Lema apingana na CHADEMA kuhusu Katiba Mpya

Lema apingana na CHADEMA kuhusu Katiba Mpya

hebu uandikie uzi mahususi jukwaani tuone wadau wa Jf wanasema, nadhani itapendeza zaidi.

but kuhusu hoja iliyoko mezani vip,
Uhuru wa kutoa maoni chadema umefutwa nini?šŸ’
Kwani sasa wana Chadema wanafanya nini wanavyo jadili ishu ya Lema kwa uwazi.

Nakumbuka wewe hadi dkk ya mwisho ulikuwa pro Nchimbi leo hata kusema free Nchimbi unaogopa.
 
Kwani sasa wana Chadema wanafanya nini wanavyo jadili ishu ya Lema kwa uwazi.

Nakumbuka wewe hadi dkk ya mwisho ulikuwa pro Nchimbi leo hata kusema free Nchimbi unaogopa.
Kama kiongozi wa kitaifa wa chadema ametoa maoni yake huru kuhusu katiba mpya, mange kakubeba ufala wa kifikra kama ulivyo na kuanza kumshambulia lema badala nawe utoe maoni yako huru kuhusu katiba hiyo hiyo mpya bila kubebwa ufala wa kifikra na mange šŸ’
 
Sijaanza leo kutoa maoni yangu kuhusu kuwa na wasiwasi na Lema fuatilia tangu uchaguzi wao wa ndani.
 
Kauli mbiu kuu ya CHADEMA ni 'No Reforms No Election', yaani hakuna uchaguzi bila mabadiliko ya katiba, hii kauli ndiyo iliyompeleka Lissu gerezani.

Lema yeye anasema Katiba haina maana yeyote, inamaana anapingana na chama chake, anapingana na msimamo wa Mkiti wake anaungana na CCM wanaosema katiba haikuletei chakula mezani.

Kifupi Lema anasema tuendelee na hii hii katiba iliyowapa CCM uhalali wa kuunda serikali haramu, inayowapa CCM kiburi cha kusema majeshi yote ni mali yake. Katiba inayowapa CCM nguvu ya kuingilia mihimili yote, Bunge Mahakama na Serikali. Katiba inayowapa CCM uhalali wa kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuiba kura bila kushitakiwa mahakamani.

View attachment 3700090
Asante. Ndo nilikuwa naandaa thread. Kuna kauli kama sita zenye utata za Lema.

Tumekuwa pamoja kwenye haya mapambano pamoja.. Na ananijua na ananisoma pia.. Hii treni yetu inaenda Kigoma, naona Lema kaamua kushukia Tabora
 
Kauli mbiu kuu ya CHADEMA ni 'No Reforms No Election', yaani hakuna uchaguzi bila mabadiliko ya katiba, hii kauli ndiyo iliyompeleka Lissu gerezani.

Lema yeye anasema Katiba haina maana yeyote, inamaana anapingana na chama chake, anapingana na msimamo wa Mkiti wake anaungana na CCM wanaosema katiba haikuletei chakula mezani.

Kifupi Lema anasema tuendelee na hii hii katiba iliyowapa CCM uhalali wa kuunda serikali haramu, inayowapa CCM kiburi cha kusema majeshi yote ni mali yake. Katiba inayowapa CCM nguvu ya kuingilia mihimili yote, Bunge Mahakama na Serikali. Katiba inayowapa CCM uhalali wa kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuiba kura bila kushitakiwa mahakamani.

View attachment 3700090
Lema yuko sahihi. Mambo mengi yanayotokea sasa hivi yanakizana na Katiba. Wanaotakiwa kuilinda wameweka mbele maagizo ya wakubwa wao kuliko kufuata Katiba. Hawa hata ikija Katiba Mpya wataendelea kutekeleza amri hata kama zinapingana na Katiba. Bila mindset kubadilika, Katiba Mpya haitasaidia kitu.

Amandla...
 
Leman ana hoja, sema ukimsoma kiushabiki lazima umnange, ila he's right bila mabadiliko ya kifikra hakuna kitu katiba inaweza kusaidia.

Kama mtu anaweza kusimama wazi kusema "katiba ni kakijitabu tu" wakati huyo mtu ameapa mbele ya watanzania kuilinda, kuiheshimu na kuitunza katiba na baada ya kusema hivyo hakuna kuulizwa wala kuhojiwa, its true kwamba bila mabadiliko ya fikra hakuna kitu katiba inaweza kusaidia.

Mfano mzuri, tuna sheria za barabarani na naamini kabisa mapolisi wakisimamia vizuri kwa utashi wa kisheria tutapunguza matatizo mengi ya barabarani. Ila kwa sababu bado uwezo wetu wa kusimamia mambo ni mdogo, ona huko barabarani watu wanavunja sheria, polisi wanakula rushwa na maisha yanaenda.
 
Back
Top Bottom