Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Lema: Sikuogopa nilipoona mwanajeshi anapiga picha na mimi

Kuna watu wanajitahidi kuficha UKWELI lakini hata Mwl.Nyerere alionya kuwa ukweli haupuuzwi kwani hauna tabia ya kujificha.Kuna watu wanasingizia eti waliopewa vyeo ccm walistaafu, wako wangapi?

Kamanda Lema amemtaja Kanali Ndomba ambaye alipewa ukuu wa mkoa wa Arusha, Mkuu wa mkoa wa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM, Je,mnataka tuamini mtu huyo ambaye sasa alihamishiwa makao makuu JWTZ na kuwa Mnadhimu wa jeshi siyo mwanachama, mshabiki au mshiriki wa siasa za CCM?

I believe that, a thing cannot be and be at the same time which means Kanali Ndomba who once worked with ccm cannot be isolated as a neutral figure from politics. The truth is changes are demanding on the site,so let us accept the truth and take some steps in a constitution.
 
Haya maelezo ukiyasoma kwa makini yanabeba ujumbe mkubwa sana si JWTZ tu wafanyakazi wengi wamechoka ila huyu kaonyesha kumbe hata huko JWTZ wapo waliochoka. Jamani hili nalo ni janga. Kesho mtaona polis waliotumwa kuzuia ghasia wanaweka mitutu chini na kuwaambia wandamanaji endeleeni kama Misri ndo tuendako.
 
Hakika Lema ni kisiki cha mpingo, natamani na nitafurahi sana siku ukija kwetu Tabora tutakupikia matoborwa na tukupe na togwa unywe.

long live lema.

Umenikumbusha mbali sana dah,michembe je ipo?
 
Lema ndiyo kaandika au kaandikiwa haya maelezo.

Sina shaka kuwa hili ni andishi la Lema. Maana Lema na Mbowe karibu mara zote hawaandiki au kuhutubia mpaka mwisho bila kutoa nukuu za Wapigania haki maarufu kama Malcon X, Che Guevera, Martin Luther, Mandela. Steve Bico, etc

Katika andishi lake sikufurahishwa na dongo alilompiga Zitto ikizingatiwa wote ni CHADEMA, japo alichokiandika ndiyo ukweli.
 
naomba kuuliza swali hapa na hapa nitaomba wale wajuzi a sheria wanisaidie kujibu.
hivi mtumish wa serkali anapofikia umri wa kustaafu ama niseme mwaka wa kustaafu hupewa likizo ya 3 months ya maandaizi ya kustaafu kwanza nijibiwe niko sahihi??

haya ndani ya miezi hio mtumish huruhusiwa kusanii mkataba wa ajira ya muda kama yuko tayari na kama nafasi yake iyo haina mtu wa kuijaza kwa wakat huo, ila kama hataki basi huandika barua yake pamoja na nyaraka muhimu ili astaafu kwa ufahari sio?? naomba jibu pia kama nko sahihi

sasa je inapotokea mtumish huyo wa akaona greener pasture je hana ruhusa ya kuingia humo kisheria?? provided kwamba ameshathibitika kwamba yuko katika hatua za mwisho za kustaafu kwake??

naomba Nyani Ngabu, EMT ruttashubanyuma Rutashobollwa na wengine wote wenye ujuzi wa sheria kunisaidia katika hili.
 
Last edited by a moderator:
Wana Arusha tunajivunia kuwa na mbunge kama Mh lema,asante Mungu kwa kumleta Lema duniani,tunamshukuru mama yako na baba yako kukuleta dunia! Tunakutakia maisha marefu Lema
 
Lema haipingiki kuwa uko sawasawa baba,huna haja ya kuogopa kwa sababu Chadema hakuna siasa za kuogopana km kw Chama Chakavu

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
kama hujorogwa na mashati na kofia za kijani wala gwanda afu ukasoma haya maelezo ka Mtanzania ukwel unakuja bila chenga.. Jeshi na vyombo vyote vya usalama lazima vijitazame sasa..
 
Lema ndiyo kaandika au kaandikiwa haya maelezo.

Riz mbona una majungu sana. Unajinsia mbili nn mkuu. Au ww ndo umemuandikia Lema huo ujumbe. Naona hamuamini kama lema anaweza toa ujumbe makini kama huo poleni sana Magamba. uzuri mmeusoma na mmeulewa vizuri tu KAZI MNAYO JIBUNI HOJA SIO MAJUNGU.
 
Tunashukuru kwa aliyemwandalia haya maelezo lema!

Tume ya Katiba habari yako!
Lema siyo wakuandaliwa hotuba, bali hicho ndo kipaji alichonacho kuongea................ ukitaka kuthibitisha hudhuria mkutano wake wa hadhara siku moja kama utamkuta hata na kikaratasi!
Kama nyie huko ADC mnaandaliwa ni kwasababu mabegani mmebeba nazi siyo vichwa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom