCM.
Naona Mungu anataka kufungua ukurasa Mwingine katika katiba mpya tunyotarajia kuiandika na sio kila jaribu ni mkosi ukitazama kwa makini Dunia imefika hapa ilipofika kwa sababu ya vitu vingi vilivyoitwa makosa na kumbe zilikuwa ni hatua muhimu katika taratibu mbali mbali za mafanikio , huyu Kijana wakati anapiga picha aliongea na kusema " Nimechoka na ndugu zangu wamechoka CHADEMA tusaidieni mabadiliko ya kweli " haya maneno uwezi kuyafuta kwa mkwara na vitisho bali kwa kuboresha maisha ya Watanzania
Kwani waliochoka na ambao hawajapiga picha ni wengi sana tena yawezekana robo tatu ya Askari wote Tanzania na huu ni ukweli na Chama Tawala warudi wakatazame matokeo ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika kambi mbali mbali za Majeshi yetu.
Hili ni jaribu kubwa kwa Serikali ya Kikwete na kama Mbunge ningeshauri fanyeni kama hamjaona jambo hili kwani litafumua chuki kubwa kati ya Askari wadogo na wakubwa ambao kimsingi wengi wao kwa wazi kabisa wanatumikia CCM wazi wazi kwa nafasi mbali mbali katika Taifa letu , Kwa mfano Kanali Ndomba alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha kabla ya kuamishiwa Makao Makuu ya Jeshi na sasa ni Mnadhimu wa JWTZ .
Dhambi kubwa kuliko zote Duniani ni Uoga na kitisho namba moja Duniani katika Maisha ya Mwanadamu ni kifo , lakini falsafa ya kifo ni ya ajabu sana hata ukiendelea kuogopa kufa hakuna maana kwamba utapata bahati ya kuishi milele kwa huruma ya kifo ni lazima tu siku moja utakufa , na sasa ndio maana Steve Biko alisema " ni heri mwanadamu akaishi miaka michache Duniani Jina lake likabaki linaishi kwa haki na wema kuliko miaka Mingi akatoweka kama mzoga" ni dhambi kubwa katika demokrasia kuupuuza ukweli eti kwa sababu anayesema uongo amejifunza kupiga na kuua.
Jeshi kabla halijamchukulia huyu Kijana hatua wafanye utafiti wa kina ni wangapi wanapaswa kufukuzwa kazi na kuondolewa vyeo vya kwa sababu ya kutumikia CCM ambacho pia ni Chama cha Siasa na pia mtusaidie sasa kulinda vyema rasilimali zetu ambazo Usalama wa Taifa na Polisi wameoneka kushindwa ndio maana Mnyama kama Twiga alipita Air Port ya Kilimanjaro bila mtu mmoja wa Usalama na kamera kumuona.
JWTZ , tusaidieni japo kukemea na kutoa Tamko kwamba hamtaki Nchini yenu iendele kuibiwa tena , Ziko pesa zetu , Uswisi , Dubai , New Jersey , na sehemu mbali mbali Duniani na Wabunge wenu wanaendelea kufanya ngojera Bungeni ambayo inaitwa " nitaje majina au Nisitaje " eti kutaja majina ya wezi na yenyewe inahitaji Itafaki , hata hivyo namshukuru Mungu kanirudisha Bungeni.
Godbless J Lema. (Mb Arusha)